Tag: tumbo kujaa gesi

  • Tumbo kujaa Gesi, Kukosa choo Gesi na Tiba asili ndani ya wiki

    tumbo kujaa gesi

    Nini kinapelekea Tumbo kujaa Gesi

    Kutokakana na lishe mbovu tunayokula kila siku kwa kutegemea zaidi vyakula vya haraka na bei rahisi . Vyanzo vingine vya tatizo ni msongo wa mawazo, matumizi ya vidonge mara kwa mara na mazingira yenye sumu yanayotuzunguka kama moshi wa magari na kemikali za viwandani.

    Kumbuka tatizo la tumbo kujaa gesi inaweza kuwa ni kiashiria cha matatizo makubwa ya kiafya. Mfano fangasi kwenye mfumo wa chakula. Fangasi hawa husababisha upate alegi ya vyakula mbalimbali, magonjwa ya autoimmune na hata saratani ya tumbo.

    Dalili za Tumbo Kujaa Gesi

    Kuwa na gesi tumboni ni tofauti kabisa na kitambi. Kitambi kinaweza kuwa cha muda mrefu lakini tumbo la gesi ni la muda tu baadae husinyaa na kurudi katika hali ya kawaida kwani huletekezwa na hewa kukwama tumboni na kufanya tumbo kutanuka. Kwa watu wengine tumbo linaweza kuwa kubwa kama mjamzito.

    Kwa bahati nzuri ni kwamba tatizo la gesi tumboni linatibika endapo utafata ushauri wetu na kutumia hizi dawa za mimea kwa usahihi. Kwa kesi chache mfano kama tatizo linakutokea mara kwa mara basi kuna haja ya kupanga appointment ukaonana na dactari kwa vipimo. Dalili zingine zinazoambatana na tumbo kujaa gesi ni kama

    Nini Husababisha Tumbo Kujaa Gesi?

    Unaweza ukawa unajiuliza ni kitu gani hasa ambacho ni chanzo cha tumbo kujaa na kufutuka kana kwamba umeshiba sana. Kuna vitu vingi nyuma ya pazia vivoletekeza tumbo kujaa. Kuanzia kwenye aleji, kuvurugika kwa homoni, matatizo kwenye tezi ya thairodi, shida kwenye mfumo wa chakula, na mengine mengi.

    Inaweza kuwa ngumu kujua kinacholetekeza tumbo kujaa geni kwa upande wako lakini kadiri unavojifunza zaidi na kuusoma mwili wako basi utajua vitu gani vya kuepuka.Huwa nasema kila siku kwamba daktari wa kwanza wa mwili wako ni wewe mwenyewe. Ni muhimu kufatilia kwa ukaribu mabadiliko ya mwili wako.

    Sababu 8 Zinazoletekeza Tumbo Kujaa Gesi

    Matatizo kwenye Mmeng’enyo wa Chakula

    Magojwa kama Ulcerative colitis, celiac disease na IBS-inflammatory bowel syndrome huletekeza kujaa gesi kwa tumbo

    Maji kubakizwa mwilini inapelekea tumbo kujaa gesi

    Wakati fulani maji yanaweza kuabakizwa kwenye sehemu fulani za mwili kama kweye magoti, tumboni na kwenye nyonga. Maji haya huletekeza maumivu makali kwenye joints na tumboni. Uwepo wa maji tumboni hujulikana kama ascites na inaweza kuashiria kwamba una tatizo kwenye ini au maambukizi ya bacteria.

    Ndio maana kuna umuhimu wa kufanya vipimo kama una homa ya ini (hepatitis B). kama kuna shida ya ini basi utapata dalili zingine kama kichfuchefu, macho na ngozi kuwa njano, kupungua uzito, kutapikadamu na chakula kutosagwa tumboni.

    Mwili kukosa maji (Dehydration)

    Umewahi kufuatilia siku ukiwa umekunywa sana pombe ama kula zaidi vyakula vyenye chumvi kwa wingi na tumbo likajaa gesi?. Mwili unapokosa maji hufanya uchakataji na usagaji wa chakula kuwa mgumu. Mwili unapokosa maji ya kutosha hufanya kazi ya kuvuta na kuhifadhi maji mengi zaidi pale utakapokunywa maji ili kuepuka kutokea kwa upungufu huu. Maji yanapokuwa mengi kupita kiasi ndipo sasa unaweza kupata choo kigumu ama kukosa choo. Hakikisha unakunywa maji mara nyingi zaidi kila siku ili kuepuka tumbo kujaa gesi.

    Kukosa choo ama kupata choo kigmu/Constipaton

    Constipation inaweza kuwa sababu kubwa ya kwanini tumbo lijae gesi. Constipation inaweza kusababisha choo kigumu, maumivu tumboni na kukosa choo kwa muda mrefu. Kukosa choo na choo kigumu husabishwa na ulaji wa vyakula vilivyokobolewa sana visivyo na kambakamba, matumizi kidogo ya maji, msongo wa mawazo na kuishi bila kufanya mazoezi.

    Alegi ya Chakula inaweza pelekea tumbo kujaa gesi

    Aleji ya vyakula mbalimbali kama maziwa, mayai na ngano vinaweza kuwa ni sababu ya kujaa gesi kwa tumbo lako. Kuna aina nyingi ya vyakula inaweza kusababisha upate mzip ama alegi. Cha kufanya sikiliza mwili wako unasemaje pale unapokula chakula. Kama mwili unakataa aina fulani ya vyakula na unapata mcharuko kama kuvimba, kuharisha, ama kutapika basi usitumie chakula hicho.

    Maambukizi

    Kama mwili unapambana na maambukizi aidha ya bacteria, virusi, fangasi au vimelea wengine basi utapata tatizo la kujaa gesi tumboni kutokana na mpambano wa ugonjwa na seli nyeupe za damu.

    Majeraha Kwenye Mfumo wa Chakula

    Wakati mwingine unaweza kupata gesi tumboni kutokana na vidonda ama uvimbe kwenye baadhi ya sehemu za mfumo wa chakula kama utumbo mdogo na utumbo mpana. Uvimbe unaweza kuzuia utolewaji wa uchafu na kuletekeza gesi na maji kukwama.

    Mabadiliko ya Homoni

    PMS (pre menstrual syndrome) ikimaanisha mkusanyiko wa dalili zisizo za kawaida za kipindi cha hedhi ni chanzo cha tumbo kujaa gesi. Tatizo linaweza kuwa kubwa kama una uvimbe kwenye kizazi na hedhi yako inavurugika. Kwanini wanawake hupata gesi tumbo wakati au karibia na kipindi cha hedhi? Mwanamke anapokaribia hedhi kiwango cha homoni ya estrogen huongezeka na ukuta wa mfuko wa mimba kuongezeka. Pale anapopata siku zake basi damu na maji mengi hutolewa nje na hivo tumbo kurudi katika hali ya kawaida.

    Saratani

    Moja ya dalili za saratani ya utumbo mpana na saratani ya mfuko wa mimba ni tumbo kujaa gesi. Ndio maana ni muhimu kuongea na daktari wako pale ambapo umejaribu kila njia ya kundoa tatizo lako lakini bado halijaisha.

    Vyakula vya Kuepuka pale Unapotaka Kutibu Tatizo la Tumbo Kujaa Gesi

    • Vyakula vya sukari na snacks zilizooongezewa utamu
    • Nafaka na vyakula vya nafaka hasa ngano na Maharage huongeza uzalishaji wa gesi tumboni
    • Vinywaji vilivosindikwa kama soda (Carbonated drinks)

    Njia zingine za Kukusaidia Kuondokana na Tatizo la Tumbo Kujaa Gesi

    1. Tembelea hospitali mara kwa mara kuonana na daktari
      Kutokana na kwamba tumbo kujaa gesi inaweza kuletekezwa na matatizo mengine mengi ya kiafya kama tulivosoma pale juu kuna umuhimu kufanya vipimo mara kwa mara ili kujua chanzo cha tatizo lako. Kumbuka hakuna kipimo kimoja cha kujua kinachokusumbua ni vyema kuongea na dactari wako ili akupe ushauri na vipimo stahili.
    2. Weka ratiba ya kufanya mazoezi: Kufanya mazoezi itakusaidia kuimarisha ufanyaji kazi wa mfumo wa chakula, kurahisisha usafirishaji, na hivo kutoa sumu mwilini. Fanya mazoezi walau dakika 30 mpaka 60 kwa siku mara 3 kwa week.
    3. Kunywa maji ya kutosha: Maji hurahisisha usagaji wa chakula na utolewaji wa choo, Hakikisha unakunywa maji kila unapopata kiu. Hakuna kipimo maalumu cha kiwango cha maji unachotakiwa kutumia unaweza kuanza na glass 6 mpaka 8 itategemea na shughuli unazofanya na mazingira unayoishi.
    4. Punguza msongo wa mawazo

