Category: tiba za kihindi

  • Tiba ya mawe ya figo ndani ya mwezi

    mawe ya figo

    Ugonjwa wa mawe ya figo linaweza kukufanya ushindwe kufanya kazi zako. Kwahivi kuna ulazima wa kutibu tatizo mapema si tu kwa ajili ya kuepusha maumivu bali pia kupunguza hatari ya kufeli kwa figo.

    Mawe ya figo ni tatizo la mfumo wa mkojo linalowatokea watu wengi sana. Inasemekakana kwamba mtu mmoja kati ya kumi atapata tatizo la mawe kwenye figo katika kipindi flani cha maisha yake. Najua umekuwa unawaza jinsi gani upate tiba bila kupata matumaini ndio maana tumeandika makala hii kwa uchambuzi na weledi wa hali ya juu kukupa majibu kwa maswali yako yote.

    Mawe ya figo ni kitu gani hasa?

    Ni vijimawe vidogovidogo sana ambavyo hufanyika ndani ya figo yako, kutokana na muunganiko wa madini na taka mbalimbali ambazo ni matokeo ya kuchujwa kwa mkojo.

    Mawe ya Figo ni Mkusanyiko wa Kemikali

    Mkusanyiko wa kemikali hizi  yaani chemical crystals, wakati mwingine hugandamana na kutengeneza chembechembe ya vitu kama mchanga.

    Kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo vinavyozidi kukua hadi wengine hufikia hatua ya kuziba njia ya mkojo katika figo yenyewe (nephrone) au kwenye mirija yakupeleka mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu (ureter). Hapo ndipo mtu anaanza kupata shida ya kukojoa na kusikia maumivu makali.

    Kufeli kwa figo kutokana na mawe ya figo

    Mawe kwenye figo husababisha kufeli kwa figo ambalo ni tatizo linalotishia uhai wa mtu kama hutapata tiba mapema. Kama unaanza kupata dalili za mawe kwenye figo basi makala hii itakufundisha hatua kwa hatua kuhusu huduma ya kwanza wakati unatafuta pesa uchukue tiba zetu.

    Nitajuaje Kama Tayari Nina Mawe Kwenye Figo?

    Kujua kama tayari una shida ya mawe ya figo tazama uwepo wa dalili hizi

    • Maumivu makali chini ya mbavu zako, maumivu ambayo huja na kuondoka kila baada ya dakika 10 mapaka 15 hasa unapokojoa.
    • Maumivu chini ya mgongo ambayo yanayosambaa mpaka kwenye nyonga
    • Kupata mkojo wenye harufu kali na wenye damu
    • Kuhisi kukojoa kila muda kuliko kawaida wakati mwingine unaweza kwenda haja lakini usitoe mkojo.
    • Maumivu wakati wa usagaji wa chakula tumboni, kutapika na kupata kizunguzungu kikali

    Watu wenye hatari zaidi ya Kupata mawe ya figo

    • Wanaume wapo kwenye hatari zaidi kuliko wanawake
    • Umri wa makamo kuanzia miaka 30 mpaka 50
    • Wanaotumia madawa mbalimbali kwa mda mrefu
    • Waliowahi kuugua magonjwa maka gout, UTI, na matatizo ya tezi ya thyroid na
    • Watu wasiofanya mazoezi, shughuli zao nyingi wanakuwa wamekaa+wenye uzito mkubwa na kitambi

    Hatua Tano Za Kutibu Mawe Kwenye Figo

    1. Hatua Ya Kwanza: Kunywa Maji Ya Kutosha Kila Mara Kama Moja Ya Tiba Ya Mawe Kwenye Figo..
    2. Hatua Ya Pili :Kula Chakula Chenye Virutubisho Vya Kutosha Vyakula vyenye kambakamba/fibers kwa wingi: kwenye mlo wako wek vyakula vingi vyenye kambakamba au nyuzinyuzi mfano karanga, nafaka isiyokobolewa, maharage, mboga za majani, na mbegu. Parachichi, broccoli, na viazi vitamu
      • Mbogamboga za kijani na matunda :tafiti zinasema kwamba watumiaji wa vyakula vya majani kwa wingi kuliko nyma wapo kwenye hatari ndogo zaidi kupata mawe kwenye figo ukilinganisha na walaji wa nyama zilizosindikwa na kuhifadiwa kwenye vifungashio.
      • Vyakua vyenye magnesium na potassium kwa wingi: hii itasaidia kubalance uwepo wa madini ya calcium kwenye mwili, kwahiyo hakikisha unaongeza kweye mlo wako mbogamboga za kijani, matikiti, parachichi na ndizi.
    3. Hatua Ya Tatu: Epuka vinywaji vyenye sukari kwa wingi huongeza ukubwa wa tatizo, hasa soda. Nafaka zilizosindikwa na kusafishwa sana: bidhaa hizi ni kama unga wa ngano, ugali na mikate siyo nzuri
      • Nyama zilizosindikwa: nyama zilizosindikwa husababisha mwili kutoa calcium nyingi n hivo kuongezeka kwa hatari yam awe kutengenezwa kwenye figo.
      • Pombe na vyakula vyenye caffeine: vyakula na vinywaji vyenye caffeine na pombe hupunguza maji kwa kiasi kikubwa kwenye mwili na hivo kuharakisha kufanyika kwa mawe kwenye figo.
    4. Hatua ya nne: Weka Ratiba Ya Kufanya Mazoezi Mara Tatu Kwa Week, ni Tiba Nzuri Ya Mawe Kwenye Figo
    5. Hatua ya tano:Tumia virutubisho mbalimbali na tiba asili zenye ubora

    Tumia tiba zetu asili kutoka india upone mawe kwenye figo ndani ya siku 30. 

    Gharama za dawa ni Tsh 75,000, Chati nasi kwa no 0678626254 uanze tiba mapema

  • Muwasho ukeni na Tiba ya wiki mbili tu

    muwasho ukeni

    Nini husababisha Muwasho ukeni na kuvimba ukeni

    • Kuugua fungus ukeni
    • Maambukizi ya bacteria ukeni
    • kuvurugika kwa uwiano wa viumbe kwenye mazingira ya uke (vaginal microflora) ambayo inahusisha uwepo wa bacteria na fangasi pia
    • Kukoma hedhi ambapo inafanya uke uwe mkavu sana

    Vipimo kwa tatizo la Muwasho ukeni

    Kama tatizo litaendelea na dalili kuwa kali zaidi ya wiki hapo utahitaji kwenda kupima uanze tiba. Dactari atafanya pelvic examnation ambapo atangalia dalili anazopata mgonjwa kwenye via vya uzazi eneo la nje la uke, mfuko wa mimba, mlango wa kizazi, mirija ya uzazi, kibofu cha mkojo na mifuko ya mayai Daktari pia anaweza kuchukua sample ya uchafu unaotoka na kuufanyia vipimo ili kugundua chanzo cha tatizo.

    Tiba ya tatizo hili la kuwasha kwa uke itategemea na chanzo ama ugonjwa unaosababisha kama ugonjwa

    Ushauri wa Kufuata na Tiba Mbadala kama Unapata Muwasho Ukeni.

    1. Epuka kuvaa pedi mds mrefu, kutumia cream na spray zenye harufu kali tabia hizi zinavuruga mazingira ya ukeni na kutoa mwanya wa fangasi na bacteria kukua.
    2. Tumia maji na sabuni zisizo na kemikali kujisafisha ukeni na usioshe uke zaidi ya mara moja kwa siku.
    3. Unapojisafisha ukeni fifute kuanzia mbele kwenda nyuma. Kufanya hizi inazuia kusambaa kwa bacteria walioko mkunduni kwenda ukeni.
    4. Vaa nguo za ndani za pamba ambazo huruhusu hewa kupita na kukausha unyevu ambao ni mbolea kwa fangasi na bacteria wabaya.
    5. Epuka kufanya kusafisha uke kupita kiasi
    6. Tumia condom ili kujikinga na magonjwa ya zinaa
    7. Usifanye sex mpaka pale ukishapona ugonjwa

    Tiba kwa Tatizo la Muwasho ukeni

    Kwa mwanamke mwenye changamoto ya muwasho na harufu mbaya ukeni,hedhi kuvurugika, tunashauri atumie tiba zetu asili kutoka india apone haraka ndani ya wiki mbili

    Tuandikie kwa namba 0678626254 uanze tiba

  • Tiba asili ya Bawasiri Bila upasuaji

    bawasiri

    Je, Unajua Bawasiri nini Nini?

    Bawasiri ni ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya mkundu. Wakati mwingine mishipa hiyo yaweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama. Kitaalamu ugonjwa wa bawasiri tunauita hemorrhoids.

    Aina Za Bawasiri

    Kuna Aina kuu mbili za bawasiri

    (A) Bawasili ya ndani

    Hii ni bawasiri inatokea ndani ya mkundu na huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili kwenye hatua za mwanzo mpaka inakuwa sugu. Bawasiri hii inatokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa adamu za ndani ya mkundu.

    (B)Bawasili ya nje

    Bawasiri hii inatokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa mkundu na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu. Inaweza pia kufanya mishipa ya damu kupasuka na damu kuganda.

    Unajuaje Kama tayari una Bawasiri

    Je wajua unaweza kuwa na bawasiri lakini usipate dalili na baada ya mfupi tatizo likapotea lenyewe. Dalili moja kubwa kwa wagonjwa wetu wengi ni kuvuja kwa damu, na maumivu makali wakati wa kunya.

    Unapoona dalili kama hizi hakikisha unaanza tiba mapema ili usifikie kufanyiwa upasuaji.

    Visababishi Vingine Vya  Ugonjwa wa Bawasiri

    • Kula ngano kila siku
    • Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
    • Kuharisha kwa muda mrefu
    • Kukaa kwenye kiti mda mrefu mf watu wa maofisini
    • Kutumia choo cha kukaa kwa muda mrefu

    Ushauri wa kufuata wakati unatibu bawasili ili upone mapema

    1. Kula mbogamboga za majani, kwenye kila mlo na nafaka ambazo hazijakobolewa
    2. Usijikamue sana unapoenda chooni
    3. Usikae mda mrefu chooni ukijisaidia, hii inaongeza mgandamizo katika eneo la chini kwenye mishipa ya damu na hivo kukuongeza hatari ya kupata bawasili
    4. Tumia dakika 3 mpaka 5, ama subiri mpaka unapokuwa na haja, kama unajiskia kutoa uchafu lakni ukienda chooni kinyesi hakitoki basi tembea tembea ama fanya zoezi la Squats.
    5. Weka barafu sehemu ya haja kubwa kwa dak 10 mpaka 15 kwa siku kupunguza maumivu makali.
    6. Tumia maji ya mmea wa aloe vera kupaka eneo la mkundu kupooaza maumivu

    MUHIMU: Ushauri huu ni kwa ajili ya kupata nafuu ya haraka, hivo hakikisha unafika ofsini kwetu kupata huduma ya dawa na virutubisho, zingatia haya ili kutibu tatizo likaisha kabisa.

    Tiba Asili ya bawasiri Tunayoweza kukupatia ukapona ndani ya wiki mbili

    Dawa hizi ni dawa asili zilizotengenezwa kwa mimea, zinakuwa kwenye mfumo wa vidonge na mafuta mafuta tiba.

    Kumbuka upasuaji kukata nyama siyo suluhisho la kudumu. Njoo uchukue tiba upone na baada ya hapo zingatia ushauri ili tatizo lisijirudie tena

    Tiba yetu inajumuisha vidonge vya asili vya kumeza na mafuta ya kupaka, dozi ya wiki mbili. Usihofu kuhusu gharama maana tunakupa huduma za uhakika kumaliza tatizo lako.

    Kutokana na ukubwa wa tatizo lako tutapendekeza utumie dozi ngapi za dawa.

  • Uvimbe kwenye mayai na Tiba bila upasuaji

    uvimbe kwenye mayai

    Uvimbe kwenye mayai ni Kitu gani

    Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke unatokana na mkusanyiko wa majimaji ndani ya mayai ya mwanamke yaani ovary. Kumbuka uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst.

    Kwa kawaida mwanamke anakuwa na pande mbili ambazo zinazalisha mayai mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya yanapatikana juu pembezoni mwa mfuko wa uzazi.

    Mayai yanakuwa kwenye vifuko vidogo ambavyo hupotea baada ya yai kutolewa kwenye siku za hatari yaani ovulation. inapotokea yai halijatolewa ndipo mifuko hii huanza kujaa maji na kufanya uvimbe. Kumbuka Uvimbe huu unamtokea mwanamke wa umri wowote japo kwa kiasi kikubwa huonekana kwa wanawake waliokoma hedhi.

    Makundi ya wanawake waliopo kwenye hatari Zaidi ya kuugua uvimbe kwenye mayai

    • Kama familia yako huwa wanaugua vimbe kwenye mayai. Kwa wanawake ambao wazazi wao au watu wao wa karibu kama dada na mama wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo kuna uwezekano mkubwa na wewe ukapata huu ugonjwa.
    • mwanamke kuwa mvurugiko wa hedhi.
    • mafuta mengi ama uzito mkubwa na kitambi
    • Kukosa mimba mda mrefu yaani ugumba na
    • kuvunja ungo mapema chini ya miaka 10 ni chanzo cha uvimbe kwenye mayai

    Dalili za kuwa una uvimbe kwenye mayai na unahitaji tiba haraka

    • Kupata maumivu makali ya tumbo kushoto au kulia, ambayo hayana mwanzo maalum na yanayochoma, maumivu yanaweza kuanzia tumboni na kusambaa eneo la makalio
    • Kuhisi tumbo ni zito, limejaa au kuvimba
    • Maumivu kwenye matiti na hedhi isiyokuwa na mpangilio maalum
    • Maumivu ya nyonga wakati wa hedhi hasa chini mgongoni, maumivu yanaweza kuanza muda mfupi tu baada ya kuanza hedhi, wakati wa hedhi au mwisho wa hedhi.
    • Nyonga kuuma sana baada ya kufanya kazi ngumu, mazoezi au baada ya sex
    • Kupatwa na kichefuchefu, kutapika na kutokwa na matone ya damu ukeni siku ambazo siyo za hedhi

    Matibabu ya Uvimbe kwenye Mayai

    Wanawake wengi wenye  vimbe ndogo ndogo lakini kwa sababu hazina shida, hawaendi hospitali kutibiwa . Wanawake hawa wakibeba mimba uvimbe unaongezeka sababu ya mabadiliko ya homoni. Hapo itahitaji kufanyiwa upasuaji wakati wa kutoa mtoto.

    Njia kubwa kutibu uvimbe hospitali kwa ni operation kutoa uvimbe. Endapo kama uvimbe ni mkubwa sana daktari anaweza kupendekeza kutolewa na kizazi.

    Jaribu tiba zetu asili upone kabla ya upasuaji.

    Kama wewe hupendi upasuaji, na unataka kupona kwa njia asili, basi hapa ndio mahali pake sahihi. Tiba zetu asili zinazalishwa nchini India na zimeonesha kuleta matokeo makubwa sana kwa waliotumia. Tumekuwa tukipokea shuhuda nyingi za watu kupona ndani ya mwezi.