Tiba asili ya Bawasiri Bila upasuaji

Written by

in

bawasiri

Je, Unajua Bawasiri nini Nini?

Bawasiri ni ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya mkundu. Wakati mwingine mishipa hiyo yaweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama. Kitaalamu ugonjwa wa bawasiri tunauita hemorrhoids.

Aina Za Bawasiri

Kuna Aina kuu mbili za bawasiri

(A) Bawasili ya ndani

Hii ni bawasiri inatokea ndani ya mkundu na huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili kwenye hatua za mwanzo mpaka inakuwa sugu. Bawasiri hii inatokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa adamu za ndani ya mkundu.

(B)Bawasili ya nje

Bawasiri hii inatokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa mkundu na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu. Inaweza pia kufanya mishipa ya damu kupasuka na damu kuganda.

Unajuaje Kama tayari una Bawasiri

Je wajua unaweza kuwa na bawasiri lakini usipate dalili na baada ya mfupi tatizo likapotea lenyewe. Dalili moja kubwa kwa wagonjwa wetu wengi ni kuvuja kwa damu, na maumivu makali wakati wa kunya.

Unapoona dalili kama hizi hakikisha unaanza tiba mapema ili usifikie kufanyiwa upasuaji.

Visababishi Vingine Vya  Ugonjwa wa Bawasiri

  • Kula ngano kila siku
  • Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
  • Kuharisha kwa muda mrefu
  • Kukaa kwenye kiti mda mrefu mf watu wa maofisini
  • Kutumia choo cha kukaa kwa muda mrefu

Ushauri wa kufuata wakati unatibu bawasili ili upone mapema

  1. Kula mbogamboga za majani, kwenye kila mlo na nafaka ambazo hazijakobolewa
  2. Usijikamue sana unapoenda chooni
  3. Usikae mda mrefu chooni ukijisaidia, hii inaongeza mgandamizo katika eneo la chini kwenye mishipa ya damu na hivo kukuongeza hatari ya kupata bawasili
  4. Tumia dakika 3 mpaka 5, ama subiri mpaka unapokuwa na haja, kama unajiskia kutoa uchafu lakni ukienda chooni kinyesi hakitoki basi tembea tembea ama fanya zoezi la Squats.
  5. Weka barafu sehemu ya haja kubwa kwa dak 10 mpaka 15 kwa siku kupunguza maumivu makali.
  6. Tumia maji ya mmea wa aloe vera kupaka eneo la mkundu kupooaza maumivu

MUHIMU: Ushauri huu ni kwa ajili ya kupata nafuu ya haraka, hivo hakikisha unafika ofsini kwetu kupata huduma ya dawa na virutubisho, zingatia haya ili kutibu tatizo likaisha kabisa.

Tiba Asili ya bawasiri Tunayoweza kukupatia ukapona ndani ya wiki mbili

Dawa hizi ni dawa asili zilizotengenezwa kwa mimea, zinakuwa kwenye mfumo wa vidonge na mafuta mafuta tiba.

Kumbuka upasuaji kukata nyama siyo suluhisho la kudumu. Njoo uchukue tiba upone na baada ya hapo zingatia ushauri ili tatizo lisijirudie tena

Tiba yetu inajumuisha vidonge vya asili vya kumeza na mafuta ya kupaka, dozi ya wiki mbili. Usihofu kuhusu gharama maana tunakupa huduma za uhakika kumaliza tatizo lako.

Kutokana na ukubwa wa tatizo lako tutapendekeza utumie dozi ngapi za dawa.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *