Tag: Aleji ya chakula

  • Kinga+ Tiba ya Aleji pamoja Ushauri wa daktari

    aleji ya ngozi

    Mzio yaani aleji ni Matokeo ya uliyopitiliza kati ya mpambano wa kinga ya mwili na kitu chochote ambacho kwa ujumla huwa hakina madhara kwa mwili inapotokea kimeingia ndani ya mwili au kimegusa sehemu fulani ya mwili.

    Aleji husababishwa na nini ?

    kinga ya mwili huulinda mwili dhidi ya vitu mbalimbali hatari kwa afya kama vile vimelea vya bakteria na virusi, lakini wakati mwingine inaweza kupambana pia na vitu ambavyo havina madhara yeyote kwa mwili ambavyo huitwa allergens. Watu wenye aleji/mzio huwa na hisia zisizo za kawaida za mwili dhidi ya baadhi ya vitu.
    Mwili unapokumbana na vitu vinavyosababishia aleji (yaani allergens), mfumo wa kinga ya mwili huzalisha kemikali mbalimbali ikiwemo histamine ambayo hupambana na allergens hizo. Mpambano huu ndo husababisha mtu kuwa na dalili za aleji/mzio kwasababu mpambano unapelekea mwili kureact kama vile umeona adui.

    Vinasaba na aleji

    Matatizo ya vinasaba pamoja na hali tofauti tofauti za kimazingira zote zinahusika sana katika kusababisha mtu kuwa na aleji. Baadhi ya vitu vinavyosababisha aleji ni pamoja na vumbi, baadhi ya dawa, baadhi ya vyakula, kung’atwa na wadudu kama vile nyuki, aina fulani ya uyoga, vumbi vumbi la maua (pollens) Harufu kama manukato, viungo vya vyakula. Wapo baadhi ya watu ambao hukumbana na mzio pindi wanapokuwa katika mazingira ya joto au baridi wakati wengine hupatwa na mzio pindi wanapopigwa na jua kali. Nyakati zingine hata msuguano kidogo tu wa ngozi unaweza kuwasababishia baadhi ya watu dalili fulani fulani za mzio.

    Je aleji inaambukizwa kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto?

    Kwa kawaida, aleji ya aina fulani huwa haurithishwi miongoni mwa wanafamilia. Mfano kama mzazi ana aleji na baridi si lazima watoto wake pia wawe na aleji hiyo hiyo ya baridi ingawa wanaweza kuwa na aina nyingine ya aleji. Uwezekano wa mtoto kupata aleji huongezeka zaidi iwapo wazazi wote wawili wana aleji na vitu fulani fulani na huwa mkubwa zaidi iwapo mama ndio mwenye aleji.

    Dalili za mtu mwenye ALeji

    Dalili za aleji zipo nyingi kuendana na eneo gani la mwili linahusika. Kwa ujumla hizi hapa chini ndio dalili za alajei kufuatana naeneo la mwili.

    1. Mfumo wa hewa: Mtu anaweza kuwa na matatizo katika kupumua (kikohozi au kubanwa na pumzi, makamasi na kuziba kwa pua, muwasho kwenye pua na koo, au kupumua kwa kutoa sauti kama mtu anayepiga filimbi.
    2. Macho: Muhusika hujihisi hali ya kuchoma choma, kutokwa na machozi na muwasho kwenye macho, macho kuvimba na kuwa mekundu
    3. Vyakula: Endapo mtu atakula kitu ambacho ana aleji nacho anaweza kuwa na dalili kama vile kuharisha, kichefuchefu, kutapika, Kusokotwa au kuumwa na tumbo na pia kupoteza fahamu.
    4. Ngozi:Ngozi inaweza kuwa na mabaka mabaka, kubabuka, kuvimba, muwasho, kuota vipele na malengelenge, michubuko au ngozi kuwa nyekundu.
    5. Aleji za mwili mzima: hizi zinakuwa na mkusanyiko wa dalili zote za hapo juu

    Vipimo na uchunguzi kugundua aleji

    Unapoenda kumwona daktari wa Ngozi utaratibu unaweza kuwa kama nilivoeleza hapa chini

    Mgonjwa akiwa na daktari ataulizwa kuhusu historia ya tatizo lake, ni lini lilianza na vitu gani humfanya awe hivyo. Aidha tabibu pia atapenda kufahamu kuhusu dalili nyingine zinazoambatana na tatizo linamlomkabili mgonjwa.

    Baadaye vipimo vya aleji vinaweza kufanyika ili kufahamu hasa ni kitu gani mgonjwa ana aleji nacho na kama kweli dalili alizonazo mgonjwa ni kweli zinatokana na aleji au zinatokana na sababu nyingine. Hii ni kwa sababu kuna baadhi ya mambo yanaweza kumsababishia mtu kupatwa na dalili zinazofanana kabisa na mtu aliye na aleji ya kitu fulani.

