Category: Uncategorized

  • Kukaza Misuli ya uume na Kuchelewa kumaliza tendo

    kukaza misuli ya uume

    Nini kinapelekea kulegea uume na Tiba gani kukaza misuli ya uume

    Uume kulegea na kushindwa kurudia tendo ndio shida kubwa kwa sasa kwa vijana wengi. Tatizo linatishia kuvunjika kwa mahusiano ya kimapenzi kwani linapelekea kushindwa kumridhisha mwanamke kitandani. Leo nitakupa ushauri na tiba ya kukaza misuli ya uume ili upige show vizuri uondoe fedheha.

    Umri unachangia misuli ya Uume kulegea

    Kadiri umri unavosonga ni wazi kwamba uwezo wa kufanya ngono
    hupungua. Lakini tafiti za hivi karibuni zinasema kwamba watu walio na umri mkubwa bado wanaendelea kujihusisha na ngono japo siyo kwa kasi kubwa kama vijana.

    Kutokana na mabadiliko ya mitindo ya kimaisha ikiwemo swala la lishe. Imetokea hata kwa vijana wa umri wa chini ya miaka 40 wanapata shida kwenye kusimamisha uume vizuri. Sababu kubwa ikiwa ni kuangalia sana picha na vidoe za X. Na tatizo ni kubwa sana kutokana na upatikanaji wa internet na smartphone.

    Nini maana ya kulegea misuli ya uume?

    Kitaalamu (Erectile dysfunction kwa kifupi ED) ni kupungua ama kutokuwa na uwezo wa kuhimili kusimama kwa uume kwa mda mrefu kwenye tendo la ndoa. Ni tatizo kubwa linalowakumba wanaume wengi hasa kwa wanaume wazee.

    Asilimia 80 ya wagonjwa wanaofika ofsini kwetu wana tatizo hili na hawawezi kuwaridhirisha wanawake wao. Kikawaida unapokuwa kwenye tendo la ndoa damu nyingi husukumwa kuelekea kwenye uume na hivo kufanya misuli kujaa na uume kusimama. Misuli inaposinyaa baada ya kumaliza kufanya ngono basi damu nyingi pia hupungua kwenye eneo la uume.

    Kupungua huku kwa uwezo wa kusimama kwa uume inaonesha kwamba kuna shida ya kiafya. Kwa wanaume wachache hali hii huchukua muda mfupi na kupotea kutokana changamoto za kawaida za kimaisha kama msongo wa mawazo, mwili kuchoka na matumizi ya pombe. Lakini kwa wanaume wengi hali hii huendelea kuwa mbaya zaidi kila wanapotaka kufanya ngono.

    Picha za Ngono na Misuli Ya uume kulegea

    Tafiti za hivi karibuni zinaonesha kuongezeka kwa tatizo la misuli kulegea miaka ya hivi karibuni. Hii inatokana na upatikanaji wa vifaa kama simu na kompyuta hivo kuwarahisishia vijana wengi uwezo wa kuingia mtandaoni kiurahisi na kutazama picha za ngono muda wowote.

    Wengi hutazama picha na video za ngono ili kujiridhisha kimapenzi na kupiga punyeto. Wanaume wanaoangalia pono wanafadhaika pale wenza wao wanaposhindwa kuwafanyia vitu kwa mtazamo kama ule kwenye pono.

    Video na Picha za X zinakufanya ushindwe kukaza misuli ye uume

    Japo kuna mchango wa mitindo fulani ya maisha kama kuwa na uzito
    mkubwa na kitambi. Lakini kutazama picha chafu za ngono zinaufanya mwili utake msisimko mkubwa sana kuliko uliozoeleka na jinsi mwili ulivoumbwa ili kuamsha hisia.

    Mazingira mengine hatarishi yanaosabisha misuli ya uume kulegea

    ED inaweza kuletekezwa na matatizo ya kiafya pamoja mitindo ya
    kimaisha kama

    • Kisukari:Wanaume wenye kisukari hasa tatizo la muda mrefu wana upungufu wa nguvu za kiume na uume kutosimama kwa nguvu
    • Shinikizo la damu: Utafiti unaonesha kwamba shinikizo kubwa la damu pamoja na uume kufeli kusimama ni vitu vinavyoenda kwa pamoja.
    • Matatizo kwenye njia ya mkojo: matatizo kwenye njia ya mkojo
      huambatana na dalili kama kupata mkojo mara kwa mara, kushindwa kutoa mkojo wote kwenye kibofu ambayo hupelekea kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa na uwezo wa kufanya ngono kikamilifu.
    • Uzito mkubwa na kitambi: Uzito mkubwa na kitambi ni chanzo kikuu kusababisha shida kwenye nguvu za kiume na kulegea kwa jogoo. Kitambi na uzito huvuruga homoni, kufanya mwili kutosikia uwepo wa insulin na hivo kiasi cha sukari kupandakwenye damu. Kiwango cha sukari kwenye damu kinapokuwa kingi hupunguza utengenezaji wa
      kichocheo cha testosterone kupungua. Testosterone ndio kichocheo kinachofanya mwanaume kuwa mwanaume kwa kuchoche hamu ya tendo la ndoa na kusaidia uzalishaji wa mbegu.
      kuishi kizembe (sedentary life) bila kushugulisha mwili na kufanya
      mazoezi:
    • Mazoezi ni muhimu kwa wanaume wanaotaka kufurahia tendo la ndoa miaka yote, kama hukujua hili basi nashauri weka ratiba sasa anza mazoezi mepesi walau mara tatu kwa week.
    • Umri: Kadiri umri unavoenda kasi na uwezo wa kufanya ngono
      hupungua kutokana na mifumo mbalimbali ya mwili kuchoka, matatizo moyo, na matatizo ya kisaikolojia na msongo wa mawazo. Pia wazee ni kundi linalotumia dawa ngi sana na hivo homoni zao kuvurugika.
    • Kuvuta sigara: wavutaji wa sigara wapo kwenye hatari zaidi ya kupata matatizo ya uzazi na misuli ya uume kulegea
      Matumizi ya vidonge vya hospitali kwa muda mrefu,mfano dawa za presha, usingizi, msongo wa mawazo, tezi dume . dawa hizi huweza kupunguza hamu ya tendo la ndoa, kushindwa kuwamwaga mbegu, na kushindwa kusisimka.

    Muhimu pambana na Chanzo cha tatizo

    Kumbuka Unapotaka kutatua changamoto ya kushindwa kusimama kwa uume, basi hakikisha unalenga chanzo cha tatizo. Kama una uzito mkubwa na kitambi hakikisha unapunguza uzito, kama ni matatizo ya mfumo wa damu na moyo basi lenga kwenye lishe utaishi kwa raha sana.

    Hatua 5 Za Kukaza Misuli ya Uume wakati unajiandaa kuanza dozi

    1.Punguza uzito mkubwa na kitambi.

    Kitambi na uzito ni adui wa afya yako, si tu katika tendo la ndoa, kitambi ni chanzo cha magonjwa mengi. Magonjwa kama kisukari, presha, ugumba na saratani. Katika safari yako ya kupunguza uzito epuka vyakula vya wanga na sukari. Tumia zaidi vyakula vya mafuta mazuri kama samaki, parachichi, nyama, mayai, karanga na nazi.

    2.Mazoezi ni muhimu kukaza misuli ya uume

    Watu wengi wamelemewa na magonjwa kwa sababu tu mwili haupati damu ya kutosha kwenda sehemu mbalimbali. Sehemu kama vile ubongo,ini, na figo ambazo ndio sehemu zenye kuufanya mwili wako ufanye kazi katika uhalisia wake.

    Hivyo basi magonjwa mengi ya mzunguko wa damu ni pamoja na nguvu za kiume. Kwasababu kama hufanyi mazoezi mwili wako unadhofika na kukosa uwezo wa kuhimili ndoa yako pia inapunguza nguvu za kiume.

    Mazoezi huimarisha mwili wako na kuweka mbali mwili wako na maradhi mbalimbali yanayo sababishwa na uzembe. Kama hujui pa kuanzia basi anza na mazoezi mepesi ya kukimbia. Kisha jaribu kegel exercise- unapokojoa hakikisha unatoa mkojo kidogo kisha unabana kwa sekunde 10 kisha ruhusu tena, fanya hivo kila unapoenda kukojoa walau mara 10 kwa kila awamu. Kegel exercise husaidia kuimarisha mishipa ya uume.

    3.Punguza msongo wa mawazo

    Matatizo ya kisaikologia kama msongo wa mawazo huathiri uwezo wako wa kufanya ngono kwa uzuri na kukupelekea heshima ya ndoa kupungua, hivo hakikisha unabalansi kazi za kimaisha zisiathiri tendo la ndoa.

    4.Punguza Wanga na Sukari

    Vyakula vya wanga ni kama ugali, wali, viazi, na magimbi. Epuka vinywaji vyote vyenye sukari nyingi,vya kusindika. Vyenye vionjo vya sukari, rangi na ladha katika afya yako kwani vyakula hivyo ni adui mkubwa sana wa afya yako. Hasa wakati unataka kurudisha nguvu za kiume.

    Kula vyakula asili, nafaka ambayo haijakobolewa,matunda kwa wingi ambayo hayasagwa yenye nyuzi nyuzi nyingi na pia juice ya matunda na mboga za majani. Utafurahia maisha ya kula vyakula asili na utafurahia ndoa yako.

    Madhara ya kutumia dawa za famasi na hospitali kiholela

    Dawa unazopewa hospitali ama kunua famasi zinaweza kukupa matokeo kwa muda mfupi sana, lakini zinaleta madhara ya muda mrefu. Madhara hayo ni pamoja na kushindwa kusimamisha kabisa uume kwa siku zinazokuja.

    Tumia tiba yetu Asili kutibu Kukaza misuli ya uume

    Hakikisha mwili wako unaupa madini ya msingi kama zinc,chuma, selenium, manganese na vitamin nyingi. Madini haya ndiyo yanafanya mwili wako ufanye kazi katika kiwango stahiki kwani huwezesha viendesha shughuli za mwili yani enzymes kufanya kazi katika kiwango kizuri na kuimarisha mwili wako.

