
Kukosa hedhi mda mrefu na kuvurugika kwa mpangilio wa hedhi inawapata wanawake wengi sana kwa sasa hasa kutokana na mitindo ya maisha inayopelekea kuvurugika kwa homoni za kike. Homoni ndio zinaweka sawa hedhi yako hivo ni muhimu kurekebisha mtindo wa maisha unaovuruga homoni zako na kukupelekea kuvurugika kwa hedhi.
Homoni Kuvurugika ni Chanzo cha Kukosa Hedhi mda mrefu
Ukiwa unakosa hedhi, hedhi isiyo na mpangilio mzuri, maumivu makali wakati wa hedhi na hedhi kuchukua siku nyingi zaidi ya 7 ni kiashiria kwamba homoni zako zimevurugika. Kama una uhakika kwamba huna ujauzito na unakosa hedhi basi siyo kitu cha kuchukulia poa, nahitaji kutupigia uanze tiba haraka.
Jinsi Mzunguko wa Hedhi Unavofanya Kazi
Kikawaida kila mwezi mwanamke hutoa yai moja ili lirutubishwe kutengeneza kichanga. Pale yai lisipotolewa kwenye kikonyo chake tunaita anovulation. Moja ya dalili kwamba mayai yako yanapevuka lakini hayatolewi ni kukosa kabisa au kuvurugika kwa hedhi.
Kwa wanawake wasio na mimba na wenye umri wa kuzaa kuanzia miaka 15 mpaka 40 na hawapati hedhi, hiki ndio sababu kubwa ya kushindwa kushika mimba.
Sababu zingine za Kukosa hedhi mda mrefu na Kuvurugika kwa Mpangilio wa Hedhi.
Ukiachilia mbali ujauzito na kukoma hedhi ambavyo vyote hivi ni vipindi vya kawaida kwa mwanamke kukosa hedhi. Zifuatazo ni sababu ambazo hupelekea mwanamke kukosa hedhi
1.Msongo wa Mawazo
Kikawaida mwili unapokutana na kitu cha kuogofya ama kinacholeta msongo wa mawazo unatunza nishati kubwa ili kuzielekeza kupambana na changamoto iliyopo mbele yako. Kwa hivo kila mara unapokuwa na msongo wa mawazo utendaji wa shuguli zingine za mwili unapungua na kudhoofika ikiwemo upevushaji wa mayai.
2.Lishe Mbaya
Lishe mbaya yenye upungufu wa virutubisho ikiwemo vitamini na madini na yenye sukari na viambata vya kuongeza ladha kwa wingi hupelekea tezi za Adrenal na Thayroid kufaya kazi kupita kiasi. Kitendo hichi hupelekea uzalishaji wa kichocheo cha cortisol ambacho kinapunguza uzalishaji wa homoni za uzazi.
3.Uzito Mdogo sana ni chanzo cha kukosa hedhi mda mrefu
Ili kupima uzito wako kama uko sawa kiafya, tunatumia kipimo cha BMI yaani body mass index ni kipimo kinachotumika kupima uwiano wa uzito na urefu wako. BMI= Uzito wako kwa kg gawanya kwa (urefu kwa mita x 2). BMI kuanzia 18.5 mpaka 25 inaonesha kwamba uzito wako ni mzuri. Ukipata zaidi ya 25 manake uzito wako ni mkubwa na ukipata chini ya 18.5 ni kwamba una uzito mdogo kupita kiasi.
Mafuta mwilini huchochea uzalishaji wa homoni ya estrogen kwa wanawake na ndio maana wanawake wembamba sana hukosa hedhi maranyingi zaidi. Kufanya mazoezi makali hupelekea mahitaji ya virutubisho mwilini kuongezeka na hivo uzito kupungua kupita kiasi na kuvurugika kwa homoni.
4.Kufanya Mazoezi Kupita Kiasi inapelekea kukosa hedhi mda mrefu
Mazoezi ni muhimu kwa mwili katika kurekebisha athari za msongo wa mawazo, kuweka sawa shinikizo la damu, usingizi mzuri na kuweka sawa uzito wamo. Ila kumbuka kufanya mazoezi kupita kiasi kunachosha sana mwili kupelekea ukose hedhi mda mrefu.
5.Matatizo Kwenye Tezi ya Thairodi (tezi ya shingoni)
Tezi ya thairodi ni kiungo chenye umbo la kipepeo. Kiungo hichi kipo kwenye shingo chini ya koromeo la sauti. kazi kuu ya Tezi hii ni kuzalisha homoni za (T3) na (T4), ambazo kwa pamoja hufanya kazi ya kurekebisha mzunguko wa damu na kazi mbalimbali za mwili na pia kuweka sawa hedhi yako.
Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango

wanawake wengi hukosa hedhi kwa muda mrefu baada ya kuacha kutumia vidonge na sindano za uzazi wa mpango. Japo wahudumu watakwambia kwamba hali itakaa sawa baada ya kuacha kumeza vidonge lakini bado hali huwa mbaya kwa wanawake wengine kwani tayari vidonge vimevuruga vichocheo. Kama upo kundi hili tupigie uanze tiba mapema
7.Ugonjwa wa PCOS yaani vimbe kwenye mayai
Ni mkusanyiko wa dalili mbalimbali kama uzito mkubwa na kitambi, kupanda kwa sukari kwenye damu, kuwa na chunusi nyingi, kuota ndevu na hedhi kuvurugika ndizo tunaziita syndrome au Polycystic Ovarian syndrome. Wanawake wenye PCOS hukosa hedhi kutokana na kuvurugika kwa homoni zao.
8.Alegi ya Vyakula
Mwili kushindwa kuchakata baadhi ya vyakula kama vyakula vya ngano na maziwa ama kuwa na aleji na vyakula baadhi husababisha mwili kukosa virutubisho muhimu na hivo kuzalisha magonjwa sugu.
Tiba asili ya kukosa hedhi mda mrefu
Tumefanya utafiti na kuleta hizi dawa za kihindi zilizotengenezwa kwa mimea. Dawa utameza kwa muda wa wiki 4 tu na baada ya hapo unakuwa umepona hedhi yako na kufurahia tena Maisha.
