Category: Tiba kwa wanawake

  • Kuvimba Kisimi na Tiba ya week mbili tu

    kuvimba kisimi

    Kuvimba kisimi au Kinembe ni kitu gani?

    Kisimi au kinembe ni kiungo kinachoonekana mwanzoni mwa uke kwa juu, kazi ya kiungo hiki ni kuchochea hisia na kumfanywa mwanamke kufikia kilele katika tendo la ndoa. Kisimi kinaweza kuonekana kidogo kwa juu lakini napenda ufahamu kwamba kisimi kimejichimbia zaidi kueekea ndani kama mzizi na ni kiungo kikubwa.

    Kwenye andiko hili, tutazungumzia changamoto kadhaa wanazopata wanawake kama kisimi kuvimba, kupanuka, na kuwasha. Endelea kusoma kufahamu zaidi.

    Je kuna Size Sahihi ya Kisimi?

    Japo hakuna kiwango cha kawaida cha kisimi, lakini najua wafahamu kiwango au size ya kila siku ya kisimi chako. Kuna baadhi ya hali au shughuli huweza kusababisha kuvimba kwa kisimi kwa muda flani mfano kuongezeka kwa hisia za mapenzi, na kuna sababu zinazoweza kupelekea kuvimba kwa kisimi kwa muda mrefu.

    Kuvimba kisimi kwa muda mfupi ama siku chache

    Kuvimba kisimi kwa mda mfupi ni kawaida kama mwanamke ameamshwa kihisia. Hisia za kimapenzi zinapokuwa juu,mzunguko wa damu huongezeka kuelekea kwenye via vya uzazi. Kisimi pamoja na mashavu ya uke huongezeka ukubwa katika hichi kipindi, na kupungua ukishafika kileleni.
    Kama mwili wako unasisimuliwa mara kwa mara kimapenzi, na usifike kileleni, basi kisimi kinaweza kuendelea kuwa kimetutumka kwa mda mrefu zaidi.
    Vitu vimngine ikiwemo maambukizi vinaweza kuwa chanzo cha kuvimba kwa kisimi pamoja na mashavu ya uke. Mashavu ya uke yanaweza kuvimba kutokana na
    Aleji na vifaa au kemikali, nguo, cream au manukato
    Maambukizi ya fangasi na bacteria
    Kupiga punyeto na kuingiliwa na kitu kwa muda mrefu kwenye uke.

    Kuvimba kisimi kwa Zaidi ya wiki moja

    Kama tatizo linafikia wiki moja na zaidi linaweza kuwa limesababishwa na

    1. Matatizo ya homoni : Kuwa na homoni nyingi za kiume yania androgens kama testosterone inaweza kupelekea kisimi kuongezeka ukubwa.Wanawake wenye polycystic ovarian syndrome (PCOS) na matatizo mengine ya homoni wanapata changamoto hii ya kukua kwa kisimi.
    2. Vimbe kwenye Mayai (Ovarian Tumors)Uvimbe kwenye mifuko ya mayai huanza kuzalisha homoni za kiume kwa wingi na hivo kuepelekea kuongezeka kwa ukubwa wa kisimi.

    Lini unatakiwa Kumwona Daktari

    kama kisimi au kinembe chako hakirudi katika hali ya kawaida ndani ya siku mja basi unatakiwa kumwona daktari. Unatakiwa pia kumwona daktari kama unapata dalili zingimne kama maumivu na kutokwa na majimaji aidha damu au uchafu. Ni kwa sababu dalili hizi zinaweza kuashiria maambukizi kwenye uke.Hakikisha unamwona daktari unapoona tu dalili zisizo za kawaida. Usisubiri mpaka tatizo liwe kubwa.

    Karibu tukupe tiba asili upone shida ya kuvimba kisimi mara kwa mara. Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254 uanze tiba.

  • Njia Asili kupunguza maumivu ya tumbo la hedhi

    maumivu ya tumbo la hedhi

    BIlashaka unajua kwamba maumivu ya tumbo la hedhi ni kitu kinachokosesha raha na kukera sana kwa wanawake wengi. Maana inaweza kutatiza shughuli zako za kila siku kama masomo, biashara na hata shuguli za kiofisi. Tatizo la maumivu kipindi cha hedhi kwa kitaalamu tunaita dysmennorrhea.

