Kinga+ Tiba ya Aleji pamoja Ushauri wa daktari

Written by

in

aleji ya ngozi

Mzio yaani aleji ni Matokeo ya uliyopitiliza kati ya mpambano wa kinga ya mwili na kitu chochote ambacho kwa ujumla huwa hakina madhara kwa mwili inapotokea kimeingia ndani ya mwili au kimegusa sehemu fulani ya mwili.

Aleji husababishwa na nini ?

kinga ya mwili huulinda mwili dhidi ya vitu mbalimbali hatari kwa afya kama vile vimelea vya bakteria na virusi, lakini wakati mwingine inaweza kupambana pia na vitu ambavyo havina madhara yeyote kwa mwili ambavyo huitwa allergens. Watu wenye aleji/mzio huwa na hisia zisizo za kawaida za mwili dhidi ya baadhi ya vitu.
Mwili unapokumbana na vitu vinavyosababishia aleji (yaani allergens), mfumo wa kinga ya mwili huzalisha kemikali mbalimbali ikiwemo histamine ambayo hupambana na allergens hizo. Mpambano huu ndo husababisha mtu kuwa na dalili za aleji/mzio kwasababu mpambano unapelekea mwili kureact kama vile umeona adui.

Vinasaba na aleji

Matatizo ya vinasaba pamoja na hali tofauti tofauti za kimazingira zote zinahusika sana katika kusababisha mtu kuwa na aleji. Baadhi ya vitu vinavyosababisha aleji ni pamoja na vumbi, baadhi ya dawa, baadhi ya vyakula, kung’atwa na wadudu kama vile nyuki, aina fulani ya uyoga, vumbi vumbi la maua (pollens) Harufu kama manukato, viungo vya vyakula. Wapo baadhi ya watu ambao hukumbana na mzio pindi wanapokuwa katika mazingira ya joto au baridi wakati wengine hupatwa na mzio pindi wanapopigwa na jua kali. Nyakati zingine hata msuguano kidogo tu wa ngozi unaweza kuwasababishia baadhi ya watu dalili fulani fulani za mzio.

Je aleji inaambukizwa kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto?

Kwa kawaida, aleji ya aina fulani huwa haurithishwi miongoni mwa wanafamilia. Mfano kama mzazi ana aleji na baridi si lazima watoto wake pia wawe na aleji hiyo hiyo ya baridi ingawa wanaweza kuwa na aina nyingine ya aleji. Uwezekano wa mtoto kupata aleji huongezeka zaidi iwapo wazazi wote wawili wana aleji na vitu fulani fulani na huwa mkubwa zaidi iwapo mama ndio mwenye aleji.

Dalili za mtu mwenye ALeji

Dalili za aleji zipo nyingi kuendana na eneo gani la mwili linahusika. Kwa ujumla hizi hapa chini ndio dalili za alajei kufuatana naeneo la mwili.

  1. Mfumo wa hewa: Mtu anaweza kuwa na matatizo katika kupumua (kikohozi au kubanwa na pumzi, makamasi na kuziba kwa pua, muwasho kwenye pua na koo, au kupumua kwa kutoa sauti kama mtu anayepiga filimbi.
  2. Macho: Muhusika hujihisi hali ya kuchoma choma, kutokwa na machozi na muwasho kwenye macho, macho kuvimba na kuwa mekundu
  3. Vyakula: Endapo mtu atakula kitu ambacho ana aleji nacho anaweza kuwa na dalili kama vile kuharisha, kichefuchefu, kutapika, Kusokotwa au kuumwa na tumbo na pia kupoteza fahamu.
  4. Ngozi:Ngozi inaweza kuwa na mabaka mabaka, kubabuka, kuvimba, muwasho, kuota vipele na malengelenge, michubuko au ngozi kuwa nyekundu.
  5. Aleji za mwili mzima: hizi zinakuwa na mkusanyiko wa dalili zote za hapo juu

Vipimo na uchunguzi kugundua aleji

Unapoenda kumwona daktari wa Ngozi utaratibu unaweza kuwa kama nilivoeleza hapa chini

Mgonjwa akiwa na daktari ataulizwa kuhusu historia ya tatizo lake, ni lini lilianza na vitu gani humfanya awe hivyo. Aidha tabibu pia atapenda kufahamu kuhusu dalili nyingine zinazoambatana na tatizo linamlomkabili mgonjwa.

Baadaye vipimo vya aleji vinaweza kufanyika ili kufahamu hasa ni kitu gani mgonjwa ana aleji nacho na kama kweli dalili alizonazo mgonjwa ni kweli zinatokana na aleji au zinatokana na sababu nyingine. Hii ni kwa sababu kuna baadhi ya mambo yanaweza kumsababishia mtu kupatwa na dalili zinazofanana kabisa na mtu aliye na aleji ya kitu fulani.

Je kuna madhara ya aleji?

Madhara ya aleji ni pamoja na kupata shambulio kali la mcharuko wa mwili ambalo linaweza kusababisha kifo kama usipotibiwa haraka. Wapo baadhi ya watu, kwa mfano, wakila wadudu kama senene na kumbi kumbi wanvimba mwili na kushindwa kupumua mpaka kuhitaji kulazwa hospitali na kusaidiwa kupumua kwa mashine. Madhara mengine ni pamoja na shida ya kuvuta pumzi au kushuka kwa shinikizo la damu.

Namna ya kujikinga na Aleji

Pindi mtu anapopatwa na aina fulani ya aleji, kinga bora ni kukwepa mambo yote yanayoweza kuchochea kutokea kwa shambulizi la aleji. Kama ni chakula, jitahidi kukwepa aina hiyo ya chakula na kama ni dawa mf dawa zenye sulphur, acha matumizi yake na pia mueleze daktari wako au muuguzi kuhusu hali hiyo mapema kabla hajakupa dawa hizo.

Je ni kweli Aleji inatibika?

Njia bora kabisa ya kutibu na kupunguza uwezekano wa kupata aleji ni kutambua kitu au vitu vinavyokusababishia hali hiyo na kuviepuka. Kama ni chakula au dawa au kemikali, epuka kabisa matumizi yake, na kama ni vumbi jitahidi kukaa nalo mbali.

Tumia tiba zetu asili kutibu aleji

Kama una aleji, usiache kutucheki kwa namba zetu tukupe ushauri na tiba asili.

Tuandikie kwa WhatsApp namba yetu 0678626254 uanze dozi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *