Tag: hedhi kuvurugika

  • Kukoma hedhi, ukavu ukeni, kukosa hamu ya tendo na tiba asili

    kukoma hedhi

    Kukoma hedhi au kwa kitaalamu menopause ni hali ya kawaida inayomtokea kila mwanamke. inatokea pale kupata hedhi kunapofikia kikomo na hivo uwezo wa kupata mimba au ujauzito kushuka na kukoma kabisa. Hatua hii hutokea pale mwanamke anapofikisha umri wa miaka 50 na kuendelea.

    Kwa wanawake wengine hali hii hutokea pia kabla ya hapo kuanzia miaka 40. Na inaweza kutokea kutokana na ushauri wa madactari ama kufanyiwa upasuaji mdogo. Mfano mifuko ya mayai(ovaries) na mfuko wa mimba (uterus) inapoondolewa  kutokana na athari ya magonjwa mbalimbali kama saratani.

    Pale mwanamke anapofikia umri wa kukoma hedhi basi huanza kuona dalili zifuatazo

    • Mifupa kuwa dhaifu sana
    • Joto kupanda mara kwa mara na kupata jasho jingi
    • Ukavu kwenye uke na uke kuwa mdogo kama wa mtoto
    • Kubadilika badilika kwa mpangilio wa hedhi
    • Kuongezeka uzito sana
    • Msongo wa mawazo na kubadilika kwa mood yako.

    Nini ufanye kuondoia dalili mbaya za kukoma hedhi?

    Kuna njia za mda mrefu na njia za mda mfupi kutibu madhara ya kukoma hedhi. Njia nzuri na kuepusha madhara yanayotokana na  kukoma hedhi ni kuerekebisha lishe yako na kufanya mazoezi ya viungo. Kwa kuzingatia lishe waliyokula mababu zetu hapo zamani basi utapunguza madhara ya kukoma hedhi kama kuongezeka uzito na kutokwa na jasho jingi hasa kipindi cha usiku.

    Tambua kwamba kukoma hedhi siyo ugonjwa

    Kama tulivoona hapo juu pale mwili wa mwanamke unapokoma kutengeneza homoni za estrogen na progesterone ndipo hedhi yako itakoma. Wanasayansi huenda mbali zaidi na kuwaanzishia wahanga wa tatizo hili program ya kurudisha homoni hizi kwa kuwawekea homoni zilizotengenezwa maabara.

    Kitendo hiki hufahamika zaidi kama hormone replacement therapy. Njia hii inatazama ishu ya kukoma hedhi kama ugonjwa wakati ni suala la kawaida kabisa linalomkuta kila mwanamke. Ukweli ni kwamba kitu chochote kilichotengenezwa kwa mkono wa binadamu hakitafanya kazi sawa na kitu kilitengenezwa halisi kwa ajili ya kazi fulani kwenye mwili. Ndio maana madhara ya kuwekewa homoni hizi ni makubwa zaidi.

    Njia asili za kutumia ili upunguze dalili mbaya zinazotokana na kukoma hedhi.

    1. Tumia virutubisho/supliments kama virutubisho vya mafuta ya samaki(fish oil) yenye Omega 3 , vyenye ubora wa hali ya juu, kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika.
    2. Zinc supliments: Kwa wanawake, Madini ya Zinc yanahusika katika ukuuaji wa yai (oocyte). Kama mwanamke atakuwa na upungufu wa zinc, yai halitakomaa vizuri na utolewaji wa yai (ovulation) utazuiliwa , na kusababisha ugumba. Kiwango cha zinc cha kutosha kunamwezesha mwanamke kutumia estrogen na progesterone vizuri.
    3. Ovary Nutrition: Vidonge hivi vilivyotengenezwa kiasili kwa kutumia viambata vya mimea ya Glycine, Radiz Paeoniae Alba Eztractum na Ganoderma husaidia: kuongeza ufanyaji kazi wa mfuko wa mayai (ovaries), kuzuia Saratani ya matiti na kuimarisha afya ya mifupa kwa wanawake waliokoma hedhi.(menopause).
    kukoma hedhi

    Ushauri mwingine muhimu sana

    1. Hakikisha mlo wako unakuwa na kiasi sawa cha vyakula vya mafuta yale mazuri, kwa wingi ikifuatiwa na protini na kisha matumizi ya wanga na sukari kwa kiasi kidogo sana
    2. Epuka matumizi ya vyakula na vinywaji vilivyosindikwa maana huongeza kiasi cha homoni ya estrogen.
    3. Hakikisha unakuwa na ratiba nzuri ya kufanya mazoeziili kurekebisha kiwango cha insulin na hivo kusaidia kubalansi kiwango cha estrogen.
    4. Pata vitamin D ya kutosha, miili yetu ina uwezo wakutengeneza vitamin D kutoka kwenye mwanga wa jua, hivo hakikisha kila siku unapata mwanga wa jua walau nusu saa mpaka saa 1 ili kuuwezesha mwili kutengeneza Vitamin D ya kutosha. Tafiti zinaonesha kuwa Vitamin D husaidia kupunguza athari za zinazotokana na kukoma hedhi kama kutokwa na jasho jingi usiku bila kumeza vidonge.
    5. Kupunguza uzito husaidia kurekebisha na kupunguza athari za menopause kama kubadilika kwa joto la mwili: Tafiti zinasema kwamba wanawake wanaopunguza uzito ama walio kwenye program za kupunguza uzito wana uafadhali katibu 33% zaidi ya kupunguza athari za menopause kuliko wanawake wengine.

    Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 upate dawa kwa tsh 90,000/= tu ili kutibu maudhi ya kukoma hedhi kama, ukavu ukeni, kuongeza uteute ukeni, hamu ya tendo,kurejesha ubora wa mashavu ya uke.

  • Kukosa hedhi mda mrefu,Homoni kuvurugika na Tiba ya wiki 4 tu

    kukosa hedhi mda mrefu

    Kukosa hedhi mda mrefu na kuvurugika kwa mpangilio wa hedhi inawapata wanawake wengi sana kwa sasa hasa kutokana na mitindo ya maisha inayopelekea kuvurugika kwa homoni za kike. Homoni ndio zinaweka sawa hedhi yako hivo ni muhimu kurekebisha mtindo wa maisha unaovuruga homoni zako na kukupelekea kuvurugika kwa hedhi.

    Homoni Kuvurugika ni Chanzo cha Kukosa Hedhi mda mrefu

    Ukiwa unakosa hedhi, hedhi isiyo na mpangilio mzuri, maumivu makali wakati wa hedhi na hedhi kuchukua siku nyingi zaidi ya 7 ni kiashiria kwamba homoni zako zimevurugika. Kama una uhakika kwamba huna ujauzito na unakosa hedhi basi siyo kitu cha kuchukulia poa, nahitaji kutupigia uanze tiba haraka.

    Jinsi Mzunguko wa Hedhi Unavofanya Kazi

    Kikawaida kila mwezi mwanamke hutoa yai moja ili lirutubishwe kutengeneza kichanga. Pale yai lisipotolewa kwenye kikonyo chake tunaita anovulation. Moja ya dalili kwamba mayai yako yanapevuka lakini hayatolewi ni kukosa kabisa au kuvurugika kwa hedhi.

    Kwa wanawake wasio na mimba na wenye umri wa kuzaa kuanzia miaka 15 mpaka 40 na hawapati hedhi, hiki ndio sababu kubwa ya kushindwa kushika mimba.

    Sababu zingine za Kukosa hedhi mda mrefu na Kuvurugika kwa Mpangilio wa Hedhi.

    Ukiachilia mbali ujauzito na kukoma hedhi ambavyo vyote hivi ni vipindi vya kawaida kwa mwanamke kukosa hedhi. Zifuatazo ni sababu ambazo hupelekea mwanamke kukosa hedhi

    1.Msongo wa Mawazo

    Kikawaida mwili unapokutana na kitu cha kuogofya ama kinacholeta msongo wa mawazo unatunza nishati kubwa ili kuzielekeza kupambana na changamoto iliyopo mbele yako. Kwa hivo kila mara unapokuwa na msongo wa mawazo utendaji wa shuguli zingine za mwili unapungua na kudhoofika ikiwemo upevushaji wa mayai.

    2.Lishe Mbaya

    Lishe mbaya yenye upungufu wa virutubisho ikiwemo vitamini na madini na yenye sukari na viambata vya kuongeza ladha kwa wingi hupelekea tezi za Adrenal na Thayroid kufaya kazi kupita kiasi. Kitendo hichi hupelekea uzalishaji wa kichocheo cha cortisol ambacho kinapunguza uzalishaji wa homoni za uzazi.

    3.Uzito Mdogo sana ni chanzo cha kukosa hedhi mda mrefu

    Ili kupima uzito wako kama uko sawa kiafya, tunatumia kipimo cha BMI yaani body mass index ni kipimo kinachotumika kupima uwiano wa uzito na urefu wako. BMI= Uzito wako kwa kg gawanya kwa (urefu kwa mita x 2). BMI kuanzia 18.5 mpaka 25 inaonesha kwamba uzito wako ni mzuri. Ukipata zaidi ya 25 manake uzito wako ni mkubwa na ukipata chini ya 18.5 ni kwamba una uzito mdogo kupita kiasi.

    Mafuta mwilini huchochea uzalishaji wa homoni ya estrogen kwa wanawake na ndio maana wanawake wembamba sana hukosa hedhi maranyingi zaidi. Kufanya mazoezi makali hupelekea mahitaji ya virutubisho mwilini kuongezeka na hivo uzito kupungua kupita kiasi na kuvurugika kwa homoni.

    4.Kufanya Mazoezi Kupita Kiasi inapelekea kukosa hedhi mda mrefu

    Mazoezi ni muhimu kwa mwili katika kurekebisha athari za msongo wa mawazo, kuweka sawa shinikizo la damu, usingizi mzuri na kuweka sawa uzito wamo. Ila kumbuka kufanya mazoezi kupita kiasi kunachosha sana mwili kupelekea ukose hedhi mda mrefu.

    5.Matatizo Kwenye Tezi ya Thairodi (tezi ya shingoni)

    Tezi ya thairodi ni kiungo chenye umbo la kipepeo. Kiungo hichi kipo kwenye shingo chini ya koromeo la sauti. kazi kuu ya Tezi hii ni kuzalisha homoni za (T3) na (T4), ambazo kwa pamoja hufanya kazi ya kurekebisha mzunguko wa damu na kazi mbalimbali za mwili na pia kuweka sawa hedhi yako.

    Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango

    dawa za uzazi wa mpango

    wanawake wengi hukosa hedhi kwa muda mrefu baada ya kuacha kutumia vidonge na sindano za uzazi wa mpango. Japo wahudumu watakwambia kwamba hali itakaa sawa baada ya kuacha kumeza vidonge lakini bado hali huwa mbaya kwa wanawake wengine kwani tayari vidonge vimevuruga vichocheo. Kama upo kundi hili tupigie uanze tiba mapema

    7.Ugonjwa wa PCOS yaani vimbe kwenye mayai

    Ni mkusanyiko wa dalili mbalimbali kama uzito mkubwa na kitambi, kupanda kwa sukari kwenye damu, kuwa na chunusi nyingi, kuota ndevu na hedhi kuvurugika ndizo tunaziita syndrome au Polycystic Ovarian syndrome. Wanawake wenye PCOS hukosa hedhi kutokana na kuvurugika kwa homoni zao.

    8.Alegi ya Vyakula

    Mwili kushindwa kuchakata baadhi ya vyakula kama vyakula vya ngano na maziwa ama kuwa na aleji na vyakula baadhi husababisha mwili kukosa virutubisho muhimu  na hivo kuzalisha magonjwa sugu.

    Tiba asili ya kukosa hedhi mda mrefu

    Tumefanya utafiti na kuleta hizi dawa za kihindi zilizotengenezwa kwa mimea. Dawa utameza kwa muda wa wiki 4 tu na baada ya hapo unakuwa umepona hedhi yako na kufurahia tena Maisha.

    Dozi ya sh 75,000/= tu kwa mwezi mmoja. Tuandikie kwa namba zetu 06786262654 uanze tiba

  • Homoni kuvurugika na Vimbe kwenye mayai

    homoni kuvurugika

    Homoni kuvurugika ni suala pana linalojumuisha vyanzo vingi, kama mtindo wa maisha, umri kwenda, sababu za kimazingira kama msongo wa mawazo. Sababu zote hizi zinaathiri uzalishaji na ufanyaji kazi wa vichocheo ama homoni zako.

