
Mimba kuharibika ni kitendo cha kupoteza kichanga kwa mama mjamzito kabla ya muda wa kujifungua kufia. Kwa kiasi kkubwa inatokea ndani ya miezi mitatu ya mwanzo baada ya kushika ujauzito. sababu za mimba kutoka zinatofautiana kwa kila mwanamke. Hapa chini ni dalili kwamba mimba yako imeharibika
Dalili za Mimba Kuharibika
- maumivu makali ya tumbo
- maumivu ya mgongo
- kuvuja damu nyingi ukeni
- kutoka kwa tishu za mabongemabonge katika ukena
- misuli kukaza
Nini hasa Kinasababisha Mimba kuharibika?
Wakati wa ujauzito mwili hupeleka virutubisho na vichocheo au homoni kwenye kiumbe kinachokua. Hivi vyote husaidia kiumbe kuwa na afya njema na kukua vizuri. Mimba nyingi zinazoharibika ndani ya miezi mitatu ya kwanza ni kutokana na kiumbe kudumaa. Kuna sababu nyingi zinapelekea Mimba kuharibika mapema kama nilivoeleza hapa chini
- Matatizo ya Kiafya: changamoto za kiafya pamoja na mtindo wa maisha unaweza kuletekeza mimba kutoka, hasa kwenye kipindi cha miezi mitatu ya pili yani second trimester. Kumbuka mazoezi ya mwili na kushiriki ngono haiwezi kusababisha mimba kutoka. Mazingira yafuatayo yanaweza kuhataraisha mimba yako
- Vinasaba: Karibu 50% ya mimba zinazoharbika kabla ya wakati ni kutokana na makosa kwenye vinasaba
- lishe mbaya inayokosa virutubisho vingi
- matumizi ya pombe, madawa na sigara
- matatizo kwenye tezi ya shingo yaani thyroid ambayo hayajatibiwa
- maambukizi kwenye njia ya uzazi yaani PID
- msongo wa mawazo
- uzito mkubwa na kitambi
- matatizo kwenye mlango wa kizazi
- kulegea kwa mfuko wa mimba
- shinikizo la damu kuwa juu zaidi na
- matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari
Je unawezaje Kuzuia Mimba Kuharibika?
- Usifanye kazi ngumu wala kubeba vitu vizito ukiwa na mimba
- Jikinge na maambukizi kwenye njia ya uzazi kwa kunawa mikono kwa maji safi na kutoambatana na watu wanaoumwa
- Usitumie pombe, madawa, na kuvuta sigara wakati wa ujauzito
- Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara ili kuimarisha ukuaji wa kichanga tumboni
Maelekezo muhimu ya kuzingatia wakati una mimba
- Kama una historia ya mimba kuharibika Zaidi ya mimba 3, basi ukishika mimba uasifanye ngono mpaka utakapojifungua
- Usipate bodaboda au chombo cha usafiri kinachokurusharusha ni hatari kwa mimba yako
- Usitumie vyakula na vinywaji vyenye caffeine kama kahawa wakati wa ujauzito
- Kula mlo mzuri wa vitamin ili kuimarisha ukuaji wa kichanga na
- Usitumie dawa yoyote kama hujapewa hospitali
Nini kinatokea baada ya mimba kuharibika
Baada ya mimba kutoka unaweza kupata dalili hizi
- Kutokwa na damu ukeni kama damu ya hedhi
- Maumivu ya tumbo na
- Kuvimba kwa matiti
- Mwili utaanza kupata tena hedhi baada ya week 3 mpaka 6 baada ya mimba kutoka
Kushika Mimba tena Baada ya Mimba ya Awali Kuharibika.
Kabla hujaamua kushika ujauzito mwingine ni vizuri kuhakikisha mwili uko sawa na afya yako ni njema. Ukiwa na afya njema inapukupunguzia hatari ya mimba nyingine kuharibika.
Unashauriwa kujipa mda wa kupumzika walau miezi 8 mpaka mwaka mmoja kabla hujaamua kushika ujauzito tena.
Tiba asili kusafisha kizazi baada ya mimba kutoka
Unahitaji kutumia dawa hizi asili kusafisha kizazi baada ya mimba kuharbika, ili kukinga na mirija kuziba, Kuugua PID, na pia kulinda kizazi ili mimba zijazo zisiharbike. Gharama ni ndogo sana kusafisha kizai na haina madhara kuliko kusafishwa na vyuma.
Leave a Reply