Tag: maumivu ya hedhi

tiba asili ya maumivu ya hedhi, hedhi kuvurugika na kukosa hedhi mda mrefu, tiba ya chango

  • Njia Asili kupunguza maumivu ya tumbo la hedhi

    maumivu ya tumbo la hedhi

    BIlashaka unajua kwamba maumivu ya tumbo la hedhi ni kitu kinachokosesha raha na kukera sana kwa wanawake wengi. Maana inaweza kutatiza shughuli zako za kila siku kama masomo, biashara na hata shuguli za kiofisi. Tatizo la maumivu kipindi cha hedhi kwa kitaalamu tunaita dysmennorrhea.

    Tumeandika makala hii yenye uchambuzi wa kina kwa tatizo hili linalowatesa wanawake wengi . Utajifunza chanzo cha tatizo na namna gani utumie njia rahisi nyumbani kwako kupunguza makali ya maumivu wakati unajiandaa kuanza tiba yetu ya uhakika.

    Maumivu ya tumbo ala hedhi ni kitu gani

    Dysmenorrhea ni jina la kitabibu kwa maumivu kipindi cha hedhi. Maumivu ambayo hutokana na kusinyaa kwa misuli ya mji wa mimba. Wakati wa hedhi misuli husinyaa, ili kuruhusu kumeguka kwa ukuta na kutoa damu iliyochanganyika na yai ambalo halikurutubishwa nje. Maumivu haya yamegawanyika katika aina mbili

    Aina Ya Kwanza Ya maumivu ya Kawaida yaani Primary Dysmenorrhea

    Haya maumivu ni ya kawaida kwa wanawake wanapopitia kipindi hiki ambacho hujirudia kila mwezi. Maumivu kikawaida huanza kati ya siku moja ama mbili kabla ya hedhi kuanza kutoka. Mwanamke anaweza kujiskia mamumivu haya kwenye tumbo la chini, kwenye nyonga na kiuno kwa ujumla.

     Maumivu Aina Ya Pili Yasiyo Ya Kawaida yaani Secondary Dysmenorrhea

    Maumivu haya ni kutokana na tatizo fulani la kiafya kweye via vya uzazi vya mwanamke. Changamoto kama vile uvimbe ambayo siyo wa saratani ndani ya mfuko wa mimba uterine fibroids, kukua kwa tishu laini za mfuko wa mimba kuelekea kwenye viungo vingine kama uke na mifuko ya mayai .

    Na pia kupanuka kwa ukuta wa uterus kutokana na kukua kwa tishu za ndani za uterus kuelekea ukuta wa nje (adenomyosis). Maumivu haya pia yasiyo ya kawaida yanaweza kuwa yamesababishwa kwa athari za bacteria ama virusi katika via vya uzazi.

    Kikawaida maumivu haya huanza mapema zaidi wakati wa hedhi ya huchukua muda mrefu zaidi kuisha ukilinganisha na ile aina ya kwanza pale juu. Na pia maumivu haya yanakuwa hayaambatani na kutapika, kuharisha, kizunguzungu wala kukosa nguvu na ganzi.

    Viungo vinavyoathirika zaidi na maumivu ya tumbo la hedhi

    • Via vya uzazi-kama maumivu yako ni kutokana na kukua zaidi kwa tishu za uterus basi maumivu husambaa hadi kwenye tumbo la uzazi.
    • Tumbo la chini-huathirika pia na maumivu haya kwa kiasi kikubwa, kama maumivu haya ni kutokana na kukua kwa tishu za uterus basi mwanamke anahisi kama ameunguzwa na kitu cha moto kwenye tumbo.
    • Maumivu chini ya mgongo- mara nyingi hutokana na kukua kwa tishu za uterus kuelekea kwenye uke na pia kwenye mifuko ya mayai.
    • Miguu– maumivu yanaweza pia kutekea kwenye hips yakishuka chini ya miguu na kufanya mwanamke kushindwa kutembea .
    • Maumivu ya kisaikologia hutokea pia kwa kiwango kukubwa kwa wanawake ambao maumivu yao ni sababu ya vimbe za kizazi. Wanawake hawa wanapata msongo wa mawazo kutokana na kufikiri kwamba
      • Labsa tatizo la uvimbe haliwezi kupona na hakuna dawa
      • Ama hawataweza kupata mtoto kwa siku za baadae
      • Mahusiano ya Rafiki ama wapenzi wao yatavunjika kama wakijua ana tatizo la uvimbe
      • Ama kufikiri jinsi ambavyo hawatafanya kazi zao vizuri na kutofurahia maisha kama mwanzo walipokuwa wazima.

    Nini chanzo cha maumivu ta tumbo la hedhi?

    Maumivu yanatokana na kitendo cha misuli ya kizazikukaza na kusinyaa. Kitendo hiki kinaendeshwa na homoni . Ni kawaida kwa mfuko wa mimba kusinyaa kipindi chote cha mzunguko wa hedhi ambacho huchukua siku 28.

    Lakini utofauti ni kwamba wakati wa kutoa hedhi yenyewe mfuko huu husinyaa na kujikaza zaidi na hivo kukatisha hewa safi ya oyygen kufika kwenye misuli ya mfuko huu wa mimba. Maumivu ni matokeo ya kukosekana kwa muda kwa hewa ya oxygen kwenye baadhi ya misuli ya uterus.

    Huduma ya kwanza/Kitu gani Ufanye ukipata Maumivu ya tumbo la Hedhi

    Kuna njia nyingi ambazo husaidia kupunguza maumivu ya hedhi ambazo unaweza kutumia ukiwa nyumbani kwako pasipo kwenda hospitali. Kama mauvimu ni makali sana unaweza

    • Kumeza dawa za kukata maumivu kama asprini na ibuprofen kwa ahueni ya haraka. Angalizo: dawa za maumivu isiwe ni nia ya kutumika kila mara kwani madhara yake ni makubwa kiafya, dawa hizi zitumike kwa uangalifu.
    • Tumia maji ya uvuguvugu kukandakanda mahali pa tumbo la chini ukiwa umelala chali
    • Usitumie vinywaji na vyakula vyenye caffeine mfano majani ya chai na kahawa na chocolate
    • Fanya masaji kwenye upande wa chini wa mgongo na sehemu ya tumbo la chini.
    • Pumzika zaidi
    • Weka ratiba ya kufanya mazoezi mara kwa mara,wanawake wanaofanya mazoezi hupunguza maumivu ya hedhi kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na wasiofanya mazoezi.

    Lini unatakiwa kwenda hospital kupimwa?

    Kama maumivu yako  ni makali zaidi kuliko kawaida na yanachukua zaidi ya siku 5. Hakikisha unamwona haraka, kwanini?. Kwasababu yawezekana maumivu yako siyo ya kawaida na yaweza kuwa una uvimbe au PID.

    Tiba yetu Asili kutoka india kwa Tsh 85,000/= tu

    Dawa ni asili na zimetengenezwa nchini India kupitia mimea ua Ashoka, Asaparagus na lodh tree na kanchnar . Kwa miaka zaidi ya mitano ambayo tumekuwa tukihudumia wagonjwa wetu wa matatizo ya hedhi na homoni, tumepokea shuhuda lukuki. Ndani ya week mbili utakaa sawa

    Baada ya kutumia tiba zetu tegemea kupata matokeo haya

    • Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi kuisha kabisa
    • Homoni zako kubalansi
    • Mzunguko wa hedhi kurekebika na kuanza kupata kila mwezi
    • Hedhi yako kuwa nyepesi ya kawaida na
    • Kizazi kuimarika sana hata kuongeza chansi ya kushika mimba kama wewe ni muhanga wa kukosa mimba kwa muda mrefu.

    Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze tiba mapema