    Tumeandika makala hii yenye uchambuzi wa kina kwa tatizo hili linalowatesa wanawake wengi . Utajifunza chanzo cha tatizo na namna gani utumie njia rahisi nyumbani kwako kupunguza makali ya maumivu wakati unajiandaa kuanza tiba yetu ya uhakika.

    Maumivu ya tumbo ala hedhi ni kitu gani

    Dysmenorrhea ni jina la kitabibu kwa maumivu kipindi cha hedhi. Maumivu ambayo hutokana na kusinyaa kwa misuli ya mji wa mimba. Wakati wa hedhi misuli husinyaa, ili kuruhusu kumeguka kwa ukuta na kutoa damu iliyochanganyika na yai ambalo halikurutubishwa nje. Maumivu haya yamegawanyika katika aina mbili

    Aina Ya Kwanza Ya maumivu ya Kawaida yaani Primary Dysmenorrhea

    Haya maumivu ni ya kawaida kwa wanawake wanapopitia kipindi hiki ambacho hujirudia kila mwezi. Maumivu kikawaida huanza kati ya siku moja ama mbili kabla ya hedhi kuanza kutoka. Mwanamke anaweza kujiskia mamumivu haya kwenye tumbo la chini, kwenye nyonga na kiuno kwa ujumla.

     Maumivu Aina Ya Pili Yasiyo Ya Kawaida yaani Secondary Dysmenorrhea

    Maumivu haya ni kutokana na tatizo fulani la kiafya kweye via vya uzazi vya mwanamke. Changamoto kama vile uvimbe ambayo siyo wa saratani ndani ya mfuko wa mimba uterine fibroids, kukua kwa tishu laini za mfuko wa mimba kuelekea kwenye viungo vingine kama uke na mifuko ya mayai .

    Na pia kupanuka kwa ukuta wa uterus kutokana na kukua kwa tishu za ndani za uterus kuelekea ukuta wa nje (adenomyosis). Maumivu haya pia yasiyo ya kawaida yanaweza kuwa yamesababishwa kwa athari za bacteria ama virusi katika via vya uzazi.

    Kikawaida maumivu haya huanza mapema zaidi wakati wa hedhi ya huchukua muda mrefu zaidi kuisha ukilinganisha na ile aina ya kwanza pale juu. Na pia maumivu haya yanakuwa hayaambatani na kutapika, kuharisha, kizunguzungu wala kukosa nguvu na ganzi.

    Viungo vinavyoathirika zaidi na maumivu ya tumbo la hedhi

    • Via vya uzazi-kama maumivu yako ni kutokana na kukua zaidi kwa tishu za uterus basi maumivu husambaa hadi kwenye tumbo la uzazi.
    • Tumbo la chini-huathirika pia na maumivu haya kwa kiasi kikubwa, kama maumivu haya ni kutokana na kukua kwa tishu za uterus basi mwanamke anahisi kama ameunguzwa na kitu cha moto kwenye tumbo.
    • Maumivu chini ya mgongo- mara nyingi hutokana na kukua kwa tishu za uterus kuelekea kwenye uke na pia kwenye mifuko ya mayai.
    • Miguu– maumivu yanaweza pia kutekea kwenye hips yakishuka chini ya miguu na kufanya mwanamke kushindwa kutembea .
    • Maumivu ya kisaikologia hutokea pia kwa kiwango kukubwa kwa wanawake ambao maumivu yao ni sababu ya vimbe za kizazi. Wanawake hawa wanapata msongo wa mawazo kutokana na kufikiri kwamba
      • Labsa tatizo la uvimbe haliwezi kupona na hakuna dawa
      • Ama hawataweza kupata mtoto kwa siku za baadae
      • Mahusiano ya Rafiki ama wapenzi wao yatavunjika kama wakijua ana tatizo la uvimbe
      • Ama kufikiri jinsi ambavyo hawatafanya kazi zao vizuri na kutofurahia maisha kama mwanzo walipokuwa wazima.

    Nini chanzo cha maumivu ta tumbo la hedhi?

    Maumivu yanatokana na kitendo cha misuli ya kizazikukaza na kusinyaa. Kitendo hiki kinaendeshwa na homoni . Ni kawaida kwa mfuko wa mimba kusinyaa kipindi chote cha mzunguko wa hedhi ambacho huchukua siku 28.

    Lakini utofauti ni kwamba wakati wa kutoa hedhi yenyewe mfuko huu husinyaa na kujikaza zaidi na hivo kukatisha hewa safi ya oyygen kufika kwenye misuli ya mfuko huu wa mimba. Maumivu ni matokeo ya kukosekana kwa muda kwa hewa ya oxygen kwenye baadhi ya misuli ya uterus.

    Huduma ya kwanza/Kitu gani Ufanye ukipata Maumivu ya tumbo la Hedhi

    Kuna njia nyingi ambazo husaidia kupunguza maumivu ya hedhi ambazo unaweza kutumia ukiwa nyumbani kwako pasipo kwenda hospitali. Kama mauvimu ni makali sana unaweza

    • Kumeza dawa za kukata maumivu kama asprini na ibuprofen kwa ahueni ya haraka. Angalizo: dawa za maumivu isiwe ni nia ya kutumika kila mara kwani madhara yake ni makubwa kiafya, dawa hizi zitumike kwa uangalifu.
    • Tumia maji ya uvuguvugu kukandakanda mahali pa tumbo la chini ukiwa umelala chali
    • Usitumie vinywaji na vyakula vyenye caffeine mfano majani ya chai na kahawa na chocolate
    • Fanya masaji kwenye upande wa chini wa mgongo na sehemu ya tumbo la chini.
    • Pumzika zaidi
    • Weka ratiba ya kufanya mazoezi mara kwa mara,wanawake wanaofanya mazoezi hupunguza maumivu ya hedhi kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na wasiofanya mazoezi.

    Lini unatakiwa kwenda hospital kupimwa?

    Kama maumivu yako  ni makali zaidi kuliko kawaida na yanachukua zaidi ya siku 5. Hakikisha unamwona haraka, kwanini?. Kwasababu yawezekana maumivu yako siyo ya kawaida na yaweza kuwa una uvimbe au PID.

    Tiba yetu Asili kutoka india kwa Tsh 85,000/= tu

    Dawa ni asili na zimetengenezwa nchini India kupitia mimea ua Ashoka, Asaparagus na lodh tree na kanchnar . Kwa miaka zaidi ya mitano ambayo tumekuwa tukihudumia wagonjwa wetu wa matatizo ya hedhi na homoni, tumepokea shuhuda lukuki. Ndani ya week mbili utakaa sawa

    Baada ya kutumia tiba zetu tegemea kupata matokeo haya

    • Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi kuisha kabisa
    • Homoni zako kubalansi
    • Mzunguko wa hedhi kurekebika na kuanza kupata kila mwezi
    • Hedhi yako kuwa nyepesi ya kawaida na
    • Kizazi kuimarika sana hata kuongeza chansi ya kushika mimba kama wewe ni muhanga wa kukosa mimba kwa muda mrefu.

    Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze tiba mapema

  • Muwasho ukeni na Tiba ya wiki mbili tu

    muwasho ukeni

    Nini husababisha Muwasho ukeni na kuvimba ukeni

    • Kuugua fungus ukeni
    • Maambukizi ya bacteria ukeni
    • kuvurugika kwa uwiano wa viumbe kwenye mazingira ya uke (vaginal microflora) ambayo inahusisha uwepo wa bacteria na fangasi pia
    • Kukoma hedhi ambapo inafanya uke uwe mkavu sana

    Vipimo kwa tatizo la Muwasho ukeni

    Kama tatizo litaendelea na dalili kuwa kali zaidi ya wiki hapo utahitaji kwenda kupima uanze tiba. Dactari atafanya pelvic examnation ambapo atangalia dalili anazopata mgonjwa kwenye via vya uzazi eneo la nje la uke, mfuko wa mimba, mlango wa kizazi, mirija ya uzazi, kibofu cha mkojo na mifuko ya mayai Daktari pia anaweza kuchukua sample ya uchafu unaotoka na kuufanyia vipimo ili kugundua chanzo cha tatizo.

    Tiba ya tatizo hili la kuwasha kwa uke itategemea na chanzo ama ugonjwa unaosababisha kama ugonjwa

    Ushauri wa Kufuata na Tiba Mbadala kama Unapata Muwasho Ukeni.

    1. Epuka kuvaa pedi mds mrefu, kutumia cream na spray zenye harufu kali tabia hizi zinavuruga mazingira ya ukeni na kutoa mwanya wa fangasi na bacteria kukua.
    2. Tumia maji na sabuni zisizo na kemikali kujisafisha ukeni na usioshe uke zaidi ya mara moja kwa siku.
    3. Unapojisafisha ukeni fifute kuanzia mbele kwenda nyuma. Kufanya hizi inazuia kusambaa kwa bacteria walioko mkunduni kwenda ukeni.
    4. Vaa nguo za ndani za pamba ambazo huruhusu hewa kupita na kukausha unyevu ambao ni mbolea kwa fangasi na bacteria wabaya.
    5. Epuka kufanya kusafisha uke kupita kiasi
    6. Tumia condom ili kujikinga na magonjwa ya zinaa
    7. Usifanye sex mpaka pale ukishapona ugonjwa

    Tiba kwa Tatizo la Muwasho ukeni

    Kwa mwanamke mwenye changamoto ya muwasho na harufu mbaya ukeni,hedhi kuvurugika, tunashauri atumie tiba zetu asili kutoka india apone haraka ndani ya wiki mbili

    Tuandikie kwa namba 0678626254 uanze tiba

  • Chanzo cha maumivu Ukeni na Tiba

    maumivu ukeni

    Njia ya uke ni njia inayopitisha mbegu za kiume kutoka kweye uume kwenda kwenye mji wa mimba. Maumivu ukeni huchangiwa na sababu za kisaikologia ama uwepo wa maambukizi fulani. Kupata tiba ya mapema kwa tatizo lako la uke ni njia nzuri ya kupunguza uwezekano wa kupata athari zaidi kwa hapo baadae

    Dalili zingine zinazoambatana na maumivu ukeni

    Maumivu ukeni yanatofautiana kwa kutegemea chanzo cha tatizo dalili hizi ni kama ifuatavyo

    • Kuhis hali ya kuungua ukeni
    • kuwasha sana ambapo ukijikuna unapata raha
    • Kupata maelengelenge na
    • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
    • kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu kali kama kuna fungus.

    Nini Kinasababisha Maumivu Ukeni

    Visababishi vikubwa vya maumivu ukeni ni maambukizi ya magonjwa ya

    • Ukavu ukeni kutokana na kukosa uteute mlaini
    • Fangasi ukeni
    • Gonorrhea na
    • Chlamydia
    • Makovu baada ya upasuaji kwenye kujifungua
    • Saratani ya mlango wa kizazi
    • Ukavu wa uke kutokana na kupungua kwa homoni ya estrogen hii inawapata zaidi waliokoma hedhi

    Wanawake wanaougua zaidi kwa kupata maumivu ukeni

    Wanawake wote wapo kwenye hatari ya kupata maumivu ukeni;
    Tatizo la maumivu ya uke huwapata karibu kila mwanamkke kwenye maisha

    Changamoto baadhi za kiafya zinaongeza hatari ya kupata maumivu ya uke. mfano mabadiliko ya homoni kutokana na kujifungua, kukoma hedhi au upasuaji wa kuondoa kizazi huongeza hatari ya kupata maumivu makali ukeni.

    Kutumia baadhi ya dawa pia kwa muda mrefu yanaweza kupelekea mwanamke kupata maumivu ukeni
    Wanawake walioenda umri wanaweza kupatwa na tatizo hili kutokana na kukoma hedhi ambapo utengenezaji wa ute unaolainisha uke hupungua kwa kasi.

    Vipimo Namna ya kugundua chanzo cha Maumivu ukeni

    Kama unapata maumivu ya uke mara kwa mara, weka mihadi uonane na dactari ili akufanyie uchunguzi kujua chanzo cha tatizo lako. Dactari atachukua historia yako ya kuumwa, anaweza kufanya uchunguzi wa kutumia mikono na macho ama uchunguzi zaidi wa wa kimaabara.

    Tiba asili ya maumivu ukeni kutoka kwetu

    Kama unaugua maumivu ukeni, Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze tiba mapema. Kabla ya kukupa tiba tutachukua maelezo yako kwanza

  • Uvimbe kwenye mayai na Tiba bila upasuaji

    uvimbe kwenye mayai

    Uvimbe kwenye mayai ni Kitu gani

    Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke unatokana na mkusanyiko wa majimaji ndani ya mayai ya mwanamke yaani ovary. Kumbuka uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst.

    Kwa kawaida mwanamke anakuwa na pande mbili ambazo zinazalisha mayai mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya yanapatikana juu pembezoni mwa mfuko wa uzazi.

    Mayai yanakuwa kwenye vifuko vidogo ambavyo hupotea baada ya yai kutolewa kwenye siku za hatari yaani ovulation. inapotokea yai halijatolewa ndipo mifuko hii huanza kujaa maji na kufanya uvimbe. Kumbuka Uvimbe huu unamtokea mwanamke wa umri wowote japo kwa kiasi kikubwa huonekana kwa wanawake waliokoma hedhi.

    Makundi ya wanawake waliopo kwenye hatari Zaidi ya kuugua uvimbe kwenye mayai

    • Kama familia yako huwa wanaugua vimbe kwenye mayai. Kwa wanawake ambao wazazi wao au watu wao wa karibu kama dada na mama wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo kuna uwezekano mkubwa na wewe ukapata huu ugonjwa.
    • mwanamke kuwa mvurugiko wa hedhi.
    • mafuta mengi ama uzito mkubwa na kitambi
    • Kukosa mimba mda mrefu yaani ugumba na
    • kuvunja ungo mapema chini ya miaka 10 ni chanzo cha uvimbe kwenye mayai

    Dalili za kuwa una uvimbe kwenye mayai na unahitaji tiba haraka

    • Kupata maumivu makali ya tumbo kushoto au kulia, ambayo hayana mwanzo maalum na yanayochoma, maumivu yanaweza kuanzia tumboni na kusambaa eneo la makalio
    • Kuhisi tumbo ni zito, limejaa au kuvimba
    • Maumivu kwenye matiti na hedhi isiyokuwa na mpangilio maalum
    • Maumivu ya nyonga wakati wa hedhi hasa chini mgongoni, maumivu yanaweza kuanza muda mfupi tu baada ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi au mwisho wa hedhi.
    • Nyonga kuuma sana baada ya kufanya kazi ngumu, mazoezi au baada ya sex
    • Kupatwa na kichefuchefu, kutapika na kutokwa na matone ya damu ukeni siku ambazo siyo za hedhi

    Matibabu ya Uvimbe kwenye Mayai

    Wanawake wengi wenye  vimbe ndogo ndogo lakini kwa sababu hazina shida, hawaendi hospitali kutibiwa . Wanawake hawa wakibeba mimba uvimbe unaongezeka sababu ya mabadiliko ya homoni. Hapo itahitaji kufanyiwa upasuaji wakati wa kutoa mtoto.

    Njia kubwa kutibu uvimbe hospitali kwa ni operation kutoa uvimbe. Endapo kama uvimbe ni mkubwa sana daktari anaweza kupendekeza kutolewa na kizazi.

    Jaribu tiba zetu asili upone kabla ya upasuaji.

    Kama wewe hupendi upasuaji, na unataka kupona kwa njia asili, basi hapa ndio mahali pake sahihi. Tiba zetu asili zinazalishwa nchini India na zimeonesha kuleta matokeo makubwa sana kwa waliotumia. Tumekuwa tukipokea shuhuda nyingi za watu kupona ndani ya mwezi.