Tag: kulainisha choo

  • Choo chenye Damu

    choo chenye damu

    Nini kinapelekea upate choo chenye damu?

    Kupata choo chenye damu ni jambo hatari, na utanatakiwa kutibiwa haraka. Kikawaida rangi ya kinyesi inatakiwa kuwa brown au mpauko. Uwepo wa damu kwenye haja kubwa inaweza kupelekewa na kuvuja damu kwenye mishipa ya eneo la ndani la mkundu.

    Wakati mwingine uwepo wa damu kwenye kinyesi inaweza kuwa ngumu kugundua. Lakini ikaambatana na dalili zingine kama maumivu ya tumbo,  mwili kuishiwa nguvu na kuchoka sana. Piua unaweza kupata shida kwenye kupumua, kutapika kubadili kwa mapigo ya moyo, kuharisha damu, na uzito kupungua kwa kasi.

    Je choo chenye kamasi kina shida?

    Kupata na kinyesi au choo chenye kamasi ni hali ya kawaida na nzuri kiafya. Kamasi hii inakusaidia kutoa hajakubwa kwa ulaini pasipo kujikaza. Lakini kamasi lisiwe jingi sana. Ukianza kuona kamasi linazidi basi kuna tatizo kubwa la kiafya na unatakiwa uende hospitali kupimwa.

    Mazingira hatari yanayopelekea Upate choo chenye damu.

    • Kuvimba kwa mishipa ya damu ndani ya mkundu
    • Kulegea kwa eneo juu ya tumbo kutokana na kutapika sana
    • Damu kutofikia baadhi ya maeneo ya utumbo mkubwa
    • msongo mkali wa mawazo
    • Kuvimba na kututumka kwa ukuta wa tumbo na hivo kuanza kuvuja damu
    • Kutanuka kwa mishipa ya damu iliyopo tumbomi
    • Kujeruhiwa kwenye eneo la mkundu
    • Kuugua bawasiri mda mrefu na
    • Saratani ya utumbo mpana

    Ushauri wa kufata kutibu hida ya choo chenye damu

    Kwenye kutibu hili tatizo muhimu sana tazama chanzo cha tatizo na siyo kutibu dalili. Hapa chini ni njia asili unazoweza kufanya pale unapoona kuna damu kwenye kinyesi kama tatizo linasababishwa na

    Vidonda vya Tumbo sugu

    Kama vidonda vyako tumboni vinavuja damu basi unaweza kupata dalili kama kutapika damu. Vidonda hivi ni mareraha tumboni yanayotokana na kuliwa kwa ukuta wa tumbo na tindikali. Mara nyingi huambatana na maumivu makali ya tumbo.

    Kutibu tatizo hili anza kwa kuepuka baaadhi ya vyakula ambavyo vinaongeza ukubwa wa tatizo. Vyakula kama vya ngano, pombe, sukari iliyochakatwa sana, kahawa na vinywaji vya soda. Badala yake kula zaidi vyakula vyenye kambakamba ambavyo havijakobolewa, mboga za majani, nazi na mafuta ya nazi. Tafiti zinasema kwamba matumizi ya juisi ya kabeji kila siku husaidia kuponya vidonda vya tumbo.

    Gastritis au kuvimba kwa tumbo la chakula

    Gastritis ni tatizo la kiafya ambalo hutokana na kuvimba na kututumka kwa tishu za ukuta wa ndani wa tumbo. Dalili za gastritis hufanana sana na zile za vidonda vya tumbo. Hakikisha unatumia vyakua vyenye kambakamba kwa wingi, Vitamin B12 na mafuta ya omega 3. Na kisha uepuke vyakula vyenye tindikali kwa wingi kama machungwa na nyanya.

    Diverticulitis-Utumbo mpana kuvimba

    Diverticulitis ni hali ya kuvimba kwa sehemu ya ndani ya utumbo mpana. Supu ya mifupa na protein powder husaidia katika kumeng’enya chakula vizuri. Kula vyakula vyenye kambakamba kwa wingi ni muhimu.

    Kula Mbogamboga za kijani kwa wingi kutibu choo chenye damu

    Licha ya kuwa na kambakamba nyingi kwenye mboga za kijani, pia kuna madini mengi ya magnesium ambayo tumeona hapo juu husaidia katika ufanyaji kazi mzuri wa misuli na hivo kupunguza tatizo la kukosa choo ama kupata choo kigumu.

    Tumia tiba hii asili kutoka kwetu upone haraka.

    Dawa zetu ni tiba asili kutoka india, zitakusaidia kuekebisha choo, kuondoa hali ya kuvimba kwenye kuta za mkundu na hivo kutibu shida ya choo chenye damu haraka sana. Pia dawa hizi zinatibu bawasili hata kama ni sugu ya mda mrefu.

    Tuandikie kwa namba 0678626254 uanze tiba

  • Tiba asili ya Bawasiri Bila upasuaji

    bawasiri

    Je, Unajua Bawasiri nini Nini?

    Bawasiri ni ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya mkundu. Wakati mwingine mishipa hiyo yaweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama. Kitaalamu ugonjwa wa bawasiri tunauita hemorrhoids.

    Aina Za Bawasiri

    Kuna Aina kuu mbili za bawasiri

    (A) Bawasili ya ndani

    Hii ni bawasiri inatokea ndani ya mkundu na huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili kwenye hatua za mwanzo mpaka inakuwa sugu. Bawasiri hii inatokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa adamu za ndani ya mkundu.

    (B)Bawasili ya nje

    Bawasiri hii inatokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa mkundu na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu. Inaweza pia kufanya mishipa ya damu kupasuka na damu kuganda.

    Unajuaje Kama tayari una Bawasiri

    Je wajua unaweza kuwa na bawasiri lakini usipate dalili na baada ya mfupi tatizo likapotea lenyewe. Dalili moja kubwa kwa wagonjwa wetu wengi ni kuvuja kwa damu, na maumivu makali wakati wa kunya.

    Unapoona dalili kama hizi hakikisha unaanza tiba mapema ili usifikie kufanyiwa upasuaji.

    Visababishi Vingine Vya  Ugonjwa wa Bawasiri

    • Kula ngano kila siku
    • Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
    • Kuharisha kwa muda mrefu
    • Kukaa kwenye kiti mda mrefu mf watu wa maofisini
    • Kutumia choo cha kukaa kwa muda mrefu

    Ushauri wa kufuata wakati unatibu bawasili ili upone mapema

    1. Kula mbogamboga za majani, kwenye kila mlo na nafaka ambazo hazijakobolewa
    2. Usijikamue sana unapoenda chooni
    3. Usikae mda mrefu chooni ukijisaidia, hii inaongeza mgandamizo katika eneo la chini kwenye mishipa ya damu na hivo kukuongeza hatari ya kupata bawasili
    4. Tumia dakika 3 mpaka 5, ama subiri mpaka unapokuwa na haja, kama unajiskia kutoa uchafu lakni ukienda chooni kinyesi hakitoki basi tembea tembea ama fanya zoezi la Squats.
    5. Weka barafu sehemu ya haja kubwa kwa dak 10 mpaka 15 kwa siku kupunguza maumivu makali.
    6. Tumia maji ya mmea wa aloe vera kupaka eneo la mkundu kupooaza maumivu

    MUHIMU: Ushauri huu ni kwa ajili ya kupata nafuu ya haraka, hivo hakikisha unafika ofsini kwetu kupata huduma ya dawa na virutubisho, zingatia haya ili kutibu tatizo likaisha kabisa.

    Tiba Asili ya bawasiri Tunayoweza kukupatia ukapona ndani ya wiki mbili

    Dawa hizi ni dawa asili zilizotengenezwa kwa mimea, zinakuwa kwenye mfumo wa vidonge na mafuta mafuta tiba.

    Kumbuka upasuaji kukata nyama siyo suluhisho la kudumu. Njoo uchukue tiba upone na baada ya hapo zingatia ushauri ili tatizo lisijirudie tena

    Tiba yetu inajumuisha vidonge vya asili vya kumeza na mafuta ya kupaka, dozi ya wiki mbili. Usihofu kuhusu gharama maana tunakupa huduma za uhakika kumaliza tatizo lako.

    Kutokana na ukubwa wa tatizo lako tutapendekeza utumie dozi ngapi za dawa.