Category: Magonjwa ukeni

  • Harufu mbaya ukeni na tiba ya wiki mbili

    harufu mbaya ukeni

    Nini kinapelekea harufu mbaya ukeni?

    Kutunza uke na kulinda afya ya uke ni jambo la muhimu sana kwa mwanamke. Kutokwa na harufu mbaya ukeni ni kiashiria kwamba unaumwa na hauko sawa. Hali hii inaweza kuathiri heshima ya mwanamke na pia mahusiano na mwenza wake.

    Harufu mbaya ukeni kwa kiasi kikubwa husababishwa na fangasi wa candida. Japo siyo kila mara ndio maana kuna umuhimu wa kutafuta chanzo cha tatizo la kunuka uke.

    Kama wewe muhanga wa tatizo hili basi tambua kwamba kuna njia za asili unaweza kuzitumia ikiwemo lishe na virutubisho na ukarudi katika hali ya kawaida. Kesi chache sana kama tatizo litazidi kuendelea basi itatakiwa uende hospitali ili upate uchunguzi.

    Ni kawaida kwa mwanamke kupata harufu ukeni kutokana na hali ya uke kujisafisha kutoa vimelea wabaya. Lakini pale harufu inapokuwa kali sana mfano wa harufu ya shombo la samaki basi ujue kuna tatizo kubwa. Kutokwa na harufu mbaya ukeni huwa inaambatana na dalili zingine kama kuwasha na kuchomachoma na kutokwa na majimaj

    Chanzo cha Harufu Mbaya Ukeni

    Ukuaji wa Bacteria (Bacteria vaginosis)

    Sababu namba moja ya kupata harufu mbaya ukeni ni ukuaji wa bacteria. Bacteria Vaginosis ni ukuaji wa bacteria usio wa kawaida kwenye uke. Rejea maelezo ya pale juu kuhusu sababu ya kukua kwa bacteria wabaya kwenye uke ikiwa ni pamoja na kubadilika kwa mazingira ya ukeni na kushuka kwa kinga.

    Bacteria vaginosis inaweza kupelekea mimba kuharibika, kujifungua kabla ya wakati na kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa mengine ya ngono. Dalili mojawapo ya kwamba tayari una maambukizi ya bacteria ni kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu kali mfano wa harufu ya samaki wabichi

    ugonjwa wa Trichomoniasis waweza kuleta harufu mbaya ukeni

    Trichomoniasis ni moja ya ugonjwa wa ngono unaosababisha harufu kali ukeni. Ugonjwa huu husababishwa vimelea na huambatana na kutokwa na uchafu ukeni,kuwasha, na maumivu makali wakati wa kukojoa.

    Trichomoniasis inaweza kuwaathiri wajawazito na kuleta hatari ya mimba kutoka. Kama utagundua una Trichomoniasis basi wewe na mwenza wako mnatakiwa kutibiwa. Hakikisha pia unatumia condom vizuri kila unapofanya ngono kama kinga dhidi ya magonjwa haya.

    Mabadiliko ya Homoni yanapelekea harufu mbaya ukeni

    Mabadiliko ya homoni kutokana na mzunguko wa hedhi unaweza kuchangia harufu mbaya ukeni. Wanawake wanaokaribia kukoma hedhi wapo kwenye hatari zaidi kwani homoni ya estrogen hupungua sana na hivo kusababisha tishu za kuwa na tindikali kidogo.

    Uchafu na Kutokwa sana na Jasho ni chanzo cha harufu mbaya ukeni

    Ni wazi kwamba uchafu na kuwepo kwa unyevunyevu sehemu za siri huzalisha harufu mbaya. Kisayansi ni kwamba tezi zilizopo ndani ya mwili (apocrine sweat glands )hutengeneza mafuta kuelekea kwenye maeneo ya mwili.

    Maeneo haya ni kama kwapa, pua, ndani ya sikio, uke, na kwenye chuchu. Bacteria waliopo maeneo hayo huchakata mafuta haya na hivo kuzalisha harufu kali. Uvaaji wa nguo zilizobana na uzito kupita kiasi huchangia kuhifadhiwa kwa jasho kwenye mikunjo ya ngozi na hivo kuletekeza harufu.

    Kuvaa Pedi kwa Masaa Mengi inapelekea harufu mbaya ukeni

    Pedi inapovaliwa kwa muda mrefu husababisha ngozi kucharuka,kututumka na kuwasha na pia. Hali hii huchangia kukua kwa bacteria na fangasi wabaya ambao ni chanzo cha harufu.

    Hatua 6 za Kujikinga dhidi ya Harufu Mbaya Ukeni

    1.Vaa nguo za ndani za pamba, zisizobana sana.

    Nguo zilizoabana zinazuia kupita kwahewa safi kuelekea ukeni na hivo kusababisha unyevunyevu ambao ni mbolea kwa bacteria na fangasi wanaoleta harufu mbaya kwenye uke. Hakikisha unabadilisha chupi kila baada ya masaa 12 inasaidia kuzuia kukua kwa bacteria wabaya.

    2.Badili Nguzo zako Kila Baada ya Kufanya Mazoezi

    Nguo zenye unyevu ni mbolea nzuri kwa ukuaji wa bacteria hivo hakikisha unavaa nguo zilizokauka na kubadilisha kila baada ya kutoka mazoezini.

    3.Punguza uzito kama inawezekana

    Uzito mkubwa na kitambi vinakufanya utokwe na jasho kwa wingi zaidi hasa kwenye uke. Na kama tulivojifunza pale juu, jasho na unyevunyevu  inaleta fangasi na bacteria wabaya. Chagua kula lishe nzuri na kufanya mazoezi ili kurekebisha mwili wako. Unaweza kutuma kifurushi chetu cha weight loss package ili upunguze uzito wako vizuri pasipo kujinyima kula.

    Epuka Kusafisha ukeni mara kwa mara

    Kusafisha uke kila mara hasa kwa kutumia kemikali na sabuni inaharibu mazingira ya bacteria wazuri. Bakteria hwa ni walinzi, na hivo kuacha nafasi kwa uke kushambuliwa na bacteria wabaya pamoja na fangasi wa candida.

    Epuka Kutumia Spray na Marashi Ukeni

    Ukweli ni kwamba ngozi ya uke ni laini sana kwa hiyo inanyonya kwa urahisi kemikali zilizopo kwenye spray kuingia kwenye damu. Usiingie kwenye mtego huu, kumbuka miili yetu imeumbwa kujisafisha yenyewe, Pale unapoongeza kitu cha ziada basi unaharibu normal flora na kuharibu kinga ya mwili.

    Epuka Baadhi ya Vyakula Ambavyo ni Adui wa afya yako

    Kuna aina nyingi ya vyakula ambavyo vianweza kukuathiri wewe kama mwanamke kwenye swala la uzazi. Vyakula hivi vinaharibu mazingira ya uke, kuua bacteria wazuri na kubadili PH. Vyakula vyenye sukari, Pombe, ngano na vyakula vilivyosindikwa huchochea ukuaji wa fangasi

    Jaribu tiba zetu asili upone harufu mbaya ukeni ndani ya wiki mbili

    Dozi ni Tsh 95,000/= tu unapona tatizo lako sugu . Tiba hizi zimetupa shuhuda nyingi sana na wewe unaweza kuwa mmoja wa mashuhuda hawa.

    Tuandikie kwa namba zetuy 0678626254

  • Chanzo cha maumivu Ukeni na Tiba

    maumivu ukeni

    Njia ya uke ni njia inayopitisha mbegu za kiume kutoka kweye uume kwenda kwenye mji wa mimba. Maumivu ukeni huchangiwa na sababu za kisaikologia ama uwepo wa maambukizi fulani. Kupata tiba ya mapema kwa tatizo lako la uke ni njia nzuri ya kupunguza uwezekano wa kupata athari zaidi kwa hapo baadae

    Dalili zingine zinazoambatana na maumivu ukeni

    Maumivu ukeni yanatofautiana kwa kutegemea chanzo cha tatizo dalili hizi ni kama ifuatavyo

    • Kuhis hali ya kuungua ukeni
    • kuwasha sana ambapo ukijikuna unapata raha
    • Kupata maelengelenge na
    • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
    • kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu kali kama kuna fungus.

    Nini Kinasababisha Maumivu Ukeni

    Visababishi vikubwa vya maumivu ukeni ni maambukizi ya magonjwa ya

    • Ukavu ukeni kutokana na kukosa uteute mlaini
    • Fangasi ukeni
    • Gonorrhea na
    • Chlamydia
    • Makovu baada ya upasuaji kwenye kujifungua
    • Saratani ya mlango wa kizazi
    • Ukavu wa uke kutokana na kupungua kwa homoni ya estrogen hii inawapata zaidi waliokoma hedhi

    Wanawake wanaougua zaidi kwa kupata maumivu ukeni

    Wanawake wote wapo kwenye hatari ya kupata maumivu ukeni;
    Tatizo la maumivu ya uke huwapata karibu kila mwanamkke kwenye maisha

    Changamoto baadhi za kiafya zinaongeza hatari ya kupata maumivu ya uke. mfano mabadiliko ya homoni kutokana na kujifungua, kukoma hedhi au upasuaji wa kuondoa kizazi huongeza hatari ya kupata maumivu makali ukeni.

    Kutumia baadhi ya dawa pia kwa muda mrefu yanaweza kupelekea mwanamke kupata maumivu ukeni
    Wanawake walioenda umri wanaweza kupatwa na tatizo hili kutokana na kukoma hedhi ambapo utengenezaji wa ute unaolainisha uke hupungua kwa kasi.

    Vipimo Namna ya kugundua chanzo cha Maumivu ukeni

    Kama unapata maumivu ya uke mara kwa mara, weka mihadi uonane na dactari ili akufanyie uchunguzi kujua chanzo cha tatizo lako. Dactari atachukua historia yako ya kuumwa, anaweza kufanya uchunguzi wa kutumia mikono na macho ama uchunguzi zaidi wa wa kimaabara.

    Tiba asili ya maumivu ukeni kutoka kwetu

    Kama unaugua maumivu ukeni, Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze tiba mapema. Kabla ya kukupa tiba tutachukua maelezo yako kwanza