
Kwanini nakushauri kusafisha kizazi?
Unajua kwamba kusafisha kizazi ni hatua muhimu katika kuuandaa mwili kushika ujauzito. Mfuko wa mimba ni kiungo chenye urefu wa sm 7 na upana wa cm 5. Kiungo hiki kimetengenezwa kwa muunganiko wa kuta tatu.
Sababu zinazopelekea Kizazi chako Kutoshika mimba na kuchafuka
Kizazi chako kinafanya kazi muda wote ili kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kiumbe kitakachotungwa. Kazi hizi zinaratibiwa na mpangilio mrefu wa vichocheo ambavyo vinafanya kazi kwa kutegemeana. Kwa hivo kihatarishi chochote ambacho kinavuruga mpangilio huu kinafanya hata uwezo wa kushika mimba kupungua.
Zifuatazo ni sababu zinapekelea kuharibu afya ya kizazi chako na kuleta ugumba
Mtindo wa Maisha yaani lifestyle
Wanawake wanaoishi pasipo kufanya mazoezi na kutumia mda mwingi wakiwa wamekaa, ama shughuli zisizoshugulisha mwili wanakuwa kwenye hatari zaidi ya kupungua uwezo wa kushika mimba. Maisha haya ya kizembe hupelekea kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye via vya uzazi. Kutoshughulisha mwili pia kunapunguza uwezo wa misuli ya kizazi na hivo kupunguza uwezo wa kuhifadhi ujauzito.
vimbe kwenye kizazi
Uvimbe kama fibroid unaota mara nyingi kwenye kuta za kizazi na kusababisha maumivu makali wakati wa hedhi. Pia uliwa na fibroid utapata dalili za hedhi nzito na inayochukua mmda mrefu na maumivu ya nyonga.
Makovu kwenye kizazi chako inachangia kizazi kutoshika mimba na kuharibika: Makovu haya kwenye kizazi yanaweza kufanyika kutokana na sababu mbalimbali
Sababu zinazopelekea makovu kwenye kizazi
- mimba kuharibika yaani miscarriage
- Kutoa mimba
- upasuaji wakati wa kujifungua
- Kutumia kitanzi ili kuzuia mimba
- kuugua magonjwa ya zinaa na PID kwa mda mrefu
- uvimbe kwenye ukuta wa ndani wa kizazi
- Wanawake waliowahi kufanyiwa upasuaji kwenye kizazi wapo kwenye hatari zaidi.
- Kuvurugika kwa homoni ni sababau ya wewe kusafisha kizazi
Utagunduaje kama homoni zako zimevurugika. Angalia uwepo wa dalili hizi
- hedhi kuvurugika tarehe tofauti kila mwezi
- kupata hedhi ya muda mrefu zaidi ya siku tano (heavy bleeding)
- uzito mkubwa na kitambi
- kuota ndevu na vinyweleo vingi mwilini
- maumivu makali ya tumbo kipindi cha hedhi
- kukosa hamu ya tendo la ndoa
Kizazi kuinama ni sababu kwanini nakupa dawa za kusafisha kizazi
Kawaida kizazi kinatakiwa kuwa kimenyooka upande wa juu na chini pale mtu akiwa wima. Kutokana na sababu mbalimbali inaweza kupelekea kizazi kuinama kuelekea nyuma au mbele. Tazama picha hapa chini
Tazama picha kuona Utofauti kati ya kizazi salama-kushoto na kizazi kilichoinama-kulia

Kizazi kinaweza kuinama kutokana na kutanuka kwa kwa misuli baada ya kujifungua, makovu na uvimbe kama fibroids na endometriosis. Kizazi kilichoinama kinaweza kuleta dalili kama maumivu makali, kuvurugika kwa hedhi, kuugua UTI mara kwa mara, ugumu kwenye kuvaa pedi na pia maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Jinsi ya kuimarisha kizazi kizazi chako
Self Fertility Massage: Kufanya msaji eneo ya tumbo chini ya kitovu pande zote kulia na kushoto ni njia moja rahisi ambayo unaweza kuifanya ukiwa nyumbani pasipo gharama. Masaji ya tumbo inasaidia
Kuimarisha mzunguko wa damu kwenye kizazi,ovari na mirija ya uzazi
Kusaidia uwiano wa vichocheo
Kuongeza uwezo wa kizazi kujisafisha kwa kutoa tishu zilizokufa na damu ya hedhi
Kuimarisha usambazaji wa hewa safi ya oksijeni kwenye kizazi na Kuimarisha misuli ya kizazi.
Uterus cleansing Package kutoka kwenye kusafisha kizazi
Dawa hizi asili zinafaa kusafisha kizazi na mirija endapo unatafuta mtoto lakini pia kama ulitoa mimba na kuna mabaki ya uchafu, basi dawa hizi zinafaa pia.Dawa ni za kuweka ukeni, utatumia kwa week mbili.
Leave a Reply