    Virutubisho asili vya Zinc na Vig power kutoka Marekani vinafanya kazi vizuri sana katika kuimarisha misuli ya kiume, kuongeza uzalishaji wa mbegu na kusaidia wanaume wanaowahi kufika kileleni, na kushindwa kurudia tendo.

    tiba ya kukaza misuli ya uume
    Tiba ya nguvu za kiume

    Dozi ni sh 150,000/= laki 1 na 50 tu. Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze dozi na uanze kupata matokeo ndani ya siku 3 tu ukianza dozi.

  • Kuvimba Tezi dume, na Tiba Asili ndani ya Mwezi

    kuvimba tezi dume

    Nini maana ya Tezi dume?

    Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum)na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).

    Kufikia mwisho wa makala hii tayari utakuwa na ufahamu wa mambo yafuatayo

    • Maana ya tezi dume na kazi yake
    • Aina za magonjwa yanayoipata tezi dume
    • Dalili na madhara ya kuvimba tezi dume
    • Makundi ya watu waliopo kwenye hatari ya kuugua tezi dume
    • Aina za matibabu kwa tezi dume
    • Ushauri kwanini njia ya upasuaji yatakiwa kuwa chaguo la mwisho zaidi.
    • Madhara ya upasuaji kwa tezi dume na
    • Tiba ya dawa za mimea kwa tatizo la tezi dume.

    Tezi Dume ina Sifa zifuatazo.

    •  Ina umbo kama yai (oval shape)
    • Ina ukubwa wenye vipimo hivi, urefu 4cm,unene 3cm na upana 2cm , hivi vipimo vinatofautiana kwa kila mwanaume.
    • Tezi huongezeka ukubwa kadri ya umri unavoongezeka.
    • Tezi hii hutengeneza majimaji yenye rutuba ya mbegu za kiume(shahawa) yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono.
    • Pia majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ili mimba kutunga.
    • Tezi pia inasaidia kupunguza hali ya kitindikali (acidic condition)  iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa,inaua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa shida.

    Kuvimba Tezi Dume Husababishwa na nini?

    Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.

    Dhana (theories) kadhaa Zinazoelezea chanzo cha BPH. Dhana hizo ni pamoja na

    • Uhusiano kati ya tezi dume na homoni ya estrogen: Wanaume huzalisha testosterone, homoni ya muhimu sana katika mwili wa mwanaume. Hali kadhalika huzalisha pia estrogen ambayo ni homoni ya kike kwa kiwango kidogo sana. Kadiri jinsi mtu anavyozeeka, ndivyo uzalishaji wa testosterone unavyokuwa mdogo na kufanya kiwango chake katika damu kupungua kulinganisha na kiwango cha estrogen ambacho huongezeka kwa kiasi fulani. Pamoja na kazi nyingine, estrogen pia huchochea ukuaji wa chembe hai za mwili. Tafiti zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha kuwa tezi inavimba kwa sababu kiwango kikubwa cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya tezi dume kuvimba.
    • Kuvimba tezi dume na Dihydrotestosterone (DHT):  DHT ni kiasili kinachozalishwa kutokana na testosterone kwenye tezi dume, ambacho husaidia kuthibiti ukuaji wa tezi dume. Ingawa wanyama wengi hupoteza uwezo wa kuzalisha DHT wanapofikia umri wa uzee, baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa, kwa binadamu, hata kama kiwango cha testosterone kitapungua sana katika damu, wanaume watu wazima bado wana uwezo wa kuzalisha kiasili hiki cha DHT katika tezi dume zao. Uzalishaji huu wa DHT huchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa seli za tezi dume na kusababisha BPH. Wanasayansi wamegundua kuwa wanaume watu wazima wenye kiwango kidogo cha DHT hawapati BPH.
    • Uhusiano kati ya BPH na maelekezo ya seli.                                       Dhana nyingine inasema kwamba baadhi ya seli kutoka katika sehemu fulani ya matezi yanayohusika na ukuaji mwilini hupewa maelekezo wakati mtu anapokuwa bado mdogo. Seli hizi hutunza maelekezo hayo na baada ya miaka kadhaa maelekezo haya huanzwa kutekelezwa na seli za matezi mengine. Mojawapo ya melekezo hayo ni kuchochea ukuaji wa tezi dume na kusababisha BPH.

    Dalili za Kuvimba kwa Tezi Dume

    • Kupata mkojo mara kwa mara
    • Kubakiza mkojo kwenye kibofu
    • Kukujoa sana usiku
    • Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa
    • Kupungukiwa nguvu za kiume
    • UTI ya mara kwa mara
    • Mawe kwenye kibofu kutokana na mrundikano wa mkojo.
    • Figo kujaa maji. Hii sababu mkojo huo unarudi nyuma kuelekea figo (hydronephrosis)
    • Kupoteza fahamu(uremia)

    Madhara ya Kuvimba Tezi Dume

    Kuvimba tezi dume kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na

    • Mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu
    • Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
    • Mawe kwenye kibofu cha mkojo
    • Kuugua UTI sugu
    • Madhara katika figo au kibofu
    • Shinikizo la damu
    • Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
    • Nimonia
    • Damu kuganda

    Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa hapo juu, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi. Vipimo vyaweza kutofautiana kati ya mgonjwa namgonjwa, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na

    Vipimo kugua kuvimba kwa tezi dume

    1.Kkuchunguza kupitia njia ya haja kubwa

    Hiki ni kipimo cha kwanza kabisa ambacho mgonjwa hufanyiwa na daktari wake. Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake katika njia ya haja kubwa kisha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la .

    2.Kipimo cha damu cha Prostate specific antigen (PSA)

    PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.

    3.Utrasound ya eneo la haja kubwa(Rectal Utrasound)

    Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humuwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.

    4.Kipimo cha kuchunguza kibofu cha Mkojo Yaani Cytoscopy

    Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Pia kinawezesha kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.

    Matibabu ya Tezi Dume.

    Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo. Aidha matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.

    Matibabu kwa Njia ya Dawa

    Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake.

    Matibabu kwa Njia ya Upasuaji

    Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha mafanikio yeyote.

    Tiba ya kutumia Joto la maji (Water-induced thermotherapy):

    Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume. Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH.

    Aina Za Upasuaji wa Tezi dume

    Zipo njia nyingi za upasuaji wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo (Transurethral surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open surgery), upasuaji wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume Laser surgery), na upasuaji wa kutumia joto la fibreoptic probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser coagulation).

    Madhara Ya Upasuaji

    1. Kukosa uwezo wa kufikia kishindo yani hutoi shahawa(retrogade ejaculation) wazee wengi hulalamika sana baada ya hizi operation hivyo ushauri nasaha lazima utolewe ili mgonjwa ajue nini madhara yake kabla ya operation.
    2. Kuziba kwa njia ya mkojo kutoka na kuumia kwa njia hizo wakati wa kitendo hicho. Baadaya ya upasuaji mgonjwa anapoendelea kupona kovu linaweza kuziba njia ya mkojo.
    3. Shida ya kushindwa kudhibiti mkojo usitoke ovyo (Incontinence): Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kudhibiti kutoka kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.
    4. Kutokwa na damu katika siku za awali mara baada ya upasuaji kupitia njia ya mkojo: Kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo itaonekana katika mkojo.
    5. Wanaume kuwa wagumba yaani wasioweza kupata watoto. Kwa kawaida, wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani huingia kwenye urethra karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo. Wakati wa tendo la ngono, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume. Hata hivyo, upasuaji wa tezi dume huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.

    Tiba zetu Asili Zimetuletea shuhuda Nyingi za Kupona Tezi dume, bila Upasuaji kupitia hizi dawa mbili

    1. LYCOPENE

    Lycopene

    Lycopene ina uwezo wa kupenya kwenye tezi dume na kusafisha seli zilizokufa pamoja na kuzuia kabisa kukua kwa tezi dume. Pia ina uwezo mkubwa wa kuzuia kansa ya tezi dume. Hivyo tunashauri kila mtu mwenye umri wa miaka 40 atumie dawa hizi ili kujilinda na tezi kukua. Utumiapo lycopene iliyotengenezwa kwa kiwango kingi(concentrated) kuna uwezekano mkubwa wa kutopata kabisa tezi hii dume.

    Lycopene inashauriwa kutumiwa pia kwa wagonjwa wa tezi dume ambao tayari wanaugua.

    2.PROSTACARE

    Prostacare

    Dawa hii ni ya kiasili imetengenezwa kwa kutumia viambata vya Extractum of Radix Rehmanniae, Rhizoma Anemarrhenae, Cortex Phellodendri Chinsis, Herba Ecliptae, Fructus Ligustri Lucidi, Harba Plantaginis, Radix Paeoniae Rubra Ambavyo kwa pamoja husaidia

    • Kuboresha mzunguko wa damu ndani ya tezi dume
    • Kuzuia kuzaliana kwa wadudu wabaya ndani ya tezi dume
    • Kuondoa dalili za matatizo ya tezi dume
    • Inafaa kwa mwanamme mwenye tatizo lolote la tezi dume na inawafaa pia wanaume wenye umri unaozidi miaka 40 kwaajili ya kujikinga na magonjwa ya tezi dume.


    Ushuhuda wa Mgonjwa Kupona Tezi Dume.

    Tarehe 28 january mwaka 2018 Bwana Eliudi (Jina siyo halisi ili kutunza siri ya mgonjwa)kutoka Mbeya alinitumia ujumbe huu hapa chini kupitia namba yangu ya huduma ya whatsapp akinieleza kuhusu dalili za maumivu wakati wa kukojoa na kupata mkojo kwa shida.

    Baada ya kuanza kupata dalili hizi alienda kufanya vipimo na ndipo aligundulika kwamba tezi dume imeanza kukua kupita kiasi.
    Nilimweleza bwana Eliudi kuhusu madhara ya kukua kwa tezi dume na pia utaratibu na gharama za dawa zetu namna zinavoweza kutibu na kurudisha furaha yake.
    Siku iliyofuata Bwana Eliudi alifanya malipo ya dawa kisha tukamtumia dawa aina mbili ambazo ni Prostacare na Lycopene,na tarehe 1 February alianza dozi yake. Tar 5 mwezi huo wa pili nilimtumia meseji bwana Eliudi kutaka kujua maendeleo yake na ndipo nilishtuka pale aliponambia ameanza kupona ndani ya siku 5 pekee tangu aanze kumeza dawa. Huu ni ujumbe wake alionitumia.

