Tag: Tiba ya choo kwa mtoto

  • Choo kigumu kwa Mtoto na Tiba asili

    choo kigumu kwa watoto

    Tukisema choo kigumu kwa mtoto maana yake haja kubwa inayopatikana isiyozidi mara tatu katika wiki au haja kubwa inayotoka kwa shida kutoka na utokaji wake kama mavi ya mbuzihata kama inapatikana kila siku. Hali hii ya choo inapokuwa sugu mtoto husika hupata choo si zaidi ya mara tatu katika kipindi cha mwezi mmoja. Ni moja ya tatizo katika mfumo wa kusaga chakula yanayowakumba watu wengi si hapa kwetu Tanzania au Afrika tu bali dunia nzima kwa jumla. Shida ya kupata choo ni hali inayowakabili watu mbalimbali.

    Nini kinapelekea choo kigumu kwa mtoto

    Kuna sababu nyingi zinazopelekea kutokea kwa tatizo la kukosa kupata haja kubwa . Baadhi ya hizo ni kama hizi zifuatazo

    • Madhara ya kutumia dawa fulani mda mrefu
    • Matumizi ya Maziwa ya ng’ombe au formula: Unywaji wa maziwa mengi ya ng’ombe kwa watoto wadogo au mabadiliko ya ghafla ya aina ya maziwa ya kopo yaani formula yanaweza kufanya choo kuwa kigumu. Maziwa ya formula ni yale ya makopo yanauzwa kwenye mafamasia
    • Kutokunywa Maji ya Kutosha: Upungufu wa maji mwilini huufanya utumbo mkubwa kufyonza maji yote kwenye mabaki ya chakula, jambo linalofanya kinyesi kuwa kikavu na kigumu.
    • Kutumia uji wa aina moja ya nafaka na mzito sana: Kumpa mtoto uji wa mahindi au mchele pekee bila kuchanganya na nafaka zisizokobolewa (kama dona) hupunguza nyuzinyuzi au fiber. Pia uji mzito sana bila maji ya kutosha huchelewesha mmeng’enyo

    Huduma ya kwanza ikiwa kuna shida ya choo kigumu kwa mtoto

    1. Jaribu kumpa mtoto wako maji safi na salama kuanzia mililita 60 hadi 120 kwa siku. Punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa. Ni bora maji ya mtoto yachemshwe na kufunikwa vyema.
    2. Ongeza vyakula Vyenye Nyuzinyuzi yaani fiber: Mpe mtoto matunda kama papai, maparachichi, na maembe. Mboga za majani (kama mchicha na sukumawiki) na nafaka zisizokobolewa (kama ugali au uji wa dona, na ulezi) husaidia sana kulainisha choo. Lishe hii mpe mtoto ambaye kaanza kula tu. Mtoto mchanga usimpe chakula mpaka atimize miezi 6.
    3. Jiepushe kumpa mtoto wako vyakula vyenye wanga na sukari na vyakula vinavyotengenezwa kwa unga uliokobolewa.
    4. Mpake mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Tumia mafuta ya nazo au mafuta ya black seed
    5. hata baada ya kubadilisha aina ya chakula cha mtoto au linaambatana na dalili nyingine kama vile kutapika au mtoto kukosa utulivu na kuhangaika.
    6. Mkande mtoto tumbo lake wakati akiwa anaoga kwenye maji na njia hiyo husaidia kulegeza misuli ya mwili wa mtoto, na kumsaidia kupata choo wa urahisi.

    Tumia tiba zetu asili kutoka india mtoto apone haraka choo kigumu

    Dawa tumeanyia utafiti na inaleta matokeo mapema ndani ya siku 1. Dawa imetengenezwa kwa mimea asili na haina kemikali, kwahivo ni salama kutumika na mtoto. Dawa ipo mfumo wa maji, anatumia kijiko kimoja asbhi,mchana na jioni kulingana na umri wake.

    Tuandikie kwa namba zetu 0678626254