Tag: dawa asili ya stroke

  • Tiba asili ya Stroke, dozi ya Mwezi mmoja

    stroke

     Stroke au kiharusi ni mshutuko wa mwili na kuparalize mwili pale mishipa inayosambaza damu  kwenye ubongo inapopatwa na mshtuko na misukosuko kiasi cha kushindwa kupeleka damu kwenye ubongo. Hali inayoathiri ufanyaji kazi wa ubongo kwa zaidi ya masaa 24.

    Kulingana na shirika la afya duniani kiharusi ni nakisi katika neva ambayo hutokana na tatizo katika mishipa ya damu ya ubongo. Tatizo ambalo huendelea zaidi ya masaa 24 au kukoma ndani ya masaa 24.

    Kiharusi au stroke hutokea bila kutoa kiashiria chochote. Na ndio maana kuchukua tahadhari za kuepuka kutokea kwa tatizo ni muhimu zaidi. Kwasababu endapo utapata kiharusi na kwa bahati njema mwili ukaendelea kufanya kazi basi matokeo na madhara yake yatakusumbua sana maisha yote.

    Kuepuka madhara makubwa ya kiharusi mgonjwa anahitajika kutibiwa ndani ya saa moja baada ya kupata shambulizi. Hakikisha pia unafika haraka hospitali kama ukigundua moja ya dalili zifuatazo zimekutokea bila kutaraji.

    Dalili za mgonjwa wa Stroke

    • Kushindwa ghafla kutembea na kupoteza balansi ya mwili.
    • Kuchanganyikiwa ghafla na kushindwa kufanya utambuzi
    • Kukosa nguvu ghafla kwa upande mmoja wa mwili
    • Kushindwa kuoa vozuri na kizunguzungu
    • Mgonjwa anaweza kuwa na dalili za kuhisi mabadiliko ya harufu, ladha, kusikia na kuona; kulegea kwa misuli ya macho (aptosis)
    • kupungua kwa ufahamu na kulegea kwa misuli ya uso; Ulegevu wa Ulimi (kushindwa kutoa nje au kusogeza upande upande)
    • kupungua uwezo wa kumeza; ulegevu wa misuli ya shingo na kushindwa kugeuza shingo upande mmoja;
    • Kujihisi kizunguzungu na pia kutapika.
    • Kupata maumivu makali sana ya kichwa kwa haraka.

    Aina za stroke

    Stroke imegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na jinsi kinavyotokea

    Mgawanyo Wa Kiharusi  Kutokana Na (Visababishi Vyake).

    1.Stroke ya kukosa hewa kwenye Ubongo (Ischemic stroke)

    Aina hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo hupungua na kupelekea tishu za ubongo za eneo liliathirika kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

    Aina hii ya stroke husababishwa na damu iliyoganda kuziba mishipa midogo ndani ya ubongo (cerebral thrombosis). Au kipande cha damu kumeguka na kwenda kuziba mshipa wa damu kwenye ubongo(cerebral embolism)  na kupungua kwa usambazaji wa damu kwa ujumla.

    Stroke ya kuvuja damu ndani ya Ubongo (Hemorrhagic Stroke)

    Aina hii ya kiharusi hutokea pale ambapo mishipa midogo ya damu ndani ya ubongo hupasuka na kusababisha kusambaa kwa damu kwenye ubongo. Mara nyingi aina hii ya kiharusi hutanguliwa na dalili za kichwa kuuma, au kuwepo kwa historia ya ajali ya kichwa.

    Vipimo Kugundua tatizo la Kiharusi yaani Stroke

    Vipimo Mionzi CT-scan na MRI. Vipimo vingine ni; ECG ambacho huwezesha kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia). Na kama kuna damu iliyoganda kwenye moyo ambayo inaweza kufika kwenye ubongo.

    Holter monitor husaidia kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia) zinazotokea kwa vipindi. Angiogram huwezesha kugundua matatizo kwenye mishipa ya damu, na ni mishipa ipi ya damu iliyoziba. Vipimo vya damu huwezesha kutambua uwepo wa lijamu mwilini (hypercholesterolemia) na mabadiliko mengine katika damu

    Tabia zinazokuweka kwenye mazingira ya kupata stroke

    • Kutofanya mazoezi ya viungo
    • matumizi ya pombe mda mrefu
    • Ulaji wa vyakula vya wanga na sukari kupindukia

    Vyakula gani ule Zaidi kupunguza hatari ya stroke?

    Tafiti zinaonesha kwamba ulaji wa vyakula vya mafuta kama parachichi, nyama, samaki, nazi, mafuta ya olive, mafuta ya mawese, karanga na jamii zake , mboga za majani, matunda vinasaidia sana kuepukana na cholesterol mbaya.

    Matibabu ya stroke hospital

    1. Matibabu ya kiharusi kinachotokana na ubongo kukosa hewa (Ischemic stroke) Mgonjwa hutibiwa kwa kutumia dawa za kuyeyusha damu iliyoganda (thrombolytics) au kwa kuondoa damu iliyoganda kwa njia mbalimbali (thrombectomy). Dawa nyingine kama vile junior Aspirin na Clopidogrel hutolewa kwa ajili ya kuzuia chembe sahani kukusanyika na kuganda.
    2. Matibabu ya kiharusi kinachotokana na damu kuvujia kwenye ubongo (Hemorrhagic stroke) Aina hii ya kiharusi huitaji tathmini ya upasuaji wa neva ili kuchunguza na kutibu sababu ya damu kuvuja. Angalizo: kumpa mgonjwa wa aina hii ya kiharusi dawa za kuyeyusha damu iliyoganda au za kuzuia kuganda maana inhatarisha maisha ya mgonjwa badala ya kumsaidia. Kwahiyo ni vizuri kwa wataalamu kufanya ufanya uchunguzi wa kutosha ili kuwa na uhakika na tatizo.

    Tumia na Tiba zetu asili ili mgonjwa apone mapema

    Mgonjwa wa stroke kupona kwa dawa za hospital pekee ni ngumu sana, ndiomaana tumeleta tiba hizi asili zikusaidia kupone. Wakati unatumia dawa za hospital, na kuhudhuria mazoezi basi tumia na hizi dawa zetu asili utawahi kupona stroke.

    Tiba ni Tsh 135,000/= dozi ya mwezi mmoja, tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze dozi