    Ushuhuda wa kupona tezi dume

    Naamini nawe ungependa kupona tatizo lako, basi karibu tukuhudumie uwe miongoni mwa mashuhuda wetu. Kumbuka siyo lazima uanze kuumwa tezi dume ndipo upate tiba. Wanaume wote wenye umri kuanzia miaka 40 wanafaa kutumia virutubisho hivi ili kujikinga na tatizo la kukua kwa tezi dume.
    Maelezo ya ushuhuda tumetoa kwa ruhusa ya bwana Eliudi siyo uamuzi wetu kuanika siri za mgonjwa.

    Gharama ya dawa hizi inaweza kuwa juu lakini tunakuhakikishia kupona tatizo lako na kurudi kwenye hali ya kawaida kama utafata maelezo sahihi ya kutumia dawa.

    Jumla kuu kwa dawa hizi mbili utalipia Tsh 195,000/=

    Ofisi zetu zipo Mwembechai Dar, Chati na Daktari kwa Whatsapp kupitia namba : 0678626254 kupata tiba haraka.

  • Njia 5 za kurudisha Nguvu za kiume ndani ya Mwezi tu

    tiba ya nuguvu za kiume

    Upungufu wa nguvu za kiume kwa vijana

    Vijana wa umri wa miaka 20 hadi 30 ndio wanao ongoza kwa kusumbuka na matatizo haya ya nguvu za kiume. Tofauti na matarajio yetu wote kuwa tatizo hili tunasoma kuwa linawapata wazee. Swali la kujiuliza kwa nini sasa vijana tena katika umri mdogo?

    Ndio maana nimeamua kukuandikia makala hii. Ukimaliza kusoma makal hii nina uhakika tatizo lako utapata suluhisho kutokana na elimu hii ili uache tena kutia aibu kitandani.

    Upungufu wa nguvu za kiume inaleta hofu na mawazo

    Usiwe mkimya kwani inahitaji utashi wa juu sana kumweleza mwenzi wako kuhusu hili swala. Kwani upungufu wa nguvu za kiume unasababisha msongo wa mawazo . Mbali na hivyo husababisha kutokujiamini na woga wa kuwa na mwanamke.

    Wengi wamejaa wasiwasi na hofu kubwa ya kugunduliwa na mwezi wake kuwa ana tatizo hilo. Na wengi wao ni woga sana kutogunduliwa tatizo hilo. Ndio maana inapofikia hatua mwenza wako umembaini ni mara chache sana atakubali kuwa kweli hujamfiskisha kileleni kwa kuogopa kwamba atakukwaza. Kwa nini usumbuke na matatizo kama haya wakati tiba ipo?

    Nini husababisha upungufu wa nguvu za kiume.

    Katika mwili wa binadamu kuna homoni/vichocheo aina ya testosterone ambavyo vinazalishwa. Malengo ni kuimarisha utendaji kazi wa ubongo, ufanye kazi katika hali tulivu, kuondoa msongo na kuondoa mstuko wa aina yoyote.

    Kazi zingine za homoni ya testosterone ni kuimarisha uwezo wa kufikiri, kuimarisha nguvu za kiume na hatimaye kufurahia tendo la ndoa. Kazi kubwa ya kichocheo hiki ni kuhakikisha mwili wako unakuwa katika hali tulivu kabisa kwa kuutuliza ubongo wako ndipo utafurahia sex.

    Homoni ya Testosterone inasaidia Nguvu za Kiume

    Kichocheo hiki ndio silaha ya mwanaume kwani ndicho kichocheo kinachokufanya uwe na sifa zote za kiume. Na ndicho kichocheo ambacho kinakufanya uwe imara katika tendo la ndoa. Upungufu wa kichocheo hiki kinasababisha kupungua kwa matamanio kwa jinsia tofauti, kupungua kwa nguvu za misuli yako kiutendaji, mafuta kurundikana ovyo mwilini.

    Lakini pia ijulikane kuwa kichocheo hiki cha testosterone sio kwamba kinapatikana kwa wanaume tu, la hasha! Kichocheo hiki hata wanawake wanacho ingawaje kwa kiwango cha chini sana. Endapo kinapokuwa kimepungua kinaweza kumsababishia mwanamke kukosa matamanio kwa jinsia ya kiume wakati wa tendo la ndoa, kukosa nguvu ya misuli ya kuhimili tendo la ndoa ama kuchoka sana, kuongezeka uzito kupita kiasi na nyama uzembe pia kupunguza uwezo wako katika kufikiri na kumbukumbu.

    Vitu 4 vinavyo angamiza nguvu zako za kiume na kukuacha mwenye msongo wa mawazo 

    1.Vinywaji vyenye sukari nyingi kama soda

    2.Kuepuka kabisa ulaji wa vyakula vya mafuta haya yale mazuri

    3.Vyakula vyote vya kusindika viwandani

    4.Sumu mbali mbali kutoka kwenye mazingira

    Njia tano za kurudisha nguvu za kiume

    Najua umekuwa ukisumbuka kila siku kufurahia ndoa yako, hadi imefikia hatua mbaya. Najua umekuwa mnyonge na mwoga wa kugundulika kwa mwenza wako kuwa unasumbuka na tatizo hilo. Umejaa woga, umegubikwa na msongo wa mawazo na umekuwa ukizunguka kila sehemu upate msaada na hatimaye umekuwa ukitoa pesa bila hata kurudisha furaha ya ndoa yako na nafsi yako!

    Pole kwa changamoto lakini elimu ni bora kuliko yote yaliyokupata. Hebu soma hiki ambacho nimekuwa nikipewa asante kila siku na wagonjwa wangu wewe pia uwe miongoni mwao.

    1. 1.Epuka vinywaji vyote vyenye sukari nyingi,vya kusindika, vyenye vionjo vya sukari,rangi na ladha.
    2. Fanya mazoezi ya kutosha walau mara 4 kwa week
    3. Rudisha Virutubisho Vilivyopungua mwilini mwako
    4. Ondoa mafuta mabaya yanayopunguza mzunguko wa damu. Mafuta haya huitwa bad cholesterol
    5. Safisha Sumu mwilini kwa kutumia viondoa sumu unaweza kutumia tiba zetu asili kusafisha sumu bila madhara

    GREEN HEALTH MALE SEX DRIVE PACKAGE

    Tiba yetu ina combination ya dawa mbili za vig power na zinc tabltes zitakusaidia

    1. Kuimarisha uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa kuchelewa mpaka dakika 30 kwa bao moja
    2. Kuongeza uzalishaji wa mbegu(sperm count) na ubora wa mbegu(sperm quality)
    3. Kuimarisha mzunguko wa damu kuelekea kweye uume na hivo kukufanya usichoke mapema unapofanya ngono

    Inafaa kwa wanaume wote wanaowahi kufika kileleni, kukosa hamu ya tendo la ndoa na wanaoshindwa kuwapa mimba wanawake.

    Gharama ya Tiba ni Tsh 150,000/= ambayo utaitumia kwa week 4 kudisha nguvu za kiume. Virutubisho na dawa zetu ni za asili zipo katika

    Ofisi zetu zipo hapa Dar salaam na mikoani tunatuma dawa
    Tuandikie kwa namba 0678626254 kupata tiba kwa Tsh laki 1 na 50 tu ili uwe shuhuda wetu.

  • Kukoma hedhi, ukavu ukeni, kukosa hamu ya tendo na tiba asili

    kukoma hedhi

    Kukoma hedhi au kwa kitaalamu menopause ni hali ya kawaida inayomtokea kila mwanamke. inatokea pale kupata hedhi kunapofikia kikomo na hivo uwezo wa kupata mimba au ujauzito kushuka na kukoma kabisa. Hatua hii hutokea pale mwanamke anapofikisha umri wa miaka 50 na kuendelea.

    Kwa wanawake wengine hali hii hutokea pia kabla ya hapo kuanzia miaka 40. Na inaweza kutokea kutokana na ushauri wa madactari ama kufanyiwa upasuaji mdogo. Mfano mifuko ya mayai(ovaries) na mfuko wa mimba (uterus) inapoondolewa  kutokana na athari ya magonjwa mbalimbali kama saratani.

    Pale mwanamke anapofikia umri wa kukoma hedhi basi huanza kuona dalili zifuatazo

    • Mifupa kuwa dhaifu sana
    • Joto kupanda mara kwa mara na kupata jasho jingi
    • Ukavu kwenye uke na uke kuwa mdogo kama wa mtoto
    • Kubadilika badilika kwa mpangilio wa hedhi
    • Kuongezeka uzito sana
    • Msongo wa mawazo na kubadilika kwa mood yako.

    Nini ufanye kuondoia dalili mbaya za kukoma hedhi?

    Kuna njia za mda mrefu na njia za mda mfupi kutibu madhara ya kukoma hedhi. Njia nzuri na kuepusha madhara yanayotokana na  kukoma hedhi ni kuerekebisha lishe yako na kufanya mazoezi ya viungo. Kwa kuzingatia lishe waliyokula mababu zetu hapo zamani basi utapunguza madhara ya kukoma hedhi kama kuongezeka uzito na kutokwa na jasho jingi hasa kipindi cha usiku.

    Tambua kwamba kukoma hedhi siyo ugonjwa

    Kama tulivoona hapo juu pale mwili wa mwanamke unapokoma kutengeneza homoni za estrogen na progesterone ndipo hedhi yako itakoma. Wanasayansi huenda mbali zaidi na kuwaanzishia wahanga wa tatizo hili program ya kurudisha homoni hizi kwa kuwawekea homoni zilizotengenezwa maabara.

    Kitendo hiki hufahamika zaidi kama hormone replacement therapy. Njia hii inatazama ishu ya kukoma hedhi kama ugonjwa wakati ni suala la kawaida kabisa linalomkuta kila mwanamke. Ukweli ni kwamba kitu chochote kilichotengenezwa kwa mkono wa binadamu hakitafanya kazi sawa na kitu kilitengenezwa halisi kwa ajili ya kazi fulani kwenye mwili. Ndio maana madhara ya kuwekewa homoni hizi ni makubwa zaidi.

    Njia asili za kutumia ili upunguze dalili mbaya zinazotokana na kukoma hedhi.

    1. Tumia virutubisho/supliments kama virutubisho vya mafuta ya samaki(fish oil) yenye Omega 3 , vyenye ubora wa hali ya juu, kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika.
    2. Zinc supliments: Kwa wanawake, Madini ya Zinc yanahusika katika ukuuaji wa yai (oocyte). Kama mwanamke atakuwa na upungufu wa zinc, yai halitakomaa vizuri na utolewaji wa yai (ovulation) utazuiliwa , na kusababisha ugumba. Kiwango cha zinc cha kutosha kunamwezesha mwanamke kutumia estrogen na progesterone vizuri.
    3. Ovary Nutrition: Vidonge hivi vilivyotengenezwa kiasili kwa kutumia viambata vya mimea ya Glycine, Radiz Paeoniae Alba Eztractum na Ganoderma husaidia: kuongeza ufanyaji kazi wa mfuko wa mayai (ovaries), kuzuia Saratani ya matiti na kuimarisha afya ya mifupa kwa wanawake waliokoma hedhi.(menopause).
    kukoma hedhi

    Ushauri mwingine muhimu sana

    1. Hakikisha mlo wako unakuwa na kiasi sawa cha vyakula vya mafuta yale mazuri, kwa wingi ikifuatiwa na protini na kisha matumizi ya wanga na sukari kwa kiasi kidogo sana
    2. Epuka matumizi ya vyakula na vinywaji vilivyosindikwa maana huongeza kiasi cha homoni ya estrogen.
    3. Hakikisha unakuwa na ratiba nzuri ya kufanya mazoeziili kurekebisha kiwango cha insulin na hivo kusaidia kubalansi kiwango cha estrogen.
    4. Pata vitamin D ya kutosha, miili yetu ina uwezo wakutengeneza vitamin D kutoka kwenye mwanga wa jua, hivo hakikisha kila siku unapata mwanga wa jua walau nusu saa mpaka saa 1 ili kuuwezesha mwili kutengeneza Vitamin D ya kutosha. Tafiti zinaonesha kuwa Vitamin D husaidia kupunguza athari za zinazotokana na kukoma hedhi kama kutokwa na jasho jingi usiku bila kumeza vidonge.
    5. Kupunguza uzito husaidia kurekebisha na kupunguza athari za menopause kama kubadilika kwa joto la mwili: Tafiti zinasema kwamba wanawake wanaopunguza uzito ama walio kwenye program za kupunguza uzito wana uafadhali katibu 33% zaidi ya kupunguza athari za menopause kuliko wanawake wengine.

    Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 upate dawa kwa tsh 90,000/= tu ili kutibu maudhi ya kukoma hedhi kama, ukavu ukeni, kuongeza uteute ukeni, hamu ya tendo,kurejesha ubora wa mashavu ya uke.

  • Uvimbe kwenye kizazi na tiba yake asili bila upasuaji

    Uvimbe kwenye kizazi yaani Fibroids ni uvimbe ambao siyo wa saratani unaojitokeza kwenye kuta za mfuko wa kizazi. Uvimbe huu husababisha kubadilika kwa shape na size ya kizazi na pia dalili zingine mbaya. Mgonjwa huanza kupata maumivu makali wakati wa hedhi kutokana na uvimbe kwenye kizazi yaani fibroids .

    Unajuaje kama tayari una uvimbe kwenye kizazi

    Hapa chini ni ni dalili za kukwambia kwamba tayari kuna uvime kwneye kizazi

    1. Kupata Hedhi inayochukua siku nyingi kuanzia 7 na zaidi
    2. Hedhi nzito ya mabonge
    3. Kujiskia umeshiba mda mwingi
    4. Maumivu ya nyonga
    5. Kupata mkojo mara kwa mara na kushindwa kukujoa mkojo wote
    6. Kukosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu
    7. Kupata maummivu kwenye sex
    8. Maumivu makali kwenye mgongo wa chini
    9. Kukosa mimba mda mrefu yaani ugumba na mimba kuharibika mara kwa mara

    Mambo haya yanaongeza chansi kwa mwanamke kupata uvimbe kwenye kizazi

    • Umri Mkubwa: uvimbe kwenye kizazi yaani fibroids inatokea zaidi kwa wanawake wanaokaribia kukoma hedhi kuanzia miaka 35 mpaka 40.
    • Kurithi kwa familia: kama mama au dada  yako aliugua uvimbe hapo zamani basi wewe pia utakuwa kwenye hatari zaidi ya kupata uvimbe huu.
    • Lishe mbaya: matumizi ya vyakula vya wanga na sukari kupita kiasi yanaongeza chansi ya kuugua fibroids
    • Uzito mkubwa na kitambi: wanawake wenye uzito mkubwa na kitambi wako kwenye hatari zaidi ya kupata uvimbe
    • Wanawake wenye presha kubywa ya kupanda
    • Matumizi ya uzazi wa mpango wa kisasa: kama vidonge huongeza ukuaji wa fibroids kwani vidonge hivi huweza kupandisha homoni ya estrogen kwa wingi
    • Kubalehe mapema sana: wanawake wanaovunja ungo mapema Zaidi na kuanza kupata hedhi chini ya miaka 11 wako kwenye hatari zaidi ya kuugua fibroids na
    • Wenye matatizo ya tezi ya shingo yaani thyroids

    Jaribu Tiba yetu asili kwa ajili Upone Uvimbe Haraka bila upasuaji

    Kwa mwanamke mwenye uvimbe kwenye kizazi(fibroids) chini ya cm 3 nakushauri kutumia tiba zetu asili za kanchnar gugglu kutoka India .Dawa inatumika ndani ya mwezi mmoja na lengo ni kupunguza vimbe na kuziondoa kabisa. Dawa zipo kwenye mfumo wa vidonge 80. Dozi ni kwa unameza 2×2 kila siku. Kabla hujawaza upasuaji, njoo nikupe hizi tiba upone na urudishe furaha yako

  • Mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa na tiba asili

    mwanamke kukosa hamu ya tendo

    Nini kinapelekea mwanamke kukosa hamu ya tendo?

