Tag: Tiba za Kusafisha tumbo

  • Tumbo kujaa Gesi, Kukosa choo Gesi na Tiba asili ndani ya wiki

    tumbo kujaa gesi

    Nini kinapelekea Tumbo kujaa Gesi

    Kutokakana na lishe mbovu tunayokula kila siku kwa kutegemea zaidi vyakula vya haraka na bei rahisi . Vyanzo vingine vya tatizo ni msongo wa mawazo, matumizi ya vidonge mara kwa mara na mazingira yenye sumu yanayotuzunguka kama moshi wa magari na kemikali za viwandani.

    Kumbuka tatizo la tumbo kujaa gesi inaweza kuwa ni kiashiria cha matatizo makubwa ya kiafya. Mfano fangasi kwenye mfumo wa chakula. Fangasi hawa husababisha upate alegi ya vyakula mbalimbali, magonjwa ya autoimmune na hata saratani ya tumbo.

    Dalili za Tumbo Kujaa Gesi

    Kuwa na gesi tumboni ni tofauti kabisa na kitambi. Kitambi kinaweza kuwa cha muda mrefu lakini tumbo la gesi ni la muda tu baadae husinyaa na kurudi katika hali ya kawaida kwani huletekezwa na hewa kukwama tumboni na kufanya tumbo kutanuka. Kwa watu wengine tumbo linaweza kuwa kubwa kama mjamzito.

    Kwa bahati nzuri ni kwamba tatizo la gesi tumboni linatibika endapo utafata ushauri wetu na kutumia hizi dawa za mimea kwa usahihi. Kwa kesi chache mfano kama tatizo linakutokea mara kwa mara basi kuna haja ya kupanga appointment ukaonana na dactari kwa vipimo. Dalili zingine zinazoambatana na tumbo kujaa gesi ni kama

    Nini Husababisha Tumbo Kujaa Gesi?

    Unaweza ukawa unajiuliza ni kitu gani hasa ambacho ni chanzo cha tumbo kujaa na kufutuka kana kwamba umeshiba sana. Kuna vitu vingi nyuma ya pazia vivoletekeza tumbo kujaa. Kuanzia kwenye aleji, kuvurugika kwa homoni, matatizo kwenye tezi ya thairodi, shida kwenye mfumo wa chakula, na mengine mengi.

    Inaweza kuwa ngumu kujua kinacholetekeza tumbo kujaa geni kwa upande wako lakini kadiri unavojifunza zaidi na kuusoma mwili wako basi utajua vitu gani vya kuepuka.Huwa nasema kila siku kwamba daktari wa kwanza wa mwili wako ni wewe mwenyewe. Ni muhimu kufatilia kwa ukaribu mabadiliko ya mwili wako.

    Sababu 8 Zinazoletekeza Tumbo Kujaa Gesi

    Matatizo kwenye Mmeng’enyo wa Chakula

    Magojwa kama Ulcerative colitis, celiac disease na IBS-inflammatory bowel syndrome huletekeza kujaa gesi kwa tumbo

    Maji kubakizwa mwilini inapelekea tumbo kujaa gesi

    Wakati fulani maji yanaweza kuabakizwa kwenye sehemu fulani za mwili kama kweye magoti, tumboni na kwenye nyonga. Maji haya huletekeza maumivu makali kwenye joints na tumboni. Uwepo wa maji tumboni hujulikana kama ascites na inaweza kuashiria kwamba una tatizo kwenye ini au maambukizi ya bacteria.

    Ndio maana kuna umuhimu wa kufanya vipimo kama una homa ya ini (hepatitis B). kama kuna shida ya ini basi utapata dalili zingine kama kichfuchefu, macho na ngozi kuwa njano, kupungua uzito, kutapikadamu na chakula kutosagwa tumboni.

    Mwili kukosa maji (Dehydration)

    Umewahi kufuatilia siku ukiwa umekunywa sana pombe ama kula zaidi vyakula vyenye chumvi kwa wingi na tumbo likajaa gesi?. Mwili unapokosa maji hufanya uchakataji na usagaji wa chakula kuwa mgumu. Mwili unapokosa maji ya kutosha hufanya kazi ya kuvuta na kuhifadhi maji mengi zaidi pale utakapokunywa maji ili kuepuka kutokea kwa upungufu huu. Maji yanapokuwa mengi kupita kiasi ndipo sasa unaweza kupata choo kigumu ama kukosa choo. Hakikisha unakunywa maji mara nyingi zaidi kila siku ili kuepuka tumbo kujaa gesi.

    Kukosa choo ama kupata choo kigmu/Constipaton

    Constipation inaweza kuwa sababu kubwa ya kwanini tumbo lijae gesi. Constipation inaweza kusababisha choo kigumu, maumivu tumboni na kukosa choo kwa muda mrefu. Kukosa choo na choo kigumu husabishwa na ulaji wa vyakula vilivyokobolewa sana visivyo na kambakamba, matumizi kidogo ya maji, msongo wa mawazo na kuishi bila kufanya mazoezi.

    Alegi ya Chakula inaweza pelekea tumbo kujaa gesi

    Aleji ya vyakula mbalimbali kama maziwa, mayai na ngano vinaweza kuwa ni sababu ya kujaa gesi kwa tumbo lako. Kuna aina nyingi ya vyakula inaweza kusababisha upate mzip ama alegi. Cha kufanya sikiliza mwili wako unasemaje pale unapokula chakula. Kama mwili unakataa aina fulani ya vyakula na unapata mcharuko kama kuvimba, kuharisha, ama kutapika basi usitumie chakula hicho.

    Maambukizi

    Kama mwili unapambana na maambukizi aidha ya bacteria, virusi, fangasi au vimelea wengine basi utapata tatizo la kujaa gesi tumboni kutokana na mpambano wa ugonjwa na seli nyeupe za damu.

    Majeraha Kwenye Mfumo wa Chakula

    Wakati mwingine unaweza kupata gesi tumboni kutokana na vidonda ama uvimbe kwenye baadhi ya sehemu za mfumo wa chakula kama utumbo mdogo na utumbo mpana. Uvimbe unaweza kuzuia utolewaji wa uchafu na kuletekeza gesi na maji kukwama.

    Mabadiliko ya Homoni

    PMS (pre menstrual syndrome) ikimaanisha mkusanyiko wa dalili zisizo za kawaida za kipindi cha hedhi ni chanzo cha tumbo kujaa gesi. Tatizo linaweza kuwa kubwa kama una uvimbe kwenye kizazi na hedhi yako inavurugika. Kwanini wanawake hupata gesi tumbo wakati au karibia na kipindi cha hedhi? Mwanamke anapokaribia hedhi kiwango cha homoni ya estrogen huongezeka na ukuta wa mfuko wa mimba kuongezeka. Pale anapopata siku zake basi damu na maji mengi hutolewa nje na hivo tumbo kurudi katika hali ya kawaida.

    Saratani

    Moja ya dalili za saratani ya utumbo mpana na saratani ya mfuko wa mimba ni tumbo kujaa gesi. Ndio maana ni muhimu kuongea na daktari wako pale ambapo umejaribu kila njia ya kundoa tatizo lako lakini bado halijaisha.

    Vyakula vya Kuepuka pale Unapotaka Kutibu Tatizo la Tumbo Kujaa Gesi

    • Vyakula vya sukari na snacks zilizooongezewa utamu
    • Nafaka na vyakula vya nafaka hasa ngano na Maharage huongeza uzalishaji wa gesi tumboni
    • Vinywaji vilivosindikwa kama soda (Carbonated drinks)

    Njia zingine za Kukusaidia Kuondokana na Tatizo la Tumbo Kujaa Gesi

    1. Tembelea hospitali mara kwa mara kuonana na daktari
      Kutokana na kwamba tumbo kujaa gesi inaweza kuletekezwa na matatizo mengine mengi ya kiafya kama tulivosoma pale juu kuna umuhimu kufanya vipimo mara kwa mara ili kujua chanzo cha tatizo lako. Kumbuka hakuna kipimo kimoja cha kujua kinachokusumbua ni vyema kuongea na dactari wako ili akupe ushauri na vipimo stahili.
    2. Weka ratiba ya kufanya mazoezi: Kufanya mazoezi itakusaidia kuimarisha ufanyaji kazi wa mfumo wa chakula, kurahisisha usafirishaji, na hivo kutoa sumu mwilini. Fanya mazoezi walau dakika 30 mpaka 60 kwa siku mara 3 kwa week.
    3. Kunywa maji ya kutosha: Maji hurahisisha usagaji wa chakula na utolewaji wa choo, Hakikisha unakunywa maji kila unapopata kiu. Hakuna kipimo maalumu cha kiwango cha maji unachotakiwa kutumia unaweza kuanza na glass 6 mpaka 8 itategemea na shughuli unazofanya na mazingira unayoishi.
    4. Punguza msongo wa mawazo

    Tiba Ya tumbo kujaa gesi Kupitia vidonge asili kutoka india

    Vidonge hivi asili vimekuwa yakitumika kwa muda mrefu huko india kwa ajili ya changamoto mbalimbali kama kiungulia, gesi tumboni , vidonda tumbo na kukosa choo.
    Hivi sasa vidonge hivi yameonekana kutibu magonjwa mengine zaidi kama bawasili, kuharisha na kuimarisha usagaji wa chakula tumboni.

    Dawa ni Tsh 85,000/= dozi ya wiki mbili. Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze dozi

  • Kiungulia,Ushauri na Tiba asili ya wiki mbili

    kiungulia

    Kiungulia ni Kitu Gani

    Kiungulia kwa kitaalamu tunaita heartburn ni hali ya kukera inayosababisha maumivu makali kwenye kifua na upande wa juu wat umbo. Hali hii inaendana kwa ukaribu wa kupanda kwa tindikali(acid reflux). Kuna tofauti kati ya acid reflux na heartburn, acid reflux ni kitendo cha kupanda kwa tindikali kutoka tumbo kurudi juu kwenye umio la chakula na kusababisha maumivu ya kifua ambayo sasa tunaita ni Heartburn. Kwahiyo acid reflux inaweza kusababisha heartburn.

    Dalili za Kuonesha Tayari una Kiungulia

    • Kupata hali ya kuunguza kwenye kifua karibu na moyo, hali inayotokea baada tu ya kula
    • Mdomo kuwa mchachu muda mwingi
    • Kupata usingizi kwa shida kutokana na maumivu
    • Mdomo kukauka sana
    • Meno kupoteza uimara na kuanza kumomonyoka kutokana na uwepo wa tindikali.
    • Mdomo kunuka kutokana na kurudi juu kwa chakula cha tumboni chenye tindikali
    • Tumbo kujaa na kujamba sana baada ya kula
    • Kukosa hamu ya chakula na kichefuchefu.

    Mazingira Yanaopelekea upate Kiungulia Pamoja na Visababishi vyake

    Vifuatavyo ni vyakula na mazingira yanayokusababishia uwe na kiungulia

    1. Lishe mbovu: wanaokula zaidi vyakula vilivyosindikwa, sukari, chocolate, cyakula vyenye caffeine kama kahawa wapo kweye hatari zaidi ya kupata kungulia.
    2. Upungufu wa madini kama Mgnesium na Potassium
    3. Ulaji wa mlo mkubwa badala ya kula kidogo kidogo kwa kuweka gape la muda hasa unapokarbia kulala
    4. Kuwa na alegi au mzio kwa vyakula baadhi
    5. Maisha ya kizembe, kwa kutumia muda mwingi ukiwa umekaa pasipo kushugulisha mwili wako
    6. Uzito mkubwa na kitambi
    7. Msongo wa mawazo kupita kiasi ni chanzo cha kiungulia
    8. Matumizi ya vidonge kwa muda mrefu, hasa antibiotics, ibuprofen na asprini
    9. Kufanya mazoezi kupita kiasi bila kupata muda wa kupumzika kitendo kinachoweka presha kubwa sana kwenye tumbo.

    Hatua 4 za Kupunguza Kiungulia wakati unajiandaa kuja kuchukua dawa

    1. Kula lishe nzuri ya uhakika na pia tupa mbali vyakula vinavyoongeza tatizo
      • Vyakula vilivyosindikwa na vyenye sukari kwa wingi+mafuta ya kupikia yalisosafishwa sana kiwandani siyo salama kwako
      • Pombe na vyakula vyenye caffeine kwa wingi kama kahawa, wanga kupita kiasi, Vinywaji vilivyoongezewa sukari kama soda na juisi za viwandani, hivi siyo salama
      • Vyakula vulivyokaushwa kwa mafuta kama chips na viazi
      • Vyakula vyenye utindikali mwingi kama limau, nyanya, machungwa , tangawizi na kitungu maji. Badala yake hakikisha unakula
      • Vyakula vya mbogamboga kwa wigi hasa mboga za kijai, matangoo, kuku, nyama kutoka kwa mnyama laiyefugwa na kulishwa majani siyo nafaka, mafuta ya kupikia tumia mafuta ya nazi au mafuta ya mizeituni.
    2. Weka ratiba ya mazoezi na kupunguza uzito na kitambi
      • Maisha ya kizembe ya kutokushugulisha mwili ni chanzo cha uzito mkubwa na kitambi na magonjwa mengine lukuki ya lishe. Hakikisha unapata walau nusu saa kila siku kufanya mazoezi mepesi ili kuweka sawa uzito wako na kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya lishe kama kisukari, kitambi, presha, upungufu wa nguvu za kiume, kuvurugika kwa homoni na mengine mengi.
    3. Epuka uvutaji wa sigara na kunywa pombe kupita kiasi : Uvutaji wa sigara na kunywa pombe unakuongeze hatari ya kupata kiungulia kutokana na kwamba vitu hivi vinaathiri misuli ya mfumo wa chakula na hivo kuongeza utolewaji wa tindikali.
    4. Rekebisha mazingira ya chumbani mwako

    Kama tayari una shida ya kiungulia basi badili namna unavolala usiku. Jaribu zoezi hili. Kwenye kitanda chako upande unakoweka kichwa, chini ya godoro weka nguo ili kunyanyua kisi flani upande huo wa kichwa hii itakusaidia kupata nafuu. Jaribu pia kupata usingizi wa kutosha walau masaa 8 na kuendelea.

    Tiba ya Kiungulia Kutoka india

    Vidonge hivi asili vimekuwa yakitumika kwa muda mrefu huko india kwa ajili ya changamoto mbalimbali kama kiungulia, gesi tumboni, na kukosa choo.
    Hivi sasa vidonge hivi yameonekana kutibu magonjwa mengine zaidi kama bawasili, kuharisha na kuimarisha usagaji wa chakula tumboni.Dozi ya week mbili tu utakuwa umepona kiungulia na kuendelea kufurahia Maisha .

    Gharama za dawa ni Tsh 85,000/= tu Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze tiba