    Je kuna madhara ya aleji?

    Madhara ya aleji ni pamoja na kupata shambulio kali la mcharuko wa mwili ambalo linaweza kusababisha kifo kama usipotibiwa haraka. Wapo baadhi ya watu, kwa mfano, wakila wadudu kama senene na kumbi kumbi wanvimba mwili na kushindwa kupumua mpaka kuhitaji kulazwa hospitali na kusaidiwa kupumua kwa mashine. Madhara mengine ni pamoja na shida ya kuvuta pumzi au kushuka kwa shinikizo la damu.

    Namna ya kujikinga na Aleji

    Pindi mtu anapopatwa na aina fulani ya aleji, kinga bora ni kukwepa mambo yote yanayoweza kuchochea kutokea kwa shambulizi la aleji. Kama ni chakula, jitahidi kukwepa aina hiyo ya chakula na kama ni dawa mf dawa zenye sulphur, acha matumizi yake na pia mueleze daktari wako au muuguzi kuhusu hali hiyo mapema kabla hajakupa dawa hizo.

    Je ni kweli Aleji inatibika?

    Njia bora kabisa ya kutibu na kupunguza uwezekano wa kupata aleji ni kutambua kitu au vitu vinavyokusababishia hali hiyo na kuviepuka. Kama ni chakula au dawa au kemikali, epuka kabisa matumizi yake, na kama ni vumbi jitahidi kukaa nalo mbali.

    Tumia tiba zetu asili kutibu aleji

    Kama una aleji, usiache kutucheki kwa namba zetu tukupe ushauri na tiba asili.

    Tuandikie kwa WhatsApp namba yetu 0678626254 uanze dozi.

  • Aleji ya Chakula, Ushauri na Dawa za Kutibu

    aleji ya chakula

    Nini kinasababisha Aleji Ya Chakula?

    Ndani ya seli za mwili kuna kemikali zinazoitwa histamine. Kazi ya histamine ni kuiruhusu kinga ya mwili kupambana na kitu chochote kigeni ambacho kimeleta athari kwenye tishu zako. Kinga ya mwili inaweza kupambana na kitu chochote ambacho kinaleta shida kwenye mwili mfano vimelea vya ugonjwa, hewa chafu, virusi, bacteria, baadhi ya vyakula nk.

    Kwahiyo tunaelewa sasa kwamba histamine husababisha aleji juu ya chakula fulani. Maana yake umekula lakini mwili unaonesha kukikataa chakula hicho kwasababu mwili umeona kinaweza kuleta madhara makubwa. Kemikali hii ya histamine ndio inaleta matokeo kama kutapika, kukohoa au kujikuna.

    Dalili Zinazoletekezwa na Aleji ya chakula

    Viashiria kwamba una aleji ya chakula vinaonekana, ndani ya dakika au masaa kadhaa baada ya kula chakula husika. Dalili hizi tunaziita allergic reactions ni kama

    • Malengelenge yanayowasha kweye ngozi.
    • Mdomo kuvimba, kutetemeka na kuwasha
    • Ulimi kuvimba, koo na uso
    • Kutapika na Kuharisha
    • Maumivu ya tumbo
    • Kukohoa sana na mafua makali
    • Mwili kuchoka sana na kujiskia uvivu
    • Kupumua kwa shida ma pumzi kukata
    • Kupoteza fahamu

    Food allergy na Food intolerance ni tofauti na aleji ya chakula

    Wakati mwingine ni vigumu sana kwa madaktari kugundua chanzo cha aleji yako. Hii ni kutokana na kwamba kuna vitu viwili, aleji ya chakula(food allergy) na mwili kutovumilia uwepo wa chakula fulani(food intolerance). Tofauti na aleji ya chakula ambayo ni matokeo ya kinga kupambana na kitu kinachoingia.

    Mwili kutovumilia chakula fulani ni kwa sababu aina ya chakula haiwezi kumng’enywa na mwili, mfano kwa watu wengi miili yao haiwezi kumeng’enya vyakula vya ngano na maziwa, vyakula vilivyoongezwa ladha na rangi .

    Watu wanaopata aleji juu ya chakula fulani ni muhimu kuacha kutumia aina hiyo ya chakula mapema iwezekanavyo.

