
Maumivu makati wakati wa kukojoa kitaalamu inaitwa dysuria. Kitendo hichi huwapata zaidi wanawake kuliko wanaume. Maumivu haya mara nyingi hutokana na maambukizi kwenye njia ya mkojo yaani UTI au maambukizi ya magonjwa ya zinaa, lakini pia maumivu haya yanaweza kuashiria tatizo kubwa la kiafya kama saratani au kisukari.
Dalili zingine mbaya zinazoambatana na maumivu wakati wa kukojoa ni pamoja na
- Mkojo kutoka kwa shida sana
- Kujihisi hali ya kuchomachoma wakati wa kukojoa
- Muwasho wakati na baada ya kukojoa
- Mkojo kuwa na rangi ya mawingu
- Kupata mkojo wennye damu , kwa kesi hii ni muhimu kumwona daktari mapema ili ufanyiwe vipimo kugundua chanzo.
Chanzo cha Maumivu Wakati wa Kukojoa
- Maaambukizi ya bakteria kama PID
- Maaambukizi kwenye njia ya mkojo(UTI)
- Kuvimba kwa tishu za ndani za mrija kwa kutolea mkojo
- Kufanya sex kama ugomvi
- Kuosha uke mara kwa mara
- Matumizi ya njia za kupanga uzazi hasa za kuweka ukeni
- Matumizi ya sabuni kuosha ukeni
- Magonjwa ya tezi dume
- Saratani
- Matatizo kwenye figo mfano mawe ya figo
- Lishe mbovu
- Tiba ya Chemotherapy radiotherapy kwa ajili ya saratani
- Vimbe kwenye utumbo mdogo
- Matatizo kwenye kibofu cha mkojo
Kwa watoto mamumivu haya yanaweza kutokana na kitendo cha mkojo kurudi kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo. Mkojo waweza kurudi kutokana na uwepo kwa jeraha au kizuizi kwenye njia ya kutolea mkojo
Watu wanaopata zaidi maumivu wakati wa kukojoa
- Wanawake karibu wote
- Wanawake wajawazito
- Wagonjwa wa kisukari
- Kukua kwa tezi dume
- Kuwa na matatizo kwenye kibofu cha mkojo
- Kufanya ngono bila kutumia kinga, unakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya zinaa.
Huduma ya kwanza wakati unajiandaa kuja kuchukua dawa
- Kunywa maji ya kutosha
Kunywa maji mengi kunasaidia kusatoa nje sumu na taka na hivo kupunguza mamumivu wakati wa kukojoa. hakikisha kila unapopata kiu kunywa maji na siyo soda. - Mafuta ya karafuu
- mafuta ya karafuu yanafahamika kwa kupambana na vimelea wbaya na fangasi na pia kuimarisha kinga ya mwili. Mafuta ya karafuu yasitumike zaidi ya week moja kama unameza.
Angalizo
Kama shida yako ya mamumivu wakati wa kukojoa imetokana na magonjwa ya zinaa, muhimu kwa mwanamke mwenye maambukizi haya kumaliza dozi vizuri ili kuzuia hatari ya kuwa mgumba na maatizo mengine ya uzazi.
Kama tatizo lako limesababishwa mchafuko wa mkojo yaani UTI ni muhimu upige simu haraka tukupe dawa. UTI usipotibu vizuri inaweza kusababisha matatizo kwenye figo.
Leave a Reply