    1. Kuvurugika homoni ama vichocheo kunapelekea kukosa hamu ya tendo
      Utajuaje kama homoni zako zimevurugika? angalia kama unapata dalili za hedhi kuvurugika, kuota ndevu, mwili kuchoka sana na mood kubadilika, uzito mkubwa na kitambi, na kupoteza kumbukumbu.
    2. Uvimbe kwenye kizazi inapelekea mwanamke kukosa hamu ya tendo . Uvimbe huu kitaalam tunaita fibrod au myoma. uvimbe unaanza kudogo kama punji na unaweza kuwa mkubwa kama mpira endapo hautaondolewa mapema.
    3. Kutumia uzazi wa mpango wa kisasa inachangia mwanamke kukosa hamu ya tendo. Kama hakuna ulazima basi acha kutumia njiti, sindano, vidonge na kitanzio kupanga uzazi. Tumia njia asili kama kalenda
    4. Kukoma hedhi au menopause: wanawake wemgu wakifika miaka 40 wanaanza kukoma hedhi na hapo shida ya uke mkavu inapoanzia. Kama uko kwenye hili kundi kuna dawa maalumu tutakupa ikusaidie urudi ujana wako.
    5. Kutofika kileleni vizuri: Hii ni sababu mojawapo ya mwanamke kukosa hamu ya tendo, kama hakojozwi vizuri kitandani wakati wa tendo, aidha kwa mtu wake kukosa ufungi au shid ya homoni

    Tiba asili kwa tatizo la mwanamke kukosa hamu ya tendo

    Kama hujafurahia tendo tangu uzaliwe, au hujafurahia kwa miaka mingi, na huna kabisa hamu ya tendo basi hapa upo sehem salama. Hakikisha tu kama unatumia uzazi wa mpango wa kisasa basi utoe kwanza, kisha tuykupe dawa.

    Dawa zipo makundi mawili.

    1. Dawa kwa wenye umri mdogo chini ya miaka 40 (soy power)
    2. Dawa ya wamama watu wazima Zaidi ya miaka 40 ambao bado wanaopwata hedhi au tayari walishakoma hedhi(ovary nutrition)
  • Fangasi ukeni na Tiba Asili

    fangasi ukeni

    Fangasi Ukeni Husababishwa Na Nini?

    1. Mabadiliko ya mazingia ya uke inapelekea fangasi ukeni
      Vimelea hawa wa Candida Albicans ambao ndio hupelekea fungus, kawaida wanapatikana katika midomo, koo la kupitishia chakula, kibofu cha mkojo, uume au katika uke na kwenye ngozi pia. Kuhamisha vimelea hawa kwenda eneo linguine la mwili inapelekea uugue. Mfano kutoa kwenye mkundu mpaka kwenye uke.
    2. Kupungua kwa Kinga ya mwili kutokana na magonjwa mbalimbali inapelekea kukua kwa Candida. Ndiomaana wagonjwa wa ukimwi na saratani au wanaopata matibabu ya mionzi huwa kwenye hatari kubwa ya kuumwa fangasi ukeni

    Makundi ya watu wanaougua Zaidi fangasi ukeni

    • wanawake wanaofanya ngono mara kwa mara na watu tofauti tofauti bila kinga yani kavu
    • kufanya ngono kupitia mdomo(oral sex)
    • matumizi makubwa ya kondomu kwenye tendo
    • matumizi makubwa ya pedi au pantliners
    • Wanawake wanaoosha uke kila mara/usafi kupitiliza na
    • wanaotumia manukato ukeni
    • Wagonjwa wa kisukari na
    • Wanaokula madawa kwa mda mrefu

    Dalili za fangasi ukeni

    • Kuwashwa sana ukeni
    • Kupata aumivu makali wakati wa tendo
    • Kuhisi kuwaka moto ukeni baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa au kutoka kukojoa.
    • Kupata vidonda ukeni (soreness) .
    • Kuvimba na kuwa mwekundu katika mdomo wa uke
    • Kupata maumivu wakati wa kukojoa na
    • Kupata uchafu ukeni wa rangi nyeupe au kijivu mwepesi au mzito

    Matibabu ya Uhakika na asili kwa Fangasi ukeni

    Mwanamke mwenye fangasi sugu , tunashauri atumie Uterus cleansing pill kusafisha kizazi ili kuondoa maambukizi haya. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 2 vilivyotengenezwa kitaalamu zaidi kwa kuzingatia uasili wa dawa kutibu fangasi ukeni. Baada ya dozi utapona, muwasho, uchafu na harufu mbaya ukeni na PID.

    Matumizi ya dawa

    Vidonge hivi asili vinatumika kwa wiki moja. Unaweka ukeni kidonge kimoja na kisha unatoa baada ya siku 3, kisha unapumzika masaa 24 ,unaweka tena kidonge kingine. Usitumie wakati wa hedhi na kama una mimba.