Tag: Tiba ya PID

  • PID sugu na Tiba ya Wiki mbili tu

    PID sugu

    Tiba asili ya PID sugu inapatikana hapa, ila kwanza unatakiwa kujua PID ni kitu gani.

    PID sugu ni hali ya kututumka, kuvimba au kucharuka kwa sehemu ya njia ya uzazi kwa mwanamke kunakosababishwa na athari ya bakteria, fungus au hata virusi kwenye kizazi. Sehemu hizi zinazoathiriwa ni kama mirija ya uzazi na mifuko ya mayai yani ovary.

    Haya ni mambukizi ya bacteria yanayoathiri sana wanawake kwenye mfumo wa uzazi. Na kuweza kuleta athari katika sehemu zozote kwenye njia ya uzazi. Moja ya madhara ya makubwa ya PID ni kuzuba kwa mirija ya uzazi na hivo kuutoweza kushika mimba yaani ugumba.

    Tafiti zinasema kati ya wanawake nane waliowahi kuugua PID basi mmoja wao atakutana na shida kupata mimba siku zijazo. Huku wale wanaofanikiwa kupata ujauzito basi hupata matatizo pia ikiwemo mimba kuharibika au kuzaa njiti.

    Nini kinasababisha PID sugu?

    Madkatari wa afya ya binaadamu wanaamini kwamba magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa ipasavyo hasahasa gonorrhea na chlamydia yanaongoza kwa kusababisha PID. Japo kuna baadhi ya wanawake wanaugua PID pasipo magonjwa ya zinaa hasa wale waliotoa mimba. Pengine kutokana na maambukizi ya kawaida ya bacteria.

    Madhara ya PID sugu kwenye kizazi

    • Kuziba kwa mirija ya uzazi na kukosa mimba
    • makovu kwenye mirija ya uzazi na kupelekea kujifungua njiti
    • Maumivu ya tumbo ya muda mrefu husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa na mwanamke kutofurahisa unyumba.
    • Kupata matatizo Zaidi wakati wa ujauzito na kujifungua.

    Je mtu aliyetoa mimba anaweza kuugua PID sugu?

    Jibu ni ndio, endapo umetoa mimba unakuwa kwenye hatari kubwa ya kuugua PID. Hii ni kutokana na mazingira ya uke kuvurugika na hivo kurhusu bakteria kusambaa mpaka eneo la uzazi. PID kwa mwanamke alieytoa mimba endapo haitatibiwa yaweza kupelekea mirija kuziba na hivo ukashindwa kushika mimba siku za mbele. Unatakiwa kusafisha kizazi kupitia vidonge vya UCP ama ukasafishwa hospitali kwa vyuma.

    Dalili Za PID sugu

    1. Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ambayo yanaweza kuwa upande mmmoja au pande zote kulia na kushoto
    2. uke kuwa na ulaini sana
    3. Kupata maumivu wakati wa sex na hata kuvuja damu
    4. Kuvurugika kwa hedhi
    5. Kupata majimaji ukeni isiyo kawaida hasa yenye rangi ya njano na kijani
    6. Maumivu makali wakati wa kukojoa
    7. Maumivu wakati wa kunya
    8. Homa, kizunguzungu, mwili kukosa nguvu, kukosa hamu ya kula na uchovu mwingi.

    Dalili za magonjwa ya zinaa yanayoleta PID sugu ni kama

    • Kutokwa na uchafu kupita kiasi ukeni, wenye rangi ya njano na kijani na unaonuka kwenye.
    • Maumivu makali wakati wa kukojoa na kutoa haja kubwa
    • Kupata maumivu mahala pa haja kubwa na kutokwa na uchafu

    Mazingira Na Sababu Hatarishi Zinaongeza Uwezekano Wa Kupata PID sugu

    • wanawake wenye umri kati ya miaka 25 mpaka 35
    • Kufanya ngono bila kinga na watu wengi
    • Wanawake waliowahi kuugua PID huko nyuma ama kupata maambukizi mengine ya bacteria kwenye njia ya uzazi.
    • Kusafishwa kizazi mara kwa mara kwa vyuma
    • matumizi ya kemikali kujisafisha ukeni, kitendo ambacho kinaharibu viumbe wazuri na kusababisha ukuaji wa bacteria wabaya na fangus
    • Matumizi ya kitanzi kwa ajili ya kupanga uzazi
    • Kuugua UTI mara kwa mara, na wanawake waliwahi kutoa mimba wapo kwenye hatari zaidi ya kupata PID
    • Uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya.

    Ushauri wa kufuata wakati unajipanga kuchukua tiba zetu asili

    Tumia sabuni zisizo na harufu kali(mild soap) kujisafisha, na jisafishe kwa maji tu eneo la uke bila kuingiza vidole ndani
    Ukiwa kwenye hedhi tumia pedi zisizo na kemikali, pedi za asili zisizo na harufu kali. Hii itasaidia kuzuia ukuaji wa bacteria kwenye uke.

    Epuka kujisafisha mara kwa mara ukeni. Kujisafisha kupita kiasi kunaharibu mpangilio wa kawaida wa bacteria kwenye uke(normal flora)

    Tiba asili ya PID sugu ndani ya week mbili kwa Tsh 95,000/ tu

    Kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID, maambukizi ya bacteria na hedhi kuvurugika. Tunashauri atumie uterus cleansing pill pamoja na Lukol kusafisha kizazi na kutibu maambukizi. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 2 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama , harufu mbaya ukeni, muwasho, fangasi, PID na maambukizi ya bakteria. Na Lukol ipo kwenye mfumo wa vidonge 60 vya kumeza kwa week mbili.

    Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze tiba haraka

  • Chanzo cha maumivu Ukeni na Tiba

    maumivu ukeni

    Njia ya uke ni njia inayopitisha mbegu za kiume kutoka kweye uume kwenda kwenye mji wa mimba. Maumivu ukeni huchangiwa na sababu za kisaikologia ama uwepo wa maambukizi fulani. Kupata tiba ya mapema kwa tatizo lako la uke ni njia nzuri ya kupunguza uwezekano wa kupata athari zaidi kwa hapo baadae

    Dalili zingine zinazoambatana na maumivu ukeni

    Maumivu ukeni yanatofautiana kwa kutegemea chanzo cha tatizo dalili hizi ni kama ifuatavyo

    • Kuhis hali ya kuungua ukeni
    • kuwasha sana ambapo ukijikuna unapata raha
    • Kupata maelengelenge na
    • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
    • kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu kali kama kuna fungus.

    Nini Kinasababisha Maumivu Ukeni

    Visababishi vikubwa vya maumivu ukeni ni maambukizi ya magonjwa ya

    • Ukavu ukeni kutokana na kukosa uteute mlaini
    • Fangasi ukeni
    • Gonorrhea na
    • Chlamydia
    • Makovu baada ya upasuaji kwenye kujifungua
    • Saratani ya mlango wa kizazi
    • Ukavu wa uke kutokana na kupungua kwa homoni ya estrogen hii inawapata zaidi waliokoma hedhi

    Wanawake wanaougua zaidi kwa kupata maumivu ukeni

    Wanawake wote wapo kwenye hatari ya kupata maumivu ukeni;
    Tatizo la maumivu ya uke huwapata karibu kila mwanamkke kwenye maisha

    Changamoto baadhi za kiafya zinaongeza hatari ya kupata maumivu ya uke. mfano mabadiliko ya homoni kutokana na kujifungua, kukoma hedhi au upasuaji wa kuondoa kizazi huongeza hatari ya kupata maumivu makali ukeni.

    Kutumia baadhi ya dawa pia kwa muda mrefu yanaweza kupelekea mwanamke kupata maumivu ukeni
    Wanawake walioenda umri wanaweza kupatwa na tatizo hili kutokana na kukoma hedhi ambapo utengenezaji wa ute unaolainisha uke hupungua kwa kasi.

    Vipimo Namna ya kugundua chanzo cha Maumivu ukeni

    Kama unapata maumivu ya uke mara kwa mara, weka mihadi uonane na dactari ili akufanyie uchunguzi kujua chanzo cha tatizo lako. Dactari atachukua historia yako ya kuumwa, anaweza kufanya uchunguzi wa kutumia mikono na macho ama uchunguzi zaidi wa wa kimaabara.

    Tiba asili ya maumivu ukeni kutoka kwetu

    Kama unaugua maumivu ukeni, Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze tiba mapema. Kabla ya kukupa tiba tutachukua maelezo yako kwanza