Tag: Kushika mimba

dawa asili za kushika mimba haraka na kupevusha mayai

  • Kuziba mirija ya uzazi na Tiba asili kusafisha mirija bila upasuaji

    kuziba mirija ya uzazi

    kuziba mirija ya uzazi au kujaa maji kwa mirija (fallopian tubes) ni hali ya kuwepo kwa majimaji katika mirija yako . Kuziba kwa mirija kunazuia yai kusafiri kutoka kwenye mifuko ya mayai yaani ovari mpaka kwenye mfuko wa mimba

    Nini chanzo cha kuziba mirija ya uzazi ?

    Kwa kiasi kikubwa wataalamu wanasema tatizo hili linatokea endapo mgonjwa aliwahi kuugua magonjwa yoyote  katika njia ya uzazi au magonjwa ya ngono. Vyanzo vingine ni kutoa mimba na kutosafishwa vizuri, na uvimbe kwenye kizazi kutokana na kukua kwa tishu laini za mfuko wa mimba.

    Pia kama mgonjwa aliwahi kufanyiwa upasuaji kwenye kizazi kwa kipindi cha nyuma. Upasuaji ukapeleka majeraha kwenye mirija ya uzazi basi hupelekea kupata tatizo hili la kuziba mirija. Endelea kusoma zaidi makala yetu kupata ufahamu wa tatizo hili ambalo linaweza kuzuia mwanamke kupata ujauzito na hatimaye ugumba.

    Jinsi gani kuziba mirija ya uzazi inavosababisha ugumba

    Tunafahamu kwamba ili mwanamke apate mimba basi ni lazima yai ambalo lipo tayari yaani limeshapevuka litoke kwenye ovari kisha lisafiri hadi kwenye  mirija ya uzazi ndipo lipate kurutubishwa na mbegu ya kiume.

    Ovari ndicho kiwanda cha mwanamke cha kutengeneza mayai. Kitendo hichi cha urutubishaji hutokea siku ya 14 kwenye mzunguko wa hedhi. Kwahivo kama mrija umeziba manake yai halitaweza kusafiri na urutubishaji hautafanyika hivo mimba haitaweza kutungwa.

    Je kama mrija mmoja umeziba na mwingine uko vizuri je kuna uwezekano wa kushika mimba?

    Kuna mrija miwli ya uzazi, mrija mmoja kutoka kwenye kila mfuko wa mayai(ovari). Hivo kila mwezi mfuko mmoja wa mayai hutoa yai moja ili liweze kurutubishwa na mbegu ya kiume. Na mara chache hutokea mifuko yote kutoa yai moja ndani ya mwezi mmoja.

    Hivo ni wazi kwamba kama mrija mmoja umeziba na mwingine upo vizuri basi yai litasafiri vizuri na urutubishaji utafanyika na  mimba itatungwa. Lakini athari zingine zaa mrija wa kwanza kuziba itaendelea kuwepo.

    Wanasayansi wamebaini kwamba kuziba kwa mrija mmoja kunaweza kusababisha kutiririsha maji kuelekea kwenye mfuko wa mimba na hivo kuathiri kiumbe kipya.

    Matibabu ya hospital kwa kuziba mirija ya uzazi.

    Kuna aina nyingi za matibabu yanayotolewa kwa kuziba kwa mrija ya uzazi katika mahospitali. Hizi ni baadhi ya njia hizo, na tumeandika ili tu upate ufaham. Mara nyingi matibabu haya ni ghali sana, ndiomaana tunashauri uchukue tiba zetu asili kwa bei nafuu.

    1.Kukata na kuondoa mrija ulioathorika

    Madaktari wanaweza kupendekeza kufanya upasuaji na hivo kuondoa mrija ulioziba ama kujaa maji. Kitaalamu tiba hii huitwa laparoscopic salpingectomy. Njia hii huweza kuhatarisha ufanyaji kazi wa ovari kwa kukosa damu kutokana na kwamba mrija wote hukatwa na kuondolewa kabisa.

    2.Kunyonya maji yaliyoziba mirija(sclerotherapy)

    Tiba hii hufanyika kwa ultrasound na yaweza kuwa tiba salama  zaidi kuliko kukata mrija wa uzazi. Katika tiba hii tube nyembamba huingizwa kwenye mrija ulioathirika na hivo kunyonya maji yaliyopo.

    3.Upasuaji mdogo kwenye mrija

    Upasuaji huu hulenga eneo husika kwenye mrija wa uzazi. Hivo eneo hili hupasuliwa na maji kusafishwa na kisha kushonwa tena ili kuzuia maji maji kuvia kwenye mfuko wa mimba ama uterus.

    Tumia tiba zetu Asili, ni Salama zaidi na bei Nafuu sana

    Kwa mwanamke mwenye changamoto ya mirija ya uzazi kujaa maji na kuziba, tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha kizazi. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 4 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama kuziba kwa mirija ya uzazi, fangasi na PID.

    Kwa dozi ya Tsh laki 1 tu unapona mirija yako . Tuandikie kwa namba 0678626254 uanze tiba.