    Madhara ya kiafya kuwa na aleji ya chakula ya mda mrefu

    • Kupata maumivu ya viungo yasioisha
    • Kuugua pumu
    • Upungufu wa virutubisho kwenye mwili
    • Magonjwa ya Ngozi
    • Magonjwa yanayotokana na mpambano kati ya kinga ya mwili na tishu za mwili (autoimmune diseases)
    • Matatizo ya kumbukumbu
    • Kukosa usingizi
    • Kuongezeka uzito
    • Kupata kizunguzungu
    • Matatizo ya figo na bandama

    Hatua 6 Za Kutibu Aleji Ya Chakula Na Kupunguza Madhara Yake

    Kutokana na kwamba aleji ya chakula inaweza kuleta madhara makubwa ya kiafya Napendekeza wewe na watu wote wanaokuzunguka wenye tatizo hili kufutilia kwa makini na kufanya kwa vitendo hatua hizi hapa chini

    Epuka kutumia hivi vyote ­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­

    Chakula na lishe ifuatayo inaongeza mpambano ndani ya mwli, kuzorotesha kinga ya mwili na kisha kuleta matatizo kwenye umeng’enyaji wa chakula.

    Vyakula vyote vilivyosindikwa na kuhifadhiwa kwenye vifungashio visiharibike:

    Vyakula vilivyosindikwa vimeongezwa kemikali, rangi na ladha vitu ambavyo vinaweza kusababisha aleji na mwili kushindwa kuvimeng’enya. Kwahivo ni muhimu sana kwa mtu mwenye aleji kuwa makini na uchaguzi wa vyakula na vinywaji vya kutumia ili kupunguza athari ya tatizo.

    Sukari

    Sukari husababisha ukuaji wa bateria wabaya kwenye mfumo wa chakula, na hivo kuzorotesha kinga yako ya mwili. Kinga inapokuwa chini huongeza hatari ya mwili kushindwa kuchakata baadhi ya vyakula, na kisha kuleta aleji ya vyakula.

    Vyakula vya ngano

    Utafiti unaonesha kwamba watu wengi wenye matatizo kwenye mfumo wa chakula na matatizo ya aleji hupata nafuu kubwa na afya zao kuimarika pale wanapoacha kutumia vyakula vya ngano. Tafiiti pia zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya watu wazima wamelalamika kuhusu kuongezeka kwa dalili mbaya za mzio/laji pale wanapotumia vyakula vya ngano.

    Usitumie vyakula vinavyoleta mzio/aleji kama

    Maziwa ya ng’ombe: Aleji kutokana  na maziwa ya ng’ombe ni tatizo kubwa sana kwa watoto wadogo. Kwa watu wazima ni mara chache sana wengi wao ni tatizo la mwili kushindwa kumen’genya viini lishe vilivyopo kwenye maziwa (lactogen intolerance).

    Mayai:  Mayai huleta mzio/aleji kutokana na uwepo wa kiini lishe kinachoitwa ovomucoid.

    Mazao na vyakula vyote vya  soy, karanga na samaki

    Tumia kwa wingi vyakula hivi ambavyo havileti mpambano (allergic reaction)

    Katika safari yako ya kupambana na aleji, fahamu kwamba kuna baadhi ya vyakula ambavyo havileti mpambano kati ya tishu za mwili na kinga ya mwili. Vyakula hivi ni kama

    Mbogamboga za kijani: Mboga hizi ni kama spinach ambazo zinakuwa na vitamin, madini, viondoa sumu, na viambata ambavyo husaidia umeng’enyaji wa chakua  kwa wingi sana. Hakikisha unaongeza mbogamboga za kijani kwenye mlo wako zitasaidia kuimarisha kinga na kutoa sumu mwilini.

    Maziwa ya nazi na nazi: Mbadala mzuri wa maziwa ya ng’ombe ni kutumia maziwa ya nazi. Maziwa haya kwa lugha rahisi ni tui la nazi. Hivo unaweza kutengeneza nyumbani kwako na ukaongeza viungo kama limau na tangawizi ukafurahia kinywaji chako.

    Mbegu: Mbegu kama za maboga na mbegu za alizeti ni nzuri kwa mgonjwa wa aleji, huongeza madini ya zinc na mafuta ya Omega 3. Sawa na karanga, lakini uzuri wake ni kwamba hazisababishi mpambano (allergic reaction) ambayo huleta aleji au mzio.

    Maziwa ya mama:  Tafiti mbalimbali zimethibitisha kwamba kunyonyesha mtoto kwa miezi sita ya mwanzo bila kula kitu chochote na  kuendelea kunyonyesha kwa miaka miwili husaidia kupunguza hatari ya mtoto kupata pumu, matatizo ya ngozi na aleji mbalimbali. 

    Tiba ya aleji ya chakula kupitia Vidonge asili Vya kihindi

    Kupitia hizi daw aza kihindi zitakusaidia kupona kesi yako kwa asilimia kubwa ndani ya miezi milili. Shuhuda ni ni nyingi kwa wagonjwa ambao tayari wametumia dawa. Tandikie sasa nawe uanze tiba na uondoke kwenye mateso ya aleji.

    Dawa ni sh 95,000/= Tuandikie kwa namba 0678626254 uanze tiba haraka