Mbinu za kushika mimba haraka ndani ya mwezi

Written by

in

kushika mimba haraka

Lini ufanye sex ili kushika mimba haraka

Siku nzuri kwa mwanamke kushirki tendo la ndoa ili uongeze uwezekano wa kushika ujauzito ni katika siku za hatari (window period). Siku hizi zinajumuisha siku tano kabla ya siku ya 14 ambapo yai hutolewa,na siku moja baada ya siku ya 14.

Kitendo cha yai kutolewa huitwa ovulation. Kumbuka ili kupata siku ya 14 unahesabu kuanzia pale ulipopata hedhi. Siku ya 14 ni siku ambapo yai hutolewa kwenye ovari na kwenda kusubiri mbegu kwenye mirija ya uzazi.

Siku mbili kabla ya siku ya 14 ni siku zenye uwezekano mkubwa zaidi wa kushika ujauzito. Kwahivo hakikisha unafanya ngono zaidi kwenye kipindi hiki. Yai linapotolewa kwenye ovari linaweza kusubiri kwa masaa 48, lakini mbegu ya kiume inaweza kukaa kwenye kizazi kwa siku mpaka tano kusbiri yai litolewe.

Utajuaje Kama Yai Limetolewa kwenye Mfuko wa Mayai?

Lengo ni mbegu ya kiume ikutane na yai la mwanamke ili urutubishaji ufanyike na mimba itungwe.

Utajuaje kama yai limetolewa kwenye mfuko wa mayai?

Njia ya kwanza ni kuhesabu mpangilio wako wa hedhi kuanzia siku ya kwanza kupata hedhi kwenye mwezi husika. Tumia kalenda kufatilia siku zako. Angalia mzunguko wako kama unachukua siku 28 basi yai hutolewa siku ya 14.

Kumbuka siyo kila mwanamke anapata yai siku ya 14, wengine huwa na mzunguko mrefu zaidi. Kwa kesi hiyo angalia dalili zingine za kutolewa kwa yai kama hizi

  • Kubadilika kwa ute: ute huwa mzito na mweupe kama eneo jeupe la yai.
  • Kupanda kwa joto la mwili (Basal body temperature): Joto la mwili huongezeka taratibu baada ya ovulation. Unaweza kupima mabadiliko ya joto la mwili kwa kutumia kipima joto asubuhi baada tu ya kutoka kitandani. Ili kujipa uhakika fatilia mizunguko mingi ya hedhi upate siku sahihi ambayo yai hutolewa.
  • Ovulation kit: unaweza kutembelea duka la dawa kupata vifaa ambavyo hupima mkojo kujua mabadiliko ya homoni kwenye kipindi hiki cha ovulation.

Staili gani za mapenzi ni Nzuri ili Kushika mimba haraka?

Kumbuka lengo ni kufanikisha mbegu nyingi ziingie kwenye uke na zifikie yai ili mimba iweze kutungwa. Baadhi ya mikao ya kufanya ngono huongeza wingi wa mbegu zinazoingia kwenye uke kuelekea kwenye yai.

Mikao kama kuchuma mboga au mbuzi kagoma yaani (mwanaume kukaa kwa nyuma) na kifo cha mende (mwanaume kukaa juu) husaidia uume kupenya zaidi kiurahisi na hivo kurahisisha mbegu kufika kwenye mlango wa kizazi.

Mbegu za kiume ni waogeleaji wazuri, zinaweza kuogelea mpaka kwenye mlango wa kizazi ndani ya dakika 15. Kuweka mto chini ya mgongo wakati huo unafanya tendo husaidia mbegu kuogelea kwenda kwenye uelekeo sahihi.

Mara ngapi Ufanye Tendo la Ndoa ili Kushika mimba Haraka?

Pengine umewahi kusoma kwamba kufanya ngono kila mara inapunguza wingi wa mbegu na ubora wa mbegu. Baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba mbegu huwa na ubora zaidi kama mwanamume akijizuia kufaya ngono kwa siku mbili mpaka tatu.

Tafiti pia zinaonesha kwamba wanawake hushika zaidi ujauzito wanapofanya ngono kila baada ya siku moja ama mbili.
Kufanya tendo kila siku kwenye siku za hatari itaongeza uwezekano wa mwanamke kushika mimba. Pumzika siku zingine kisha shiriki tendo kwenye siku tano za hatari.

Je Vilainishi vinaweza Kuathiri Uwezekano wako wa Kushika Ujauzito?

Karibu theluthi mbili ya wanawake hutumia vilainishi wakati wa tendo la ndoa ili kupunguza maumivu wakati wa msuguano. Maswali mengi ni je vilainishi hivi vina madhara kwenye mbegu za kiume. Tafiti zinaonesha kwamba vilainishi hupunguza uwezo wa mbegu kuogelea kwa asilimia 40.

Taarifa zingine muhimu ili Kuongeza Uwezekano wa Kushika Ujauzito haraka.

  • Kufika kileleni: kwa mwanaume kumwaga mbegu ni muhimu ili kumpa ujauzito mwanamke. Kwa upande mwingine mwanamke siyo lazima afike kileleni ndipo ashike mimba japo mkao wake baada ya kufika kileleni husaidia mbegu kuogelea kiurahisi.
  • Rekebisha uzito wako: Uzito mkubwa na kitambi ama kuwa mwembamba sana kunapunguza uwezekano wa kushika mimba. Tembelea hapa kupata ushauri na virutubisho ili kupunguza uzito
  • Acha uvutaji wa sigara: Uvutaji sigara kwa mwanaume hupunguza idadi ya mbegu na pia kuongeza hatari ya mimba kuharibika kwa upande wa mwanamke.
  • Punguza matumizi ya vyakula na vinywaji vyenya caffeine mfano kahawa na energy. Zaidi ya vikombe vitano kwa siku hupunguza ubora wa mbegu.

Ni lini Unatakiwa kumwona Daktari.

Endapo umekuwa ukijaribu kutafuta ujauzito kwa muda mrefu bila mafaniko zaidi ya mwaka. Pamoja na kujaribu njia hizi nilizolekeza hapo juu hakikisha unamwona daktari mtaalamu wa magonjwa ya wanawake ili kufanya vipimo kujua chanzo cha tatizo.

Wenza wasilaumiane kwani tatizo linaweza kuwepo kwa kila mmoja.
Wanawake chini ya umri wa miaka 30 wanatakiwa kusubiri walau kwa mwaka mmoja ndipo kumwona daktari. Kama una zaidi ya miaka 30 na unatafuta mtoto bila mafaniko kwa miezi 6 mfululizo hakikisha unamwona daktari haraka.

Magonjwa yanayokwamisha kushika mimba haraka

Kama pia una matatizo haya ya kiafya nenda hospitali haraka iwezekanavyo ufanye vipimo.

Daktari atafatilia historia ya tatizo lako na kukuanzishia huduma ya dawa.

Kipindi unaendelea na tiba ya hospitali hakikisha pia unapata virutubisho kutoka kwenye ofisi yetu iliyopo Dar es salaam, Magomeni Mwembechai, Jengo la Mwembechai Plaza. Vitakusaidia kuongeza chansi ya kushika ujauzito na kuimarisha mbegu kwa mwanaume.

Virutubisho hivi Vinaongeza Chansi kushika mimba haraka endapo umetafuta kwa mda mrefu

Tuandikie kwa namba 0678626254 kupata virutubisho hivi ushike mimba haraka, hasa kama una shida ya hedhi, homoni, kukosa uteute, mirija kuziba na kizazi kichafu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *