Tag: kusafisha kizazi

  • Njia Asili ya Kusafisha kizazi

    kusafisha kizazi

    Kwanini nakushauri kusafisha kizazi?

    Unajua kwamba kusafisha kizazi ni hatua muhimu katika kuuandaa mwili kushika ujauzito. Mfuko wa mimba ni kiungo chenye urefu wa sm 7 na upana wa cm 5. Kiungo hiki kimetengenezwa kwa muunganiko wa kuta tatu.

    Sababu zinazopelekea Kizazi chako Kutoshika mimba na kuchafuka

    Kizazi chako kinafanya kazi muda wote ili kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kiumbe kitakachotungwa. Kazi hizi zinaratibiwa na mpangilio mrefu wa vichocheo ambavyo vinafanya kazi kwa kutegemeana. Kwa hivo kihatarishi chochote ambacho kinavuruga mpangilio huu kinafanya hata uwezo wa kushika mimba kupungua.

    Zifuatazo ni sababu zinapekelea kuharibu afya ya kizazi chako na kuleta ugumba

    Mtindo wa Maisha yaani lifestyle

    Wanawake wanaoishi pasipo kufanya mazoezi na kutumia mda mwingi wakiwa wamekaa, ama shughuli zisizoshugulisha mwili wanakuwa kwenye hatari zaidi ya kupungua uwezo wa kushika mimba. Maisha haya ya kizembe hupelekea kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye via vya uzazi. Kutoshughulisha mwili pia kunapunguza uwezo wa misuli ya kizazi na hivo kupunguza uwezo wa kuhifadhi ujauzito.

    vimbe kwenye kizazi

    Uvimbe kama fibroid unaota mara nyingi kwenye kuta za kizazi na kusababisha maumivu makali wakati wa hedhi. Pia uliwa na fibroid utapata dalili za hedhi nzito na inayochukua mmda mrefu na maumivu ya nyonga.

    Makovu kwenye kizazi chako inachangia kizazi kutoshika mimba na kuharibika: Makovu haya kwenye kizazi yanaweza kufanyika kutokana na sababu mbalimbali

    Sababu zinazopelekea makovu kwenye kizazi

    1. mimba kuharibika yaani miscarriage
    2. Kutoa mimba
    3. upasuaji wakati wa kujifungua
    4. Kutumia kitanzi ili kuzuia mimba
    5. kuugua magonjwa ya zinaa na PID kwa mda mrefu
    6. uvimbe kwenye ukuta wa ndani wa kizazi
    7. Wanawake waliowahi kufanyiwa upasuaji kwenye kizazi wapo kwenye hatari zaidi.
    8. Kuvurugika kwa homoni ni sababau ya wewe kusafisha kizazi

    Utagunduaje kama homoni zako zimevurugika. Angalia uwepo wa dalili hizi

    • hedhi kuvurugika tarehe tofauti kila mwezi
    • kupata hedhi ya muda mrefu zaidi ya siku tano (heavy bleeding)
    • uzito mkubwa na kitambi
    • kuota ndevu na vinyweleo vingi mwilini
    • maumivu makali ya tumbo kipindi cha hedhi
    • kukosa hamu ya tendo la ndoa

    Kizazi kuinama ni sababu kwanini nakupa dawa za kusafisha kizazi

    Kawaida kizazi kinatakiwa kuwa kimenyooka upande wa juu na chini pale mtu akiwa wima. Kutokana na sababu mbalimbali inaweza kupelekea kizazi kuinama kuelekea nyuma au mbele. Tazama picha hapa chini

    Tazama picha kuona Utofauti kati ya kizazi salama-kushoto na kizazi kilichoinama-kulia

    kizazi kuinama

    Kizazi kinaweza kuinama kutokana na kutanuka kwa kwa misuli baada ya kujifungua, makovu na uvimbe kama fibroids na endometriosis. Kizazi kilichoinama kinaweza kuleta dalili kama maumivu makali, kuvurugika kwa hedhi, kuugua UTI mara kwa mara, ugumu kwenye kuvaa pedi na pia maumivu wakati wa tendo la ndoa.

    Jinsi ya kuimarisha kizazi kizazi chako

    Self Fertility Massage: Kufanya msaji eneo ya tumbo chini ya kitovu pande zote kulia na kushoto ni njia moja rahisi ambayo unaweza kuifanya ukiwa nyumbani pasipo gharama. Masaji ya tumbo inasaidia

    Kuimarisha mzunguko wa damu kwenye kizazi,ovari na mirija ya uzazi

    Kusaidia uwiano wa vichocheo

    Kuongeza uwezo wa kizazi kujisafisha kwa kutoa tishu zilizokufa na damu ya hedhi

    Kuimarisha usambazaji wa hewa safi ya oksijeni kwenye kizazi na Kuimarisha misuli ya kizazi.

    Uterus cleansing Package kutoka kwenye kusafisha kizazi

    Dawa hizi asili zinafaa kusafisha kizazi na mirija endapo unatafuta mtoto lakini pia kama ulitoa mimba na kuna mabaki ya uchafu, basi dawa hizi zinafaa pia.Dawa ni za kuweka ukeni, utatumia kwa week mbili.

    Tuandikie kwa namba 0678626254 uanze dozi.

  • Chanzo cha mimba kuharibika

    mimba kuharibika

    Mimba kuharibika ni kitendo cha kupoteza kichanga kwa mama mjamzito kabla ya muda wa kujifungua kufia. Kwa kiasi kkubwa inatokea ndani ya miezi mitatu ya mwanzo baada ya kushika ujauzito. sababu za  mimba kutoka zinatofautiana kwa kila mwanamke. Hapa chini ni dalili kwamba mimba yako imeharibika

    Dalili za Mimba Kuharibika

    • maumivu makali ya tumbo
    • maumivu ya mgongo
    • kuvuja damu nyingi ukeni
    • kutoka kwa tishu za mabongemabonge katika ukena
    • misuli kukaza

    Nini hasa Kinasababisha Mimba kuharibika?

    Wakati wa ujauzito mwili hupeleka virutubisho na vichocheo au homoni kwenye kiumbe kinachokua. Hivi vyote husaidia kiumbe kuwa na afya njema na kukua vizuri. Mimba nyingi zinazoharibika ndani ya miezi mitatu ya kwanza ni kutokana na kiumbe kudumaa. Kuna sababu nyingi zinapelekea Mimba kuharibika mapema kama nilivoeleza hapa chini

    1. Matatizo ya Kiafya: changamoto za kiafya pamoja na mtindo wa maisha unaweza kuletekeza mimba kutoka, hasa kwenye kipindi cha miezi mitatu ya pili yani second trimester. Kumbuka mazoezi ya mwili na kushiriki ngono haiwezi kusababisha mimba kutoka. Mazingira yafuatayo yanaweza kuhataraisha mimba yako
    2. Vinasaba: Karibu 50% ya mimba zinazoharbika kabla ya wakati ni kutokana na makosa kwenye vinasaba
    3. lishe mbaya inayokosa virutubisho  vingi
    4. matumizi ya pombe, madawa na sigara
    5. matatizo kwenye tezi ya shingo yaani thyroid ambayo hayajatibiwa
    6. maambukizi kwenye njia ya uzazi yaani PID
    7. msongo wa mawazo
    8. uzito mkubwa na kitambi
    9. matatizo kwenye mlango wa kizazi
    10. kulegea kwa mfuko wa mimba
    11. shinikizo la damu kuwa juu zaidi na
    12. matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari

    Je unawezaje Kuzuia Mimba Kuharibika?

    • Usifanye kazi ngumu wala kubeba vitu vizito ukiwa na mimba
    • Jikinge na maambukizi kwenye njia ya uzazi kwa kunawa mikono kwa maji safi na kutoambatana na watu wanaoumwa
    • Usitumie pombe, madawa, na kuvuta sigara wakati wa ujauzito
    • Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara ili kuimarisha ukuaji wa kichanga tumboni

    Maelekezo muhimu ya kuzingatia wakati una mimba

    1. Kama una historia ya mimba kuharibika Zaidi ya mimba 3, basi ukishika mimba uasifanye ngono mpaka utakapojifungua
    2. Usipate bodaboda au chombo cha usafiri kinachokurusharusha ni hatari kwa mimba yako
    3. Usitumie vyakula na vinywaji vyenye caffeine kama kahawa wakati wa ujauzito
    4. Kula mlo mzuri wa vitamin ili kuimarisha ukuaji wa kichanga na
    5. Usitumie dawa yoyote kama hujapewa hospitali

    Nini kinatokea baada ya mimba kuharibika

    Baada ya mimba kutoka unaweza kupata dalili hizi

    • Kutokwa na damu ukeni kama damu ya hedhi
    • Maumivu ya tumbo na
    • Kuvimba kwa matiti
    • Mwili utaanza kupata tena hedhi baada ya week 3 mpaka 6 baada ya mimba kutoka

    Kushika Mimba tena Baada ya Mimba ya Awali Kuharibika.

    Kabla hujaamua kushika ujauzito mwingine ni vizuri kuhakikisha mwili uko sawa na afya yako ni njema. Ukiwa na afya njema inapukupunguzia hatari ya mimba nyingine kuharibika.

    Unashauriwa kujipa mda wa kupumzika walau miezi 8 mpaka mwaka mmoja kabla hujaamua kushika ujauzito tena.

    Tiba asili kusafisha kizazi baada ya mimba kutoka

    Unahitaji kutumia dawa hizi asili kusafisha kizazi baada ya mimba kuharbika, ili kukinga na mirija kuziba, Kuugua PID, na pia kulinda kizazi ili mimba zijazo zisiharbike. Gharama ni ndogo sana kusafisha kizai na haina madhara kuliko kusafishwa na vyuma.

    Tuandikie kwa namba zetu 0678626254 uanze tiba