    Tiba Ya tumbo kujaa gesi Kupitia vidonge asili kutoka india

    Vidonge hivi asili vimekuwa yakitumika kwa muda mrefu huko india kwa ajili ya changamoto mbalimbali kama kiungulia, gesi tumboni , vidonda tumbo na kukosa choo.
    Hivi sasa vidonge hivi yameonekana kutibu magonjwa mengine zaidi kama bawasili, kuharisha na kuimarisha usagaji wa chakula tumboni.

    Dawa ni Tsh 85,000/= dozi ya wiki mbili. Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze dozi

  • Kujamba sana kupita kiasi na harufu mbaya

    kujamba sana

    kujamba sana ni karaha

    Wengi wetu lazima umeshapitia hali ya kujamba sana kupita kiasi na kutukosesha raha. Japo kujamba ni kawaida na kila mtu anajamba kila siku, kuna watu wengine wanapata shida ya tumbo kujaa gesi na hivo kutoa gesi chafu mara kwa mara kuliko kawaida. Kitaalamu tatizo hili huitwa flatulence.Na kujamba kupita kiasi hilo ni tatizo kiafya linalohitaji tukupe dawa.

    Ushuzi ni kitu gani

    Ushuzi hutokana na gesi inayozalishwa tumboni kutokana na hewa tunayovuta na matokeo ya uchakataji wa chakula tumboni. Kwahivo kutokea kwa ushuzi inaweza kutofautiana kwa kila mtu kutokana na mazingira na hali yake ya mwili.

    Kama ambavyo umewahi kujishuhudia mwenyewe kuna wakati unajamba ushuzi wenye harufu mbaya. Wakati mwingine hakuna harufu, ama unaweza kujamba kwa sauti au pasiwe na sauti. Mtu mzima mwenye afya anajamba mara 14 mpaka 18 kwa siku. Wakati mwingine anajamba hata bila kujijua kwasabau hakuna harufu au sauti.
    Kwahivo unapotaka kuchambua hali ya afya yako ni muhimu zaidi kutazama harufu ya ushuzi na dalili zingine unazopata baada ya kujamba.

    Je kuna jambo lolote la Kuhofia kuhusu Kujamba kwako?

    Inaweza kuwa ndio au hapana,kwasababu wakati mwingine inategemea na aina ya chakula ulichokula. Mfano ukila vyakula vyenye kambakamba kwa wingi(high-fiber diet) na vyakula asili utapata ushuzi wa kawaida.

    Lakini unapojamba kila mara kupita kiasi na ikiambatana na dalili zingine inaweza kuwa ni kiashiria kwamba kuna tatizo kwenye mfumo wako wa chakula. Tatizo hili laweza kuwa ni mabadiliko ya mazingira ya ndani ya tumbo (microbiome), kutokana na kukua kwa bakteria wabaya au fangasi.

    Kwanini kuna utofauti wa asilimia za gesi zinazounda ushuzi na harufu?

    Hii ni kwasababu hali ya ushuzi inatofautiana kwa mtu na mtu kutokana ni kiasi cha hewa aliyobugia, chakula alichokula na hali ya umeng’enyaji wa chakula tumboni.

    Unaweza kushangaa ni kwanini unajamba lakini hakuna harufu mbaya inayotoka. Kiambata cha sulphur ndicho hufanya harufu kuwa mbaya zaidi ya kunuka. Asilimia moja tu ya sulphur inaweza kuleta harufu mbaya kwenye ushuzi. Kwahiyo kama aina ya chakula ulichokula kinategeneza sulphur kwa wingi basi ushuzi wako utakuwa unanuka.

    Nini hasa kinasababisha Kujamba sana

    Unaweza kuwa unajiuliza nini hasa hupelekea kujikusanya kwa gesi ambayo baadae unaitoa kwa njia ya kujamba. Japo visababishi vya ushuzi vinaweza kutofautiana kwa mtu na mtu lakini gesi inayotolewa ni ile ile haitofautiani.

    Gesi iliyojikusanya tumboni hupita kwenye utumbo mdogo na baadae kutolewa nje kama unavyotoa haja kubwa. Wakati mwingine utoaji wa gesi hii unaweza kuambatana na maumivu hali inayoashiria pengine kuna chakula ulichokula kina tatizo. Au hakijachakatwa vizuri na hivo kuchacha.
    Tatizo lingine kujaa gesi tumbo kikawaida huambatana na kujamba.

    Baadhi ya sababu kwanini gesi inajikusanya tumboni mwako na kukupelekea kujamba ni pamoja na

    Kumeza hewa (aerophagia): Hii inamaanisha kumeza hewa pasipo matarajio ambayo inajikusanya tumbo na kisha unaitoa kwa njia ya kujamba au kwikwi. Sababu mojawapo kwanini unabugia hewa tumboni ni kwasababu unakula chakula haraka au kutotafuna chakula vizuri kabla ya kukimeza. Kwahivo kama unaona wewe ni mtu wa kula haraka , jaribu kurekebisha tabia hii, tafuna taratibu ili usimeze hewa pamoja na chakula.

    Kukusanyika kwa hewa chafu: Kujamba ushuzi unaonuka maranyingi hutokana na gesi inayozalishwa na bacteria waliopo kweye utumbo mpana baada ya uchafu ambayo haujafozwa kuchacha.

    Mabadiliko ya mazingira ya ndani kwenye mfumo wa chakula: Fahamu kwamba katika mfumo wote wa chakula kuanzia mdomoni, kwenye koo, tumboni, mpaka kwenye utumbo kuna bacteria wazuri na wale wabaya. Bacteria wazuri wanasaidia katika uchaataji wa chakula na pia kama kinga dhidi ya athari za bacteria wabaya. sasa inapotokea bacteria wabaya wamakuwa wengi kuzidi wale wazuri ndipo utaanza kupata matatizo kama gesi tumboni na chakula kutosagwa.

    Constipation yaani Kupata choo kigumu na kukosa choo kwa muda mrefu: Inaweza kusababisha mkusanyiko wa gesi chafu na kukupelekea kujamba sana kwasababu ukiwa na tatizo hili kasi ya mmen’genyo wa chakula inapungua.

    Kwanini watu wengi wanajamba kwa sauti na wengine wanajamba polepole na harufu ni mbaya zaidi?

    Hii yaweza kusababishwa na mpangilio wa misuli ya utumbo mpana na eneo la haja kubwa. Baadhi ya misuli inakusaidia kubana ushuzi na kuutoa taratibu pasipo sauti. Kama kila mara ukijamba sauti ni kubwa basi fahamu kwamba misuli ya eneo la haja kubwa sphincter muscles imelegea kiasi kiasi cha kuruhusu hewa kutoka bila ridhaa yako.

    Je kuna Faida yoyote kwako kujamba sana au kuna Madhara

    Kujamba ni kitu cha kawaida na moja ya njia ya mwili kutoa hewa chafu, kama vile tunavyopumua kutoa nje carbondioxide. Kwahivo kama unajamba usihisi kama ni jambo baya la kupambana nalo. Maana wakati mwingine kujamba kunaweza kuwa ni ulinzi na kwama tumbo lako linafanya kazi vizuri.

    Vyakula vyenye kambakamba mfano matunda, mboga za majani, viazi, magimbi, uwele na ugali wa dona husababisha gesi kwenye mfumo wako. Lakini bado vyakula hivo vinatoa mbolea kwa bactetia wazuri kukua ambao watakukinga dhidi ya magonjwa kam saratani ya utumbo, kisukari, uzito mkubwa na kitambi na magonjwa ya moyo.

    Kwa upande mwingine ni kwamba kama unajamba sana kupita kiasi, inaweza kuashiria kuna tatizo la tumbo matatizo haya ni kama

    Mwili kukataa aina fulani ya chakula

    Kutoboka kwa kuta za utumbo mwembamba(leay gut syndrome) na kusababisha sumu na vimelea kuingia kwenye mzunguko wa damu.

    Kukua kwa vimelea kwenye utumbo/small intestinal bacteria overgrowth(SIBO).

    Utajuaje kama una shida ya kujamba sana

    Angalia kama kujamba kwako kunaambatana na dalili hizi ndipo uchukue hatua. Dalili hizi ni kama

    • Kukosa nguvu na uchovu
    • Ngozi kucharuka na kupata rashes au chunusi
    • Aleji mfano kutokwa machozi na koo kuwasha
    • Kuharisha na kukosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu
    • Kupata mkojo wenye damu au kinyesi chenye damu
    • Mumivu kwenye kwapa na katikati ya paja na viungo vya uzazi na
    • Mabadiliko ya joto la mwili, uzito, usingizi na mpangilio wa hedhi
    • Namna gani Upunguze Kujamba sana

    Haya ni matamanio ya kila mmoja wetu ili kupunguza aibu ya kujamba mara kwa mara pengine ukiwa na kundi la watu. Kitu cha kwanza kubadilisha ni lishe yako. Tumbo lako laweza kuwa linapata shida ya kuchakata aina flani ya vyakula au tumbo kuhifadhi zaidi sulphur, fangasi na bacteria.

    Zoezi hili ni la kuajaribu maana watakiwa kufatilia ni aina gani ya chakula inakufanya kujamba sana, na siyo kila chakula kinaleta gesi kwa kila mtu. Baadhi ya vyakula vya kutizama zaidi ni kama

    Maharage: Maharage ni chakula kikubwa ksababisha gesi kulio vingine. Ni kwasababu vimejaa aina ya wanga inayoitwa polysaccharides, ambayo inachacha kiurahisi inapoingia tumboni. Huhitaji kuacha kabisa kula maharage, ila fanya kuloweka kwenye maji usiku mmoja kabla ya kuyapika ili kupunza gesi inayozalishwa.

    Maziwa na bidha za maziwa: kushindwa kumeng’enya maziwa (lactose intolerance) ni tatizo kubwa na linawapata watu wengi. Hii ni kwa bidhaa zote za maziwa. Bidhaa za maizwa zina aina ya sukari zinazouwa galactose na glucose amabazo ni ngumu kuchakatwa kiasi cha kupelekea gesi tumboni.

    Mboga zenye sulphur: Mbona mboga zenye sulphur kwa wingi kama kundi la cruiferous, hapa kuna kabeji, broccoli na caulifolower huletekeza gesi kuliko mboga zozote zingine kwasabau zina kambakamba kwa wingi zaidi. Zinapopikwa gesi inapungua kiasi kuliko kuliwa mbichi.

    Vyakula vilivyosindikwa ma kusafishwa(artificial, processed foods): Baadhi ya vyakula vya viwandani vyenye mafuta mabaya vinaweza kuwa vigumu kuchakatwa na hivo kupelekea gesi tumboni. Lenga kula vyakula asili na kutumia mafuta mazuri kama ya nazi na oilve kama kiungo cha kupikia. Kadiri unavokula vyakula asili nivyo unarahisishia kazi tumbo kusaga chakula vizuri.

    Badili Mtindo wa Maisha ili Kupunguza kujamba sana

    Kufuta kwenye lishe yako vyakula ambavyo siyo rafiki.

    Tumia virutubishi (probiotics) ambavyo vitasaidia kurudia bacteria wazuri tumboni. Vyakula hivi ni kama maziwa asili ya mtindi na sprulina.

    Weka vionjo kwenye lishe yako: Vionjo hivi husaidia kuimarisha usagaji wa chakula na kuua vimelea wabaya tumboni. Vionjo hivi ni kama manjano(tumeric), tangawizi, mdalasini na pilipili.

    Fanya mazoezi na kunywa maji ya kutosha: Vyote hivi kwa pamoja vitakusaidia kutoa uchafu nje ya mwili na kusafirisha virutubishi ndani ya mwili. Mazoezi ya squats ni muhimu zaidi.

    Tiba asili ya hakika ili upone kujambajamba ovyo

    Kama una tatizo la kujamba sana. Muhimu tukupatie Chai tiba ya intestine Cleansing na vidonge vya gasex utumie pamoja. Itakusaidia kusafisha tumbo na kurekebisha mazingira ya mfumo wa chakula.
    Tiba inacost Tsh 95,000/= tu dozi ya mwezi mmoja unamaliza tatizo.

    Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze tiba