    Mambo Yanayoashiria Kwamba Una Shida ya Homoni kuvurugika

    • Kuwa na hedhi ya muda mrefu Zaidi ya siku 7 unatumia Zaidi ya pedi 2
    • Kuwa na hedhi yenye kuambatana na maumivu Makali sana
    • Kuwa na hedhi yenye kuambatana na kichefu chefu,kuharisha
    • Hedhi kuvurugika,kuingia mara tatu kwa mwezi mmoja, mara mbili au kukosa hedhi miezi 3 mpaka 6
    • Kuota ndevu sehemu za usoni,kifuani nyingi kupita kiasi
    • uzito mkubwa na kitambi cha tumbo la chini
    • Ugumba na Kukosa mtoto kwa muda mrefu
    • Kukosa hamu ya tendo la ndoa ama  lenye kuambatana na maumivu makali

    Wanawake wengi wana shida ya homoni kuvurugika

    Nimekuwa nikitafutwa na wakina mama wengi sana na wamekuwa wakinisimulia jinsi gani wamesumbuka na kutatua tatizo hilo, na kupitia tiba zetu wamepona kabisa na wanafurahia Maisha. Wanawake wengi wanaonitafuta ni wale ambao

    1. Tatizo linaanza kwahivyo wanatafuta njia nyepesi za kuondoa tatizo kabla hawajafikia zile njia ngumu za hospitali za kuliondoa tatizo.
    2. Wale watu ambao wametumia kila mbinu za kutatua matatizo kwa kuanzia ngazi za juu lakini hawapata suluhisho. Hawa huwa wamesumbuka kwa wataalamu mbalimbali lakini hawajakata tamaa.
    3. Wale watu waliotumia njia zote bila mafanikio na hadi wameambiwa na madaktari wao hapo hutaweza kufikia malengo. Wanawake hawa ni watu ambao wanaishi katika msongo wa mawazo mkubwa sana.

    Nini kinapelekea homoni kuvurugika na vimbe kwenye mayai

    Mwanamke huwa ana viwanda viwili vya kuzalisha mayai kila mwezi yaani kwa lugha nyingine ni ovari ya kushoto na ovari ya kulia. Ndani ya ovary ya mwanamke kuna mayai ambayo hayajakomaa kwa lugha ya kilatini huitwa Follice cells ,hizi ndizo hukomazwa kila mwezi na kutupatia yai ambalo linatakiwa lipatiwe urutibishaji endapo itakutana na mbegu ya kiume.

    Sasa inapotokea kifuko cha yai kimekomaa vizuri kwenye ovary na linatakiwa zipasuke zitoe mayai na ikatokea halijapasuka hivyo hizo follicles ambazo zimeshindwa kupasuka na kutoa yai zinabaki na umbo kama zabibu zilizo kwenye kikonyo chake mwonekano wake kwa kitaalamu zinafananishwa na kitu kiitwacho cyst kwa sababu zipo nyingi tunatumia neno la kitalamu polycystic.

    Kuongezeka homoni za kiume inapelekea vimbe kwenye mayai

    Kuongezeka kwa homoni za kiume zinajulikana kama  Androgens ambazo ni Testosterone inachaangi kupara vimbe kwenye mayai .Kwa kawaida mwanamke huwa ana kiwango kidogo sana cha homoni hii ya kiume Testosterone.  Homoni inayomfanya mwanaume aonekane mwanaume kuongezeka kwa homoni hii inampelekea mwanamke kuonesha dalili za kuongezeka kwa dalili za kiume kwa mwanamke kama kuota ndevu kidevuni,chunusi sugu na pia kuongezeka uzito kupita kiasi na kitambi pia.

    Nini Madhara ya Kuvurugika Kwa Homoni Hizi Kwa Mwili Wa Mwanamke

    Endapo homoni zako zitavuruguka basi unapata madhara yafyatayo

    • kukosa mimba na ugumba
    • kukosa hamu ya tendo na ukavu ukeni
    • hedhi yako kuvurugika na kushindwa kutambua siku za hatari
    • kuongezeka uzito na kitambi
    • kuugua magonjwa ya uzazi mara kwa mara

    Tiba asili kutoka kwetu kutibu vimbe kwenye mayai na kurekebisha homoni

    Endapo wewe ni mwanamke upo kwenye hili kundi na unataka kutoka kwenye haya mateso, basi tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze tiba mapema. Ni dozi ya mwezi mmoja tu kurekebisha homoni na kupona vimbe kwenye mayai. Tiba hizi asili kutoka india zimeleta shuhuda nyingi sana.