Chanzo cha maumivu Ukeni na Tiba

maumivu ukeni

Njia ya uke ni njia inayopitisha mbegu za kiume kutoka kweye uume kwenda kwenye mji wa mimba. Maumivu ukeni huchangiwa na sababu za kisaikologia ama uwepo wa maambukizi fulani. Kupata tiba ya mapema kwa tatizo lako la uke ni njia nzuri ya kupunguza uwezekano wa kupata athari zaidi kwa hapo baadae

Dalili zingine zinazoambatana na maumivu ukeni

Maumivu ukeni yanatofautiana kwa kutegemea chanzo cha tatizo dalili hizi ni kama ifuatavyo

  • Kuhis hali ya kuungua ukeni
  • kuwasha sana ambapo ukijikuna unapata raha
  • Kupata maelengelenge na
  • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
  • kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu kali kama kuna fungus.

Nini Kinasababisha Maumivu Ukeni

Visababishi vikubwa vya maumivu ukeni ni maambukizi ya magonjwa ya

  • Ukavu ukeni kutokana na kukosa uteute mlaini
  • Fangasi ukeni
  • Gonorrhea na
  • Chlamydia
  • Makovu baada ya upasuaji kwenye kujifungua
  • Saratani ya mlango wa kizazi
  • Ukavu wa uke kutokana na kupungua kwa homoni ya estrogen hii inawapata zaidi waliokoma hedhi

Wanawake wanaougua zaidi kwa kupata maumivu ukeni

Wanawake wote wapo kwenye hatari ya kupata maumivu ukeni;
Tatizo la maumivu ya uke huwapata karibu kila mwanamkke kwenye maisha

Changamoto baadhi za kiafya zinaongeza hatari ya kupata maumivu ya uke. mfano mabadiliko ya homoni kutokana na kujifungua, kukoma hedhi au upasuaji wa kuondoa kizazi huongeza hatari ya kupata maumivu makali ukeni.

Kutumia baadhi ya dawa pia kwa muda mrefu yanaweza kupelekea mwanamke kupata maumivu ukeni
Wanawake walioenda umri wanaweza kupatwa na tatizo hili kutokana na kukoma hedhi ambapo utengenezaji wa ute unaolainisha uke hupungua kwa kasi.

Vipimo Namna ya kugundua chanzo cha Maumivu ukeni

Kama unapata maumivu ya uke mara kwa mara, weka mihadi uonane na dactari ili akufanyie uchunguzi kujua chanzo cha tatizo lako. Dactari atachukua historia yako ya kuumwa, anaweza kufanya uchunguzi wa kutumia mikono na macho ama uchunguzi zaidi wa wa kimaabara.

Tiba asili ya maumivu ukeni kutoka kwetu

Kama unaugua maumivu ukeni, Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze tiba mapema. Kabla ya kukupa tiba tutachukua maelezo yako kwanza

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *