
Uvimbe kwenye mayai ni Kitu gani
Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke unatokana na mkusanyiko wa majimaji ndani ya mayai ya mwanamke yaani ovary. Kumbuka uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst.
Kwa kawaida mwanamke anakuwa na pande mbili ambazo zinazalisha mayai mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya yanapatikana juu pembezoni mwa mfuko wa uzazi.
Mayai yanakuwa kwenye vifuko vidogo ambavyo hupotea baada ya yai kutolewa kwenye siku za hatari yaani ovulation. inapotokea yai halijatolewa ndipo mifuko hii huanza kujaa maji na kufanya uvimbe. Kumbuka Uvimbe huu unamtokea mwanamke wa umri wowote japo kwa kiasi kikubwa huonekana kwa wanawake waliokoma hedhi.
Makundi ya wanawake waliopo kwenye hatari Zaidi ya kuugua uvimbe kwenye mayai
- Kama familia yako huwa wanaugua vimbe kwenye mayai. Kwa wanawake ambao wazazi wao au watu wao wa karibu kama dada na mama wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo kuna uwezekano mkubwa na wewe ukapata huu ugonjwa.
- mwanamke kuwa mvurugiko wa hedhi.
- mafuta mengi ama uzito mkubwa na kitambi
- Kukosa mimba mda mrefu yaani ugumba na
- kuvunja ungo mapema chini ya miaka 10 ni chanzo cha uvimbe kwenye mayai
Dalili za kuwa una uvimbe kwenye mayai na unahitaji tiba haraka
- Kupata maumivu makali ya tumbo kushoto au kulia, ambayo hayana mwanzo maalum na yanayochoma, maumivu yanaweza kuanzia tumboni na kusambaa eneo la makalio
- Kuhisi tumbo ni zito, limejaa au kuvimba
- Maumivu kwenye matiti na hedhi isiyokuwa na mpangilio maalum
- Maumivu ya nyonga wakati wa hedhi hasa chini mgongoni, maumivu yanaweza kuanza muda mfupi tu baada ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi au mwisho wa hedhi.
- Nyonga kuuma sana baada ya kufanya kazi ngumu, mazoezi au baada ya sex
- Kupatwa na kichefuchefu, kutapika na kutokwa na matone ya damu ukeni siku ambazo siyo za hedhi
Matibabu ya Uvimbe kwenye Mayai
Wanawake wengi wenye vimbe ndogo ndogo lakini kwa sababu hazina shida, hawaendi hospitali kutibiwa . Wanawake hawa wakibeba mimba uvimbe unaongezeka sababu ya mabadiliko ya homoni. Hapo itahitaji kufanyiwa upasuaji wakati wa kutoa mtoto.
Njia kubwa kutibu uvimbe hospitali kwa ni operation kutoa uvimbe. Endapo kama uvimbe ni mkubwa sana daktari anaweza kupendekeza kutolewa na kizazi.
Jaribu tiba zetu asili upone kabla ya upasuaji.
Kama wewe hupendi upasuaji, na unataka kupona kwa njia asili, basi hapa ndio mahali pake sahihi. Tiba zetu asili zinazalishwa nchini India na zimeonesha kuleta matokeo makubwa sana kwa waliotumia. Tumekuwa tukipokea shuhuda nyingi za watu kupona ndani ya mwezi.